Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji bi.Zainab Yusuf Lidandi wakati Rais alipokagua na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nyundo wilaya ya Mtwara vijijini jana jioni.Rais Kikwete yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kukaguana kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mtafiti wa zao la Korosho katika kituo cha utafiti wa Mazao na mafunzo cha Naliendele Mtwara, Dr.Peter Masawe akimpa maelezo Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais kikwete alipokitembelea kituo hicho jana mchana kukagua maendeleo ya tafiti za mazao mbalimbali.Baadaye Rais kikwete alikutana na uongozi wa kituo hicho na kujadili namna ya kuboresha shughuli za kituo hicho muhimu.
Mtafiti wa Muhogo na jamii ya viazi Dr.Geofrey Mkamilo(kulia) akimwonesha Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muhogo ulozalishwa kwa kutumia mbegu bora ya Naliendele wakati Rais alipotembelea kituo cha Mafunzo na utafiti wa mazao huko Naliendele,mkoani Mtwara jana mchana.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyundo Mtwara vijijini jana jioni muda mfupi baada ya kukagua na kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la AMREF(picha na Freddy Maro)
Maji tunataka majumbani sio kubeba ndoo kichwani kila siku!!!!!
ReplyDeletehii so called miradi ya maji ingekuwa inafanya kazi hakuna mtanzania angekuwa na uhaba wa maji.Viongozi wetu waache siasa wafanye vitu kwa maendeleo ya taifa.
ReplyDeleteUsituambie anasalimiana na wananchi sema WATOTO! Ebo!!!
ReplyDeleteWewe anony wa kwanza umenivunja mbavu leo..nimecheka hadi basi.
ReplyDeleteDavid V