Ankali habari za kuendeleza libeneke, nimejaaliwa kuipata picha hii,ambayo ina kumbukumbu kwa wapenzi wa kandanda, hiyo ilikuwa ni Majimaji, mie nimebahatika kumjua huyo wa  nne kushoto ni Golikipa mahiri Isihaka Majaliwa, hao wengine nisaidieni wadau. Msaada kwenye tuta tafadhali wadau...
Mdau Ussama
-------------------------
Ankali nimeweza kupata majina ya baadhi ya hao wachezaji wa majimaji, picha hii ilipigwa uwanja wa sokoine Mbeya  1984 au 1985.Kuanzia kushoto kwenda kulia,Nyoni (Team Manager),Hamisi Malumbo(GK), Andrew Kidulani(marehemu),Isihaka Majaliwa, anaepeana mkono na mgeni rasmi Maj Gen (Rtd) Makame Rashidi Mkuu wa Mkoa Mbeya enzi hizo ni Peter Mhina, Willy Kiango (Marehemu),Emmanuel Mbunga (Marehemu),anaeonekana kichwa ni Rashid Lato, Tofi au Mrope,Abdalah Chuma, Rajabu Muhoza.Majina haya nimepewa na golikipa mkongwe Isihaka Majaliwa anaepatikana mjini Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    Kwa huyo mgeni rasmi ni Balozi Mstaafu Makame Rashid. Anayemfuatia golikipa ni Mtawa Kapalata, anayefuatia kama vile ni Marehemu Rajabu Hoza samahani kama nitakuwa nimekosea kumