Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Balozi Ron Kirk amesema kuwa hakuna nchi yoyote katika Afrika ambako kwa sasa Marekani inawekeza muda wake na raslimali nyingi zaidi kuliko Tanzania.
Mwakilishi huyo amesema kuwa mwelekeo huo wa Marekani unatokana na ukweli kuwa Tanzania ni nchi nzuri, tulivu na salama kwa makampuni na taasisi za kibiashara za Marekani kufanya biashara.
Aidha, Balozi Kirk amesema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata mafanikio makubwa zaidi katika miaka ya karibuni na kuwa Marekani inataka kuwa sehemu ya mafanikio hayo.
Balozi Kirk ameyaeleza hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.
Balozi Kirk amemwambia Rais Kikwete kuwa Marekani inafurahia kwa kiwango kikubwa kiwango cha juu cha ushirikiano na uhusiano wake na Tanzania na inapenda kuona ushirikiano na uhusiano huo unakuwa kwa kasi zaidi na haraka zaidi.
“Marekani inafurahia sana uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania. Hakuna nchini nyingine yoyote katika Afrika ambako Marekani inawekeza muda wake na raslimali zake kuliko Tanzania kwa sasa kwa sababu Tanzania ni nchi nzuri kufanya nayo biashara na ushirikiano wa kiuchumi,” amesema Balozi Kirk.
Miongoni mwa maeneo makubwa ya ushirikiano ambako Marekani inaisaidia Tanzania ni kwenye sekta ya kilimo ambako Marekani inasaidia mradi wa uzalishaji chakula wa Feed the Future. Tanzania ni moja ya nchi nne katika Afrika ambazo zimechaguliwa na Marekani kusaidiwa katika mradi huo.
Maeneo mengine ni miradi mikubwa ya MCC katika miundombinu ya umeme, viwanja vya ndege, maji na barabara iliyoanza kutekelezwa kati ya mwaka jana na mwaka huu, miradi mikubwa ya sekta ya afya ya PEPFAR na PMI ya kupambana na magonjwa ya ukimwi na malaria. Tanzania pia ni moja ya nchi zinazonufaika na fursa za AGOA.
Amesema Balozi Kirk: “Sisi katika Marekani tunataka kuwa sehemu ya mafanikio haya ya Tanzania. Tunataka kusaidia kutengeneza nafasi nyingi za kazi, tunataka kuona uwekezaji mkubwa zaidi katika uchumi wa Tanzania, tunataka kuona makampuni mengi na makubwa ya Marekani yakifanya biashara na kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi hii.”
Naye Rais Kikwete ameishukuru Marekani kwa misaada yake ya maendeleo na imani kubwa ambayo nchi hiyo inaonyesha kwa Tanzania na katika maendeleo yake na kumweleza Balozi Kirk kuhusu sekta na maeneo ambako makampuni ya Marekani yanaweza kuwekeza.
Maeneo hayo ni pamoja na utalii hasa katika ujenzi wa hoteli za daraja ya kati, sekta ya madini, sekta ya kilimo, miundombinu hasa ujenzi wa Reli ya Kati na uzalishaji.



Jamani, Watanzania wenzangu, tunalitangaza hili kama jambo jema kwetu...lakini tumefumbwa macho. Tujiulize wanataka nini kwetu? Tusisahau yaliyotokea Iraq. Marekani anakuwa rafiki tu pale anapotimiza matakwa yake, na kinyume na hivyo ni vita!!!!!! China iliannza kuendelea baada ya kuanza kujitegemea na kuondoka na siasa na uchumi wa kuomba omba na ndio maana wapo hapo walipo sasa. Sisi Watanzania tunajuvunia misaada. Tena taarifa kwa vyombo vya habari toka Ikulu...sikutegemea hili kwa kweli..disappointed. Tusipoangalia tutakuja kugeuza Tanzania kuwa uwanja wa Vita baina ya Marekani, Ulaya na nchi za Asia.....maana kila mmoja anataka sehemu yake.
ReplyDeleteTukae macho, hawa jamaa hawana urafiki. Wakikuijia na kuanza kukusifu, basi jua wanalao jambo. Ni kweli TZ ni nchi nzuri,tulivu na salama. Lakini sio kwamba wao hali hiyo wanaifurahia. Kamwe hawana urafiki wala wema. TUNAWAJUA, KWA HIYO TUKAE MKAO WA KULA. SIFA KEMU KEMU NA MISAADA RUFUFU ITATUTOKEA PUANI. Nimemaliza.
