Balozi wetu Marekani Mama Mwanaidi Sinare-Maajar na Ankal wakipozi na Supa Modo Veronika Varekova wakati wa lanchi ya usiku aliyoandaa JK Ikulu jijini Dar usiku wa kuamkia leo kwa wawekezaji wa Kimarekani waliokuja Tanzania katika VIP Safari na uwekezaji iliyoandaliwa na ubalozi wetu Washington DC. Veronika pia ni Balozi wa Heshima wa taasisi ya African Wildlife Foundation na keshafanya makubwa katika kuitangaza Tanzania nje baada ya kupanda mlima Kilimanjaro mwaka 2008 na kuvutiwa na wanyama pori. Kwa habari zaidi ya supa modo huyu wa ukweli BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    Michuzi huyu Mrembo sio mwakilishi mzuri wa nchi yetu,anaitangazia kilimanjaro kuwa ipo close to Amboseli national park ya Kenya,hakuna moshi wala Arusha Tanzania,zinazozungumzwa.
    Hata jaribu kupitia blog yake utagundua hio weakness yake,hawa ndio wanaotupa tabu katika kujitetea kuwa Kilimanjaro ipo Tz.

    Mdau na Mzawa USA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2011

    Huyo kweli ni Supamodo. Mzuri kama sanamu. Ankal konoz zilishindikana nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2011

    Nimecheki blog yake naona anatangaza zaidi magorila ya rwanda. Tanzania ameitaja mara moja tuuuu. Lakini tunashukuru hata hicho kidogo alichotutangaza kwenye project yake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2011

    Hawa mamodo hawana elimu sana kwa hiyo, hajui kenya wapi tanzania wapi
    lakini kwa vile amekuja Tanzania ataanza kutangaza Tanzania , mimi
    ninamsamehe .

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2011

    ISSA MMEPENDEZA SAANA. ISSA UREFU 5/6 NA KITAMBI CHA KUVALIA SHATI AU (CHOLESTRO)NA MREBO UREFU 6 NA MWILI WA KUVALIA KANZU AU UMBO LA (VIDONGE VYA VITAMIN 6 TOFAUTI KWA SIKU). ISSA HAPO KUMEKOSEKANA MKEKA/MSWALA NA SHEHE, THEN PILAU NA SODA.

    HUYO ANATUTUMIA TUU KULIPA "THEM BILL'S" NA YEYE ANAJINAFASI "AWF". KUNA CHOMBO CHOCHOTE EITHER CHA SERIKALI YA TANZANIA AU CHA KUJITEGEMEA NGO'S YA TANZANIA KINACHO HAKIKI/RATIBU NA KUJA NA REPORT INAYOONYESHA WAZI KWAMBA HUYU/HAWA MODEL'S WA NJE ANACHANGIA ONGEZEKO LA WATALII NA KWA KIASI GANI ? AU ANACHOFANYA NI KUTUMIWA NA MAJIRANI ZETU (KWA MGOGNGO WA AWF) KUTANGAZA BIASHARA/UTALII WAO KWA KUTUMIA MLIMA KILIMANJARO..?... [TEMBELEA WEB SITE YAKE TAFADHALI NA USOME KWA "MAREFU NA MAPANA"]

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...