Kamanda wa polisi Mbeya, Afande Advocate Nyombi

Na Francis Godwin

WATOTO wawili ndugu wa familia moja wamefariki dunia kwa kuungua moto baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Watoto hao wakazi katika kijiji cha Itindi wilayani Chunya mkoani Mbeya walipoteza maisha wakati wazazi wao wakiwa kilabuni wakiendelea kunywa pombe za kienyeji pasipokujua tukio lililokuwa likiendelea nyumbani kwao.

Kamanda wa polisi mkoani hapo Advocate Nyombi amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Juni Mosi majira ya saa 8 usiku na kuongeza kuwa nyumba iliyoteketea ilikuwa imejengwa kwa miti na kuezekwa nyasi.

Kamanda Nyombi amewataja wato hao kuwa ni Misigala January(4) na John January(2) huku akimtaja baba yao kuwa ni January Mwinyi(33) aliyeacha familia na kukaa kilabuni na mkewe hadi usiku wa manane.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ya moto bado kinachunguzwa ikiwa ni pamoja na thamani halisi ya hasara iliyopatikana kwa nyumba na vitu vilivyokuwa ndani kuteketea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...