Wanenguaji wa Twanga Pepeta

African Stars Band "Twanga Pepeta" inataraji kufanya onesho pamoja na msanii Dully Sykes siku ya Jumapili tarehe 12-06-2011 katika Beach ya Mbalamwezi.

Onesho hilo linataraji kufanyika mchana kuanzia saa nne asubuhi kwa kuwa Twanga Pepeta inataraji kufanya onyesho usiku katika ukumbi wT.C.C kama kawaida.

Dully Sykes
Kwa wiki hii Twanga haitofanya onyesho katika Bonanza linalofanyika kila Jumapili kutokana na Viwanja vya Leaders kuwa na shughuli maalum ya michezo ya Basketball siku hiyo.

Badala yake tumehamishia kwa wiki hii Bonanza katika Beach ya Mbalamwezi na kumshirikisha msanii Dully Sykes ili aweze kuongeza burudani kwani mategemeo yetu ni kuvuta mashabiki wa aina nyingi wakiwemo mashabiki wa Dully Sykes.

Baada ya onesho hilo Twanga Pepeta baadae usiku itamalizia kutoa burudani Katika ukumbi wa T.C.C Changombe kwa kuwatambulisha Vimwana kumi walioingia Fainali katika Shindano la Kumtafuta Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.

Martin Sospeter.
Meneja African Stars Band "Twanga Pepeta"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    Huyo wa mwanzo kulia uso ameufanya nini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    Nime - MHAM kweli huyo dada wa katikati wajameni! Shemeji Lwiza naomba namba ya huyo mdada tafadhali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...