Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, Naibu wake Mh. Adama Malima (kulia) na Katibu Mkuu wake Bw. David Jairo, katika moja ya mikutano mingi na wanahabari kuelezea mstakabali wa hali ya umeme nchini
BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ILIYOWASILISHWA NA WAZIRI WILLIAM NGELEJA LEO HUKO BUNGENI DODOMA IMEKATALIWA NA WAHE. WABUNGE NA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA AMEOMBA SERIKALI IPEWE WIKI TATU KUIREKEBISHA NA KUIRUDISHA ISOMWE UPYA.
HII NI MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA BUNGE LA NCHI HATUA HII KUFIKIWA, INGAWA HUKO NYUMA BAJETI KAMA MBILI ZILIONDOLEWA KABLA YA KUSOMWA .
SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AMEAFIKI KUKATALIWA KWA BAJETI HIYO AKIITA NI NYETI NA KUSEMA ITAPOKUJA KUSOMWA TENA IWE NA MAJIBU YA UHALISIA NA MIPANGO INAYOTEKELEZEKA, KWA KUZINGATIA ATHARI AMBAZO WANANCHI NA NCHI YENYEWE INAPATA KUTOKANA NA UKOSEFU WA UMEME.
WENGI WALITEGEMEA KWAMBA WAZIRI NGELEJA KUKAANGWA ILE MBAYA, ILA SIO KUKATALIWA KWA BAJETI NZIMA NA KUTAKIWA IANDIKWE UPYA ILI KIELEWEKE.
----------------------------------------
Wakati huo huo Mhe. Pinda amekuja juu Bungeni na kusema amekasirishwa sana na barua inayosemekana imeandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo ikiwataka maofisa wa Wizara hiyo kuchangia Sh. 50M/- kila idara ili hotuba ya bajeti ipite.
Barua hiyo, iliyoandikwa kwa maofisa ambao majina yao yako kapuni, iliibuliwa na Mbunge wa Kilindi, Mh. Beatrice Shelikindo, na akauliza hizo pesa zingetumika vipi na kwamba ziliagiwa zipelekwe kwenye akaunti ya Geological Survey of Tanzania (GST) benki ya NMB tawi la Dodoma.
Waziri Mkuu aliliambia Bunge kwamba kama anmri ingekuwa yake angemfukuza kazi Bw. Jairo hapo hapo na kusema kitendo alichokifanya kilistahili adhabu hiyo. Ila alisema kwa vike Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumtimua Bw. Jairo atasubiri akipata nafasi ya kuongea nae na kumuomba afanye hivyo.
“Mheshimiwa Rais Kikwete yuko ndami ya ndege hivi sasa akielekea Pretoria, Afrika ya Kusini, hivyo simpati kwa simu ila nitampigia mara tu baada ya kutua na kutulia.
“Kwa manufaa ya Taifa nitamshauri Rais amfukuze kazi Jairo”, alisema huku wabunge wa kambi zote wakimshangilia kwa nguvu.
HABARI KAMILI BAADAYE
Uamuzi wa busara ni kumkataa Waziri.. na siyo kuikataa bajeti.
ReplyDeleteAnasikitika Tanzania bado hawajui maana ya KUWAJIBIKA au kiongozi asipojiona mwenyewe basi hu-WAJIBISHWA.
Angejiuzuru tu!
This is a serious matter now..can we now accept opposition Budget
ReplyDeleteKatibu mkuu wa Wizara afukuzwe kazi mara moja.
ReplyDeleteMheshimiwa Rais niko chini ya miguu yako, naomba umwachishe kazi huyu waziri kwa kifupi kashidwa kazi, wapo vijana wawajibikaji kama Mh. January makamba, hawa ni vijana wenye uchungu na nchi yao na wananchi kwa ujumla, ninaomba sana Mh. Rais huyu mtu hatufai kabisa katika karne hii,hii ni ya mwaka na historiy ya karne
ReplyDeleteoops!!
