Na Woinde Shizza,Arusha

Watu wanne wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi ya mbele na kupinduka.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea June saba majira ya saa 12:30 jioni katika eneo Mswakini lililopo katika kata ya Makuyuni wilayani Monduli mkoani hapa.

Alibainisha kuwa gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T402 AUX lilikokuwa linaendeshwa na Johnson Kibacha ambaye naye ni marehemu lilipasuka tairi la mbale na kuserereka na mwishowe kupinduka .

Alibainisha kuwa gari hilo ambalo lilikuwa limebaba abiria saba ambapo kwa mujibu wa majeruhi waliiokuwepo katika gari hilo walisema kuwa walikuwa wakitokea jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Manyara.

Mpwapwa aliwataja marehemu ambao walifariki katika ajali hiyo kuwa ni dereva ambaye alimtaja kwa jina la Johnson Kibacha, Judhi Graison,,Jackson Mgema,pamoja na mtu mwingine ambaye yeye alitambulika kwa jina moja la Shuma.

Aliwataja majeruhi kuwa ni Rose Graison,Samweli Mgema pamoja na Joshua Graison ambapo alisema kuwa wote walikuwa ni wenyeji wa jijini Dar es salaam

"kwa kweli kwa haraka haraka nikiangalia inaonyesha dhahiri kuwa watu hawa walikuwa ni ndugu wote kwani hata majina yao ya pili yanaenda na kufanana fanana na walikuwa wametokea jijini Dar es salaam wote"alisema Mpwapwa

Aidha alisema kuwa miili yote ya marehemu imeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti meru huku majeruhi nao wakiwa wamelazwa katika hospitali hiyo hiyo ya mkoa ya mounti meru .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2011

    Mr Mchuzi rekebisha hilo neno kujerulia, au ndio style

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2011

    Mungu awalaze mahali pema marehemu wote na majeruhi wapone haraka jamani hii habari imenisikitisha sana mana waliofariki ni familia moja mume na mke wake pamoja na dada wawili wa mwanaume na walikuwa wanaelekea babati kwenye send of ya mtoto wa dada yao kwa kweli imeniuma sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...