Mpiga gitaa mpya wa bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" ,Selemani Shaibu (kushoto) na Miraji Shakashia wakicharaza magitaa katika onyesho la Twanga lililofanyika Bagamoyo tarehe 03-06-2011 katika ukumbi wa Palm Tree Beach Hotel.African Stars Band “Twanga Pepeta” imefanikiwa kumpata mpiga Gitaa la Solo na Rhythm ili kuziba pengo la Adolph Mbinga aliyeondolewa ndani ya Bendi.
Mpiga gitaa huyo ni Selemani Shaibu Aliyetokea kwenye Bendi ya Akudo Impact Selemani ameshaanza kazi rasmi ndani ya Bendi na anataraji kushirikiana vizuri na akina Miraji Shakashia, Godfrey Kanuti, Jojoo Jumanne na Hassan Kado.
Twanga Pepeta kwa sasa ipo kwenye matayarisho ya kukamilisha kurekodi nyimbo 4 ili kukamilisha albamu ya nyimbo sita itakayozinduliwa hapo baadae mwaka huu na Selemani ameshiriki vilivyo kwa baadhi ya nyimbo zilizorekodiwa.
Nyimbo zinazotarajiwa kurekodiwa ni “Dunia Daraja” uliotungwa na Charlz Baba,” Penzi la shemeji” uliotungwa na Mwinjuma Muumini, “Mtoto wa Mwisho” uliotungwa na Ramadhani Athumani au Dogo Rama na “Umenivika Umasikini” wa Luizer Mbutu.
Nyimbo hizi zitaunganishwa na nyingine mbili zilizorekodiwa hapo awali ambazo ni “Kiapo cha Mapenzi” uliotungwa na Saleh Kupaza na “Kauli” uliotungwa na Rogart Hegga wakati huo kabla ya kutimkia katika Bendi ya Extra Bongo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...