Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Kagera,Henry Salewi akiongea na waendesha pikipiki zinazofanya kazi ya kubeba abiria mjini humo,kwenye ukumbi wa jeshi hilo ulioko katika manispaa ya Bukoba, alikuwa akiwaeleza wandesha pikipiki hao waachane na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vitendo vya wizi wa pikipiki vinavyofanywa na watu ambao jeshi hilo limeanza kuwasaka.
waendesha pikipiki wakimsikiliza kwa makini kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera Henry salewi.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ZeroBrainJuly 08, 2011

    Kaka

    Yaani huo ukumbi wao yaani wameshindwa hata kupaka rangi kidogo tu jamani?

    Cheki hapo kwenye dirisha! Khaah!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2011

    Yaani zerobrain kama ulikuwepo ktk brain yangu kwa hicho unachokizungumza maana ndio ninachotaka kukiandika hapa.Unafahamu kuna msururu wa watu ktk jela ambao kuna waliofanya makosa madogodogo ambao walitakiwa wapewe adhabu kama hizo za kusafisha na kupiga rangi hasa ktk vituo vya polisi au majengo ya serikali ambayo ingepunguza gharama za kulipa wafanyakazi.Kuliko kujazana ktk majela mpaka serikali inashindwa jinsi ya kuwashughulikia na matokeo yake wanakuwa ktk hali mbaya ambayo sio ya kiminaadamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...