Je unatamani kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio?
Je unatamani kuanzisha biashara yako mwenyewe?
Je una wazo la biashara lenye kuhitaji msaada?

Ikiwa ndiyo, tuma maombi ili upate nafasi ya kushinda Dola za Kimarekani 1000 zitakazo kusaidia kuanzisha biashara yako mwenyewe!

Kituo cha Mafunzo ya Uchumi wa Africa (Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza) wana shauku ya kujifunza kuhusu kukua kwa mawazo mapya ya biashara nchini Tanzania. Tunaendesha shindano la mawazo ya biashara kwa wajasiriamali vijana wanaochipukia, na tunataka wewe utume maombi ya kushiriki!

Nani: Maombi ya ushiriki yako wazi kwa mjasiriamali chipukizi yeyote mwenye umri 18-25, mwanamke au mwanaume. (zingatia unaweza kutakiwa kutoa ushahidi wa umri wako)
Nini: Mwezi Julai na Agosti, tutakuwa tunaendesha shindano la kuwazawadia wajasiriamali chipukizi. Unaweza kushinda nafasi ya kuwasilisha na kufafanua wazo lako mbele ya kundi la wafanyabiashara wakubwa wa kitanzania. Wale wenye wazo bora watashinda Dola za kimarekani 1000!

Jinsi gani: Tuma maombi kwenye mtandao (http://www.csae.ox.ac.uk/aspire/tanzania/) Hakuna gharama za kutuma maombi
Lini : Mwisho wa kutuma maombi ni Ijumaa tarehe 17.07.2011, saa 12 jioni. Tutaanza mchakato wa kuchagua katikati ya mwezi wa saba.

KUSHINDA
DOLA ZA KIMAREKANI 1000!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    HAPO NI DOLA 100,000 AU 1000 (ELFU MOJA) KAMA INAVYOONYESHA? TENA MWANDISHI ANASEMA, 'ZITAKAZOKUSAIDIA KUANZISHA BIASHARA YAKO MWENYEWE'. UTAANZISHA BIASHARA GANI NA DOLA 1000? INGESEMA NI MOTIVE YA KUWASHAWISHI VIJANA KUSHIRIKI;NI SAWA;LAKINI SI DOLA 1000 KAMA MTAJI!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2011

    dola 1000? are you serious?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2011

    Hawa ni wahuni tu wanaotaka kuiba mawazo ya wenzio. Msiwape mawazo yenu maana hilo tangazo haliwezi kuhakikishwa kuwa ni la ukweli. Achaneni na wabeba box hao wa UK wamekwama tu hawana deal. Msiwape mawazo wala nini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2011

    Ann.05;37 tuesday, umesema kweli, ni nani Mt atampa Mtz mwenzie pesa? tena hizi wanazopigia box ada, kodi na hata za kuwatumia wazazi wao bongo hawana. Wengine wamekuwa homeless, Na kama kweli wanataka kutoa hizo hela Tz kuna wajane na yatima kibao wapeleke huku. Wezi wa mawazo ya wenzao hakuna chochote. Na msijisumbue kuwapa chochote wachovu tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...