ReplyDeleteHapa naona njia ni nyeupe kwa Ngeleja. Hivi ni kwanini Ngeleja ang'ang'ania kwenye huo wadhifa. Na JK naye anamwogopa huyu dogo au vipi. Why cant he just fire him or Suck him whatever is suitable to be used. The guy has just proved to be a crap and need to be just told GO. Wakati mwengine heshima huja kwa kuachia ngazi na sio kung'ang'ania mpaka ukataliwe. Mweeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteMdau Sele
Duh!!! Imekaa vibaya
ReplyDeleteIt is a total waste of time. They passed the Mkulo budget which contained alle Ministries estimates ie what the country will spend on each sector. Hawa MPs in mabubu au vipi. Labda wanataka posho zaidi. It is useless presenting each Ministries estimates. The Finance Minister had all covered. Can someone tell me what was Mkulo's budget?
ReplyDeleteTobaaa
ReplyDeleteMakamba?!
We need to be serious at times
walau kwa hili tumpe ushauri wa kufaa Rais.
comedy
ReplyDeletewamekaangwa na mtoto wa bumbuli
ReplyDeleteAnkal naomba nisahihishe siyo sh.50,000/=kama inavyosomeka hapa ni sh.50milioni kwa kila taasisi.
ReplyDeleteHoja yangu:
Haingii akilini katibu mkuu anaandika barua kwenda kwa hizo taasisi kuomba hicho kiasi cha fedha za kuhonga/kutoa rushwa kwa wabunge bila Waziri mwenye dhamana kujua? Huyo Ngeleja anajua huo mchezo wote sema huyo Jairo ndo limemwangukia, ila wote ni wa kutimua pamoja na kurugenzi nzima ya wizara haifai. Hii wizara imeoza,inatakiwa mabadiliko makubwa sana.
Mdau Belgium
Tunawashukuru sana Wabunge kuwa wamoja katika mambo ya kitaifa.Hii imeonyesha kwamba bajeti zote ili zipite kuna kitu kidogo hutolewa kwa baadhi ya wabunge ili kuitetea.Fungueni macho na fuatilieni wizara zote ni rushwa tupu
ReplyDeletesafi sasa nitarudi nyumbani kwa furaha sana nchi inapendeza kuwa na viongozi wenye msimamo,safi waziri mkuu wewe ndie rais mtarajiwaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteNgeleja, Hawezi kazi na aachie ngazi tu....tunataka mtu anayeweza kutatua matatizo sio kuendeleza matatizo. Ngeleja anaendeleza matatizo hapunguzi wala kuondoa. We mtu mpaka anakua tayari kuhonga wabunge ili awafunge midimo mmmhhh? Wasiojiweaza ndio hufanya hayo kama alivofanya yeye na gurupu lake..but still kaumbuliwa....
ReplyDeletehivi bajeti yetu iko kwenye dollars au shillings?
ReplyDelete- - -
buffalo,
new york
Kila Wizara ya Serikali huko nyumbani ina KAMATI YA UFUNDI wakati wa vikao vya Bunge amabazo kazi yake ni kuwadhibiti wale wabunge wenye "kidomodomo" na mara nyingi huongozwa na Makatibu Wakuu, Manaibu au washauri wa Mawaziri. Yanayomfika huyo katibu mkuu ni ajali kazini tu kwani hata hizo Wizara nyingine mfumo ni huo huo.
ReplyDeleteHapo hafukuzwi mtu kazi kutokana na falsafa ya UONGOZI WA PAMOJA.
Massoud, New Albany, OHIO
INGEKUWA NI UKRAINE HAPO NGELEJE ASHAPIGWA MAKONDE NDANI YA BUNGE, MAENDELEO HAYAJI HIVIHIVI, MAENDELEO HAYAHITAJI KUONEANA HAYA WALA KUHESHIMIANA SANA, SASA TANZANIA TUNAENDEKEZA SANA VITU HIVI. YANI NCHI HAINA UMEME,MAJI, USAFIRI TABU!!!! KWELI WATU WANAFANYA MASIHARA. angalia mfano wa Watu wenye Hasira na maendeleo. http://www.youtube.com/watch?v=LXCSdJivHzU
ReplyDeleteLeo ndio naamini kuwa hakuna nchi wala viongozi, wote ni wasanii tu,kumbe ndio wanavyofanya miaka yote,inatia hasira na ni aibu kwa taifa na familia zao.
ReplyDeleteNaomba usiibanie hii kauli ustaadhi,imeniuma sana.
Nchi hii bwana nadhani viongozi wengi wapo kwa ajili ya maslahi binafsi. Ingekuwa kwenye nchi za wenzetu, waziri wa ulinzi (mabomu yalipolipuka) na waziri wa nishati na madini wangekua wamejiuzuru. Ngereja kaboronga mweke pembeni jaribu mwingine, lakini wapi! Kwa nchi hii mambo ya mabomu tuliisha yasahau na hili la umeme tutalizoea litakuwa kitu cha kawaida yaani sehemu ya maisha. Tutaendelea kutembeza bakuli letu kama tulivyozoea. Rasilimali zote tunazo na wasomi tunao wengi tu!!!!
ReplyDeleteKaka Misupu, naomba kuchangia kidogo juu ya kutemwa kwa Bajeti ya Ngeleja.
ReplyDeleteMimi sitamzungumzia Ngeleja ila najikita katika kuwepo kwa uhalali wa kutaifisha na kuvunja mikataba ya taasisi zote ambazo zimechangia hiyo Hela ya kuwahongea Wabunge.
Hapa nchi inatakiwa kuweka kifua mbele kwa kupata sababu tosha ya kuwatimua wanyonyaji wote walikuja kwa jina la uwekezaji kwani ni wazi walioombwa hizo milioni 50 kwa kila taasisi ni wale makampuni makubwa yenye uwezo ambayo yako kwa maslahi yao na hao wapambe wao ambao ndio walioomba kupatiwa hiyo hela.
Mtoa rushwa, mpokeaji na aliiwezesha wote ni wakosaji kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Na sheria za nchi hii zinazuia wawezekezaji wa aina hio kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.
Wahusika siku zote tulikuwa tunaogopa kuvunja mikataba kwa sababu ya kulipa fidia.sasa sababu ni hiyo ya kuvunja bila ya kulipa fidia.
Jamani, bajeti kuu ya mkullo imepita ambayo hii ya ngeleja ipo ndani yake, je na bajeti ya mkulo itabadilika wakati imeshapitishwa?
ReplyDeletePili, katibu mkuu pamoja na kuwa ni mtendaji mkuu, je anafanya maamuzi binafsi bila kumshirikisha waziri, tuacheni kumsulubisha katibu mkuu peke yake yeye ni mtendaji na wakati mwingine oda zinatoka kwa mkuu. Wote wanafaa kuachia ngazi sio katibu mkuu peke yake, ngeleja pia should go.Subordinate wako akifanya kosa kama hili basi wewe mkuu ndio una makosa zaidi maana hujui wanachofanya walio chini yako ambao wewe ndio kiongozi wao.
Aibu yetu milele .... ifmahali maoni ya kitaalamu na wataalamu vihusishwe katika maswala nyeti ya kitaifa. Asasi na jumuiya za wasomi fani za umeme, mikataba na tafiti hususan za nguvu/nishati km mafuta na umeme mko wapiiiiiii?????? nji inaangamia nyie mpo wapiiiii???? je veti vyenu mmevitundika mnavisoma na je vyetu mtathubutu kuwaonyesha !! watauliza Je mlifanya nini kwa nji yenuuu??? TAFAKARI!!
ReplyDelete