ReplyDeleteZubaa uchekwe, kwa nini marekani wanawekeza sana Tanzania wanajua wanapata au kutarajia kupata nini. Tanzania sio tofauti sana na nchi nyingine isipokuwa mwalimu kambarage alitutoa kwenye blanketi, wao wanataka kutufunika, na tumefunikwa, MUNGU IBARIKI TANZANIA, SIO NA VIONGOZI WAKE
ReplyDeleteMKUU WA LIBENEKE BRO MISUPU!! ASILANI SIJAWAHI ONA URAFIKI WA SIMBA NA SWALA.... SUBIRI TUONE TUNAKOPELEKWA SASA, NAHISI SASA WANAWINDA GESI, MAFUTA NA MADINI YETU!!
ReplyDeleteMradi wa Barabara ya Serengeti kwaheri. Kuna maneno yanayosemwa bila kutamkwa. Hapa Balozi anamwambia JK ajue kuwa marekani ni mfadhili wake. Hasiposikiliza analoambiwa anachungulia kaburi. Tegeni masikio. Kama huo mradi haukufa kimya kimya zitapatikana sababu za kuuacha au kuuahirisha.
ReplyDeleteKwani dunia yote alioingia hawa "Caucasians" wanavyojiita wenyewe, ama kawaangamiza wenyeji waliokuwepo, na ametawala yeye au ana maslaha napo na anaingiza kichwa kwanza, mifano ya afrika ipo na wenzetu waarabu keshawavuruga kabisa, hii yote ni mipango yao unafikiri. sasa huyu Gaddafi asietaka mabadiliko na hataki kuondoka atakiona cha mtema kuni. Kingine ni Ugaidi, inaelekea huku Afrika Mashariki kuna chimbuko la magaidi, hivyo kikosi cha ulinzi cha Africa ni uwekezaji mkubwa wanaoutaka, ndio maana hata balozi alieletwa safari ni mwanajeshi. Kaeni chonjo.
ReplyDeletesisi watu wa ajabu sana, kila kinachokuja kwetu lazima tupinge. sasa kama nyie hamtaki wawekezaji kutoka marekani, mnataka wachina? au hao waafrika kusini wanaoiba kila kitu? Acheni kuwa negative bila sababu ya msingi
ReplyDeleteWadau kumbukeni kuwa kule Marekani kuna kundi linaloitwa THINK TANK kazi yao kubwa ni kufikiri namna ya kundanya na kuhadaa Ulimwengu uamini kuwa Marekani ndio nchi bora. VIONGOZI WANATUINGIZA KWENYE KONGWA LA UTUMWA
ReplyDeleteEti kuisaidia TZ kuondowa upungufu wa ajila. Huyo balozi huko kwao wako ndugu zetu na hawana kazi wengine wamerudi hapa nyumbani TZ. Hata hivyo raia wa Marekani hasa (weusi) hawana kazi. Kwa nini asiwasaidie kwanza watu wanchini kwake kuondoa shida ya ajira kabla ya kushughurikia ajila ya TZ. Huyu barozi anataka kutueleza kuwa ana wajali sana waTZ kuliko watu wake. Anadhani anaongea na watoto wadogo. Sisi tunajuwa kuwa wao hawaoni watu wa mataifa mengine kuwa ni binadamu, wao ni mwendo wa kuuwa tu! Mkulu linda Taifa nasi tutalulinda!
ReplyDelete1.Libya kila mtu ana kazi.
ReplyDelete2. watu wa mataifa mbalimbali walikuwa pale kwa kuwa uchumi ulikuwa mzuri sana.
3.Shule bule toka chekechea mpaka mlimami.
4. matibabu hospitalini bure.
5. sehemu iliyokuwa jangwa bwana wa pamba aliibadilisha kuwa yenye rutuba nzuri ya kuzalisha chakula.
5. Aipochukuwa nchi alitaifisha visima vyote vya mafuta vikawa chini ya serikali. Hivyo fedha yote ilikuwa inakwenda serikalini. Hili liliwaudhi sana wakubwa na hasa ndilo kosa kubwa linalowafanya wamshambulie na masilaha makubwa makubwa. OLE WAKO MAMA YANGU TANZANIA, TAFUTA HEKIMA KULIKO MALI.