Naibu katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya ofisi hizo.
Naibu katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,HAB Mkwizu akiongea na waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika ambayo itafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya ofisi hizo.NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho wa wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa na Afrika yatakayofanyika jijini Dares Salaam kuanzia Juni 20 hadi Juni 23, mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam.
Alisema maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha washiriki zaidi ya 400, taasisi za hapa nchini 160 na kutoka nje ya nchi zaidi ya 50.
Mkwizu aliongeza kuwa maadhimisho hayo yatakuwa ni ya sehemu mbili yaani makongamano yatakayofanyika Mlimani City na maonyesho katika viwanja vya MnaziMmoja.
Alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anyeshughulikia Maendeleo ya Utumishi wa Umma,Haiyan Qian.Pia katika makongamano kutakuwepo wageni mbalimbali.
Pia yataambatana na maadhimisho ya shughuli za maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma ya barani Afrika, yatakayoanza Juni 16,mwaka huu hadi Juni 23,mwaka huu.
Kauli mbiu ya katika makongamano ni ‘Mabadiliko na Ubunifu wa Viongozi katika Utumishi wa Umma Utaleta Maisha Bora’, wakati ya maonyesho ni ‘Mkataba wa Kanuni na Msingi ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni chachu ya Kuimarisha Utoaji Huduma Bora kwa Umma’, ‘Miaka


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...