Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itafanyika Jumapili (Juni 5, 2011) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili jioni.
 
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange straight and curve), sh. 5,000 kwa VIP C na B na sh. 10,000 kwa VIP A. 

Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Bigbon Msimbazi (Kariakoo), Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Uwanja wa Uhuru, Ubungo OilCom na vituo vya mauzo vya Premier Sports Betting.

 Nigeria itawasili Juni 3 mwaka huu kama ilivyo kwa waamuzi wa mechi hiyo kutoka Kenya na Kamishna kutoka Ethiopia. Mwamuzi ni Sylvester Kirwa ambaye atasaidiwa na Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wakati Kamishna ni Sahilu Gebremariam.
 
Pia TFF kupitia Kurugenzi ya Masoko imepiga marufuku wachuuzi wa viburudisho kwenye mechi hiyo, isipokuwa kwa kampuni maalumu iliyopewa kazi hiyo. Hivyo vijana wote watakaofanya biashara bila kibali cha TFF watakamatwa. Suala hili pia linawahusu wachuuzi wa jezi za timu ya Taifa uwanjani.
 
Kwa habari zaidi za TFF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2011

    Taifa Stars inafika lini hapa jijini Bangui?Tupo watz kadhaa hapa na jirani zetu kadhaa tunataka kuja kuwapokea airport na kuwashangalia siku ya "gemu".TFF tafadhali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...