Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman akisoma hotuba ya makadirio na mapato ya wizara yake,katika mkutano wa Baraza la Wawakilishi huko Mbweni Zanzibar.
Muwakilishi wa jimbo la kikwajuni Mohd Mahamoud Mussa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Wizaraya Kazi Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Ushirika Asha Khalfan nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar. (Picha na Yussuf Simai Habari Maelezo Zanzibar)
NAFISA MADAI HABARI - MAELEZO,ZANZIBAR
Wizara ya kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika, imepanga kutekeleza mambo manne makuu katika kipindi kijacho cha fedha 2011/2012.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake katika baraza la uwakilishi leo,waziri wa wizara hiyo Mhe Haroun ali suleiman ameseama kuwa mipango hiyo ni kuwendeleza na kutanua programu za kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuengeza upatikanaji wa ajira kwa wananchi.
Alisema kuwa wizara yake pia itaimarisha mfumo wa utoaji taarifa pamoja na utekelezaji na uratibu wa sera,sheria na mipango.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa mbali na shughuli hizo mpango huo pia utaweza kuiimarisha uwezo wa wizara katika utekelezaji wa wizara yake.
Akizungumzia suala la ajira amesema kuwa, wizara yake imeandaa miradi mikubwa miwili kwa lengo la kutekeleza sera ya ajira na mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini zanzibar.
Alisema kuwa katika kipindi cha fedha kwa mwaka 2011/2012 wataendeleza sera ya ajira kwa kufanyia marekebisho baadhi ya sheria za kazi, pamoja na kuanzisha na kuzijengea uwezo kamati za kisekta za kukuza ajira katika mikoa na wilaya.
Wazir Haroun amesema kuwa pia wataanza mchakato wa kutayarisha sera ya hifadhi ya jamii kwa kushirikiana na wizara ya fedha na uchumi na wadau wengine wa maendeleo.
Alisisitiza kuwa wizara yake itajitahidi kuongeza fursa zaidi za ajira kwa wazelendo kwa kushirikia na kamati za kimataifa katika kujenga mikakati ya kutengeneza na kuwapatia ajira wanzanzibar na pia kutoa elimu kuhusu ajira kwa kupita njia mbalimbali.
Wizara ya kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika imeliomba baraza hilo kuidhinisha jumla ya TZSbilioni moja, milioni miatano arobaini na tano(tzs 1,545.000,000/=) kwa kipindi cha fedha kwa mwaka 2011/2012.
Mapema Baraza la Uwakilishi lilipitisha bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali baada ya mjadala mkubwa juu ya chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar,(SUZA) kupatia fedha za ziada ili kuondoa tatizo la walimu kukimbia chuo hicho kutokana na mishahara kuwa midogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...