Na Woinde Shizza,Arusha
BONANZA la sita la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, linatarajiwa kufanyika Julai 24 katika viwanja vya General Tyre mjini hapa kwa kushirikisha zaidi ya timu 8 ikiwepo timu ya waandishi wa habari wa jijini Dar es Salaam TASWA FC.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha, Mussa Juma, alisema Bonanza hilo, litashirikisha michezo mbali mbali ikiwepo Soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,kucheza muziki na mbio za magunia.
Juma alisema, bonanza hilo ambalo limekuwa likiandaliwa kila mwaka na TASWA Arusha kwa kushirikiana na Kampuni ya Ms Unique,litatanguliwa na semina ya siku moja ya waandishi wa habari .
"maandalizi muhimu ya Bonanza na Semina yanaendelea vizuri ila bado tunaomba wafadhili mbali mbali kujitokeza kudhamini ili kufanikisha mkusanyiko huo wa wanahabari"alisema Juma.
Alisema timu nyingine ambazo zitashiriki katika Tamasha hilo ni timu ya Radio 5, Triplea A, TBL Arusha, Pepsi Arusha, NSSF, NMB Bank, CRDB BANK,Wazee Klabu, timu za vyuo vya uandishi wa habari vilivyopo mkoani Arusha na timu za waandishi wa habari za Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Katibu huyo, alisema hata hivyo bado timu nyingine ambazo zitahitaji kushiriki, zinaweza kuomba na mwisho wa kuomba na kuthibitisha ni Julai 15 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...