Abas akiwa amejipumzisha nyumbani kwao.
ABBAS Abdalaah (31) aliapoanza kuvimba uvimbe mdogo katika mguu wake wa kulia hakujua kuwa ulikuwa ni mwanzo wa ugonjwa ambao hatimaye ungemfanya ashindwe kutembea.Ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujulikani, umemfanya Abbas kulala kitandni muda wote akilazimika kubebwa na watu watano kumpeleka nje kujisaidia.
Matumaini aliyokuwa nayo ya kupata tiba ya ugonjwa wake, yameanza kutoweka baada ya msamaria aliyejitokeza kumpeleka Hospitali ya Seliani mjini Arusha kushindwa kutimiza ahadi yake.
Abbas ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, anasema vurugu za wananchi na wawekezaji wa Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, ndizo anaona zimesababisha mpaka sasa asipate msaada.
“Vurugu hizi zilizoaanza Machi mwaka huu , ndizo zilizosabisha leo niwe bado hapa sina msaada, kwani mmoja wa wawekezaji katika Bonde hili alikuwa ameaahidi kunisaidia kunipeleka hospitali ya Seliani," anasema kwa uchungu akiwa amelala katika kitanda chake kilichopo sebuleni kwenye nyumba ndogo ya nyasi ya Bibi yake, Zuhura Abdalah.
Anasema hakuwa na wasiwasi kwamba huo ungekuwa ugonjwa mkubwa ambao ungemfikisha hapo alipo.
Taratibu mguu ulianza kuvimba, hali ambayo ilimfanya baba yake mzazi, mzee Abdallah Juma mwaka 2008, kumpeleka Hospitali ya Hydom, Wilaya ya Mbulu ambako baada ya kumchunguza hawakuona ugonjwa, ingawa mguu ulikuwa umevimba.
“Hydom hawakuona ugonjwa, nikawauliza mbona bado mguu umevimba kwa nini hamuoni tatizo, wakanishauri nirudi nyumbani, “ anasimulia kwa uchungu kijana huyu mchangamfu.
Kupata habari yote nenda Mwananchi
BOFYA HAPA
Allah akbar!.. uncle fanya utaratibu upate account yake tufanye harambee kidogo.
ReplyDeletehuyo kijana jamani Mungu amsaidie apate ufahamu kuwa kafanyiwa mauchawi,hivyo kama tatizo likishindikana hospitali kwa wakristo tunakuwa na imani ya kwenda kwa watumishi wa Mungu kama akina Christopha Mwakasege,mzee wa upako,Gwajima n.k na kukabidhi maisha yetu kwa bwana Yesu then unapokea uponyaji wa kuanzia roho hadi mwili.uponyaji upo na kwa Mambo yote kwa Yesu.akifanya hivo na kuamini atakuja kutushuhudia siku moja kwenye Tv nina imani.atapona kwa jina la Yesu.
ReplyDeleteit look like cancer,muhimbili au kcmc can find solution
ReplyDeleteKwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti ambalo kila goti litapigwa, naamuru ugonjwa alionao Abbas Abdalaah upige goti na utokomee kabisa. Namfunika Abbas kwa damu ishindayo yote ya agano jipya, na mloweka kwenye bwawa la damu iletayo wokovu na kutuweka huru ya Bwana wetu Yesu Kristo.
ReplyDeleteBaba yangu, Mungu wangu, Bwana wangu wewe pekee ndio muumba mbingu na dunia, wewe pekee ndiye mweza wa yote, ndio mjua yote, nakuomba ee Baba basi uende ukamhurumie huyo mwanao uleyemuumba kwa mfano wako na kumwokoa kupita mwana wako mpendwa Yesu Kristo kulingana na agano la Kalvari.
Ee Baba yangu wa mbinguni kazi yako haina makosa, na wewe huumbi kitu au mtu asiye na manufaa, basi Baba kwa mamlaka uliyonipa kupitia mwana wako Yesu Kristo, nasimama kinyume na mipango yote ya yule mwovu shetani na vibaraka wake wote ya kuiba, kuharibu na kusitisha maisha ya Abbas kabla ya wakati wake.
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Ee Yesu mwakozi wangu nakuomba basi ukajifunue kwake Abbas na jamaa zake wote wa karibu ili wapate kukujua wewe na upendo wako kwao, ukatayarishe mapito ya njia zao ili ziwe za kunyooka. Kwa jina takatifu lenye uweza la Yesu Kristo nimeomba. Amen.
Mbarikiwe wote na wewe Issa na timu yako basi Mungu na awazidishie katika kila nyanja ya maisha yenu!
Tunaomba bank account ili tuweze kuchangia
ReplyDeleteNaona watu wa kwa babu wanataka kuleta imani wakati mtu mgonjwa. Kama kawaida, kitoweo kimeonekana na simba anataka kurarua.
ReplyDeleteTatizo bongo hatuna matabibu wazuri kwa sababu ya madesa.
Michuzi, ipatikane acaunti ili watu wachange apelekwe hata india, china au ulaya. Hapo babu na ulokole si mahala pake.
Uchawi? nyie jamaa mnatania siyo?
ReplyDeleteAcheni kuleta udini wenu hapa. Changeni mtu afanyiwe upasuaji india.