Afisa Viwango Mkuu wa Shirika la Viwango la Taifa (TBS) Obadiah Msaki akitoa mada kwa wafanyabiasha watakaonyesha bidhaa zao katika maonyesho ya 35 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es salaam juu kuzingatia bidhaa zenye viwango katika maonyesho hayo.
Mratibu wa kusimamia sheria za afya na mazingira Manispaa ya Temeke William Muhemu akitoa mada kwa wafanyabiasha watakaonyesha bidhaa zao katika maonyesho ya 35 ya biashara ya kimataifa Dar es salaam juu ya wajibu wa usalama wa vyakula na usafi wa mazingira katika maonyesho hayo yatakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.
Baadhi ya wafanyabiashara watakaoshiriki maonyesho ya 35 ya biashara ya kimataifa Dar es salaam wakiwa katika semina elekezi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa maonyesho ambayo yataanza rasmi tarehe 28 Juni mwaka huu. Jumla ya Nchi 17 zitashiriki maonyesho ya mwaka huu.picha na Tiganya Vincent, dar es salaam


Hii kali ,chumba cha mkutano wa wafanya biashara wa kimataifa hakina hadhi na ukizingatia joto la bongo!,lakini mkutano wa kuwaandaa warembo huwa unafanyika sehemu maarufu kama Bagamoyo au Kilimanjaro hotel nk.hata vikao vya harusi vinafanyika sehemu nzuri.
ReplyDeletetuzingatie umuhimu wa haya mambo jamani,tuna biashara nyingi za kuzitangaza kutoka Tanzania.
naungana na Annony wa kwanza, semina ya viwango inafanyika katika ukumbi ambao hauna VIWANGO....
ReplyDeleteTuwe makini jamani especially pale tunapofanya vitu vya ngazi ya kimataifa...
Zimebaki wiki mbili tu kabla sabasaba kuanza, lakini Tovuti za Board of External Trade (BET) na ile TANTRADE Tanzania, ambazo zilipaswa ziwe active kutoa maelezo kuhusu sabasaba hii zimelala. Maofisa wapo maofisni wamejaa na kung'ang'ania kuendesha magari makubwa lakini kazi hawataki kufanya. Jamani amkeni, mnategemea maendeleo kwa mtindo huu????!!!! As of now, hakuna mahali popote unapoweza kupata taarifa zozote za uhakika kuhusu sabasaba hii, inakatisha tamaa kweli kweli, Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete