Mkurugenzi wa ZIFF Profesa Martin Mhando akiongea na wanahabari
akiwa meza kuu na wajumbe wa tamasha hilo hoteli ya Southern Sun jijini Dar


MAANDALIZI Tamasha la  14 la  kimataifa la filamu la Zanzibar International Film Festival Festival  (ZIFF) sasa yamesha kamilika ambapo linatarajiwa kuanza  mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa ZIFF Profesa  Martin Mhando amesema kwamba tamasha hilo la mwaka huu litakuwa la aina yake hasa kuzingatia uzoefu walionao tangu lilipoanzishwa.

Profesa Mhando alisema kuwa mwaka huu katika tamasha hilo kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia ikiwa ni pamoja na maonyesho ya wanamuziki wenye majina  na wa Kimataifa kama Shaggy na Oliver Mutukudzi.

Mbali ya wasanii hao pia filamu 71 zitaonyeshwa ikiwamo filamu za hapa nchini. Mhando alisema kutakuwa na filamu za mataufa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoka nchi za Iran movie, Swahili Bongo day na filami nyingine kutoka katika nchi mbalimbali zitaonyeshwa.

Wakati huohuo Mhando ameongeza kuwa kuwa filamu 58  zitashindanishwa na zawadi mbalimbali zitatolewa. Pia amesema kuwa  katika tamasha hilo watatoa tuzo ya heshima kwa marehemu  Hammie Rajab  ambaye alikuwa mtengetezaji wa filamu mzoevu hapa nchini aliyefariki dunia  Aprili 21 mwaka huu.

Mbali ya kuwa  mtengenezaji wa filamu Marehemu Hammie pia alikuwa mwandishi wa  vitabu vya tamthilia  pia aliwahi kufanya kazi  mbalimbali za uandishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...