Juzi jumatano majira ya saa 12 na nusu jioni nilikuwa ndani ya kivuko cha mv magogoni nikitokea kigamboni. Kabla kivuko hakijaanza kuondoka, ghafla kijana mmoja akateremka kutoka kwenye gari aliyokuwamo na akajitosa baharini, jambo ambalo liliaminika kwamba nia yake ilikuwa ni kujitanguliza mbele ya haki.
Ghafla watu wawili walijitokeza wakivua viatu na fulanazz kujiandaa kuchumpa baharini kwa lengo la kumuokoa. Mmoja alichumpa baharini hivyo mtu wa pili akatulia ndani ya kivuko kusubiri.  Huyo mtu wa pili nikamfahamu kuwa ni Lamar, mtayarishaji mziki katika studio ya  Fishcrab. Nilipomuuliza ni vipi Lamar, nini kimetokea baharini; akasema huyo jamaa aliyejitosa baharini ni msanii ambaye walikuwa pamoja huko kigamboni wakishoot video, lakini kijana huyo alikuwa hafati maelekezo ya maproduza na ndipo wakaamua kuacha kurekodi video yake na kurudi mjini. Kwa hiyo kijana kwa hasira akaaumua kutitosa baharini. Ila aliokolewa salama.
Na mdau Kigambonino

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    anahitaji msaada wa uchunguzi wa daktari wa magonjwa yaakili,na akionekana mzima basi ashitakiwe na afungwe kwa jaribio la kujitoa uhai

    ReplyDelete
  2. Hasira za mkizi faida ya mvuvi..ndugu producer huyo msanii bora umtose akatulize akili kwa kutafuta ushauri nasaha laa sivyo atakupa kesi ya kifo bure. wengine ni ma suicidal...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2011

    Kuchumpa? ahhh hapana hapana sikubaliani kabisa, naona sasa kiswahili kinafanyiwa mzaha wa kupita kiasi! khaaa sasa nini maana hasa ya neno chumpa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2011

    duu..anatafuta umaarufu uyo,baada ya kuukosa kwenye iyo video,aliyoshindwa kurecord

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2011

    Wangemwacha anywe mafundo kadhaa ya maji ndo wangemwokoa! hiyo ni vidio tosha kabisa ya muziki wake! LOL

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2011

    naona hapa kiingereza aandike mashaka hata kama kina makosa hakuna atakayesema lakini mwengine yeyote akiandika basi inakua kioja..au wengine mnachukia kiona mwenzenu kaandika kwa lugha nyengine me naona ujumbe ndio wa kuchambuliwa na sio kugha iliotumika...naona hata humu kuna chuki za ubinafsi jamaa anazopigia kelele..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2011

    Angalau kapata kaumaarufu sasa anaonekana dunia nzima. Wahahi huyu ndio mbunifu wa kurekodi!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2011

    Hiyo ndyo ilikuwa scene sahihi ya kufanyia shooting, vocals angeziingiza baada ya kuokolewa, singo hii ingeuzika sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...