Naibu Waziri Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia)  akizungumza na Mshauri Mwelekezi wa Baraza la Kuu la Michezo Barani Afrika (Supreme Council For Sports in Africa) Luteni Kanali Mstaafu W.D. Mbiya (shoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonald Thadeo(katikati)  jijini Dar es alaam juu ya maandalizi ya michezo ya "all African games". 


Michezo hiyo, ambayo Tanzania itashiriki, itafanyika jijini Maputo nchini Msumbiji kuanzia Septemba 3 hadi 18, ambapo hii itakuwa mara ya tatu kwa nchi iliyo kusini mwa jangwa la Sahara kuandaa. Awali Baraza hilo kuu la Michezo Barani Afrika liliiteua  Lusaka, Zambia, kuwa mwenyeji lakini nchi hiyo ikachomoa kwa kukosa pesa za kutosha, kama ilivyokuwa kwa Ghana ambayo pia ilionesha nia ya kuandaa kabla ya kujitoa baadaye na Msumbiji wakaweka kifua.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO -Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...