Mshike!mshike washabiki na FFU! Mabakuli ya "Supu ya Mawe" uwanjani kila mmoja na lake!
     
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,kinatarajiwa kutumbuiza  jukwaani tena katika onyesho kubwa la aina yake African Internationals Festival,mjini Tübingen,Ujerumani  leo siku ya jumamosi 16, julai 2011. 
FFU hao wamziki pia wamepakua jikoni wimbo mpya uliobeba jina "SUPU YA MAWE" wimbo wenye ujumbe mahusus kwa walimwengu ,ambao kwa sasa unasikia katika kambi ya FFU  at www.ngoma-africa.com, wimbo huo utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B aka "Mshenzi" wa gitaa la solo.Wimbo huo "Supu ya Mawe"  ujumbe uliomo katika wimbo huo unaonekana kuwa na nguvu na vitamin zote za maisha kuliko kikombe cha dawa.

kutokana na taarifa la gazeti moja la kimataifa hili  
http://www.africa-news.eu/entertainment/44-entertainment/2815-welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany.html   
bendi hiyo maarufu inazidi kupata umaarufu na kujizolea washabiki kiaina yake katika kila kona. 
Usikose kuwasikiliza  at 
www.ngoma-africa.com 
hili nawe upate bakuli la "Supu ya Mawe"
soma habari zaidi:
http://www.theafronews.eu/entertainment/welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...