Wanahabari na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA nje ya Sentro
 Wanahabari wakipiga gadi Sentro kutwa nzima kusubiri kitachojiri
Kamanda wa mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam
Afande Suleiman Kova akiongea na wanahabari leo
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe bado yuko mbaroni  na Jeshi la Polisi linasema alikamatwa kwa mujibu wa sheria baada ya hati kutolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kutokana na kukiuka masharti ya dhamana yake.

Kamanda wa kanda hiyo Afande Suleiman Kova amesema mahakama inapotoa hati ya kukamatwa mtu yeyote, mahakama hiyohiyo ndiyo inayotakiwa kutoa hati ya mtu huyo kuachiwa huru na siyo polisi wenye mamlaka hayo”.

Kamanda Kova kasema kuwa kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na bunge pia mahakama inapotoa hati ya kukamatwa mtu polisi wanatakiwa kutekeleza na hawaruhusiwa kujadili, hivyo baada ya Mbowe kutiwa mbaroni kinachofanyika ni taratibu za kisheria ili kumpeleka Arusha.

Amesisitiza kwa Wnahabari kuwa inapotolewa hati na mahakama ya kumkamata mtu wao polisi hawawezi kuibatilisha hata awe mtu mwenye cheo gani, na kusisitiza kuwa Mh. Mbowe atapelekwa Arusha na jeshi hilo.

“Nimeshazungumza na viongozi mbalimbali wa upinzani akiwemo Mbowe mwenyewe na kuwaeleza kuhusu wajibu wa polisi na kwa hili jeshi la polisi halina lawama yoyote mana tunatekeleza sheria zilizotungwa na bunge”.

Ameongeza pamoja na kwamba Mbowe alijisalimisha mwenyewe polisi, kukamatwa ni kukamatwa tu haijalishi mtuhumiwa alienda mwenyewe au alikamatwa kwa nguvu na polisi, na kwamba kesho asubuhi  atafikishwa mahakamani Arusha chini ya ulinzi wa polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Hakuna aliye juu ya sheria. Kutokutii amri halali ya mahakama haina uhusiano wowote na ufisadi au siasa. Ni suala la mtu binafsi. Maana anayeshitakiwa hapo sio CHADEMA mbali ni Mbowe na hata akionekana ana hatiya na kufungwa, sio CHADEMA itakachofungwa. Je mbona akina Slaa na Godbless Lema walienda mahakamani na mambo yakaisha????????. Mbowe yeye yuko busy na kutumikia wananchi wakati unatakiwa uende mahakamni. Unakamatwa then unaanza kulalamika siasa, ufisadi, CCM, majungu, nguvu ya umma itumike, n.k. Jamani hata hiyo nguvu ya umma si itaingia hatiani bila tatizo. Mnyika anataka nguvu ya umma ikavamie kituo cha polisi?? Halafu wakipigwa risasi za moto?? Polisi wauaji?? Jamani tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuitisha nguvu ya umma. Itafikia wakati hata jambazi akikatwa kama ni mfuasi wa CHADEMA basi tutahamasisha nguvu ya umma kwenda kumtoa polisi. Je huo ndiyo utakuwa utawala wa sheria ambao CHADEMA inaupigania????? Tujitahidi kufuata sheria na kuepusha harassment zisizokuwa za lazima.
    Mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Ndugu yangu wa hapo Juu,Mbowe hakwenda mahakamani coz alikuwa kwenye shughuli za bunge na kuna sheria ina mlinda mbunge akiwa mbungeni ila kutokana serikali ni ya CCM sikuhizi inajivunjia sheria coz wanasema mbunge yeyote anatakiwa asikamatwe bila barua kupitishwa bunge lakini serikali imekuwa ikijichukulia hatua ,mfano. kwa bwana G.Lema walivyomfanyia na wengineo....Nimemaliza

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    SAFI SANAAAAAAA. DAH nimefurahi sana na khabari hiii,!! huyu mtu anadharau sana! Ankal nakuona na ze fulanazzzzzzzzz kwa mbaaaaali !

    ReplyDelete
  4. mimi siungi mkono kabisaaaa maoni ya CHADEMA kuliona suala la kukamatwa mwkt wao kuwa ni la kisiasa. Alipaswa kuhudhuria mahakamani kama alivyotakiwa lkn kama amekiuka basi alistahili kukamatwa! Hakuna aliye juu ya sheria! Mbona wenzake walikwenda yeye alikuwa wapi?! Wananchi watakaoandamana na kukutana na vijana wa Mwema wakiwa na risasi za moto, shauri yao, wasiwalaumu polisi kwa hilo! Watanzania tuache uvivu wa kufikiri, suala liko wazi kabsaaaa! Tusitumiwe na wanasiasa kwa ajili ya kutimiza matakwa yao! Wajikusanye wao viongozi wa CHADEMA waandamane wenyewe! Wasitusumbue wananchi kwa uzembe wao na kutufanya kuwaacha watoto na wake zatu bila msaada! TAFAKARI.........!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2011

    Si uhutubie huko huko selo. Kwani kuna shida wananchi wako popote pale na walio selo ni wananchi, kazi iendelee mtu wangu, Jeuri ilimsaidia nani, halafu ukiwa mwanasiasa mwenye jazba kama Mbowe anategemea nini. Mwisho mwanamume kweli kweli lazima aonje selo, usijali. Hivi ndio tunaimarisha utawala bora ikifika 2015 akina mwema, kova nje wote.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2011

    Mbowe aache ujeuri na ufedhuli wake. (1) Mtu yoyote akiitwa na mahakama (summons) lazima aitikie wito. Kama ana udhuru lazima aiarifu mahakama mapema. Mbowe is no exception. (2)Sisi wenyeji na wazawa wa Arusha tumeanza kuchoshwa na baadhi ya ndugu zetu wa mkoa jirani ambao wameigeuza Arusha uwanja wa vurugu. Mbona sisi hatuendi Moshi kufanya fujo? (3) Tarehe 5/1/2011, wabunge watatu wa Chadema wa mkoa huo jirani (wa kabila moja)walikuja Arusha kuchochea vurugu. (4) Komeni kuuita mji wa Arusha eti "Moshi B". Naiomba sheria ifuate mkondo wake na safari hii sisi wenyeji wa Arusha tutakuwa macho. Only a fool does not learn from history.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2011

    Ama kweli Mh Freeman amebadilika. Nadhani kuna nguvu za giza za chuki zilizo nyuma yake ndizo zinamfanya awe hivyo. Mh Freeman niliyekuwa namjua hakuwa kabisa na vitimbi vya aina hiyo. Namuombea Mungu amwezeshe ajirudi. Mangelepaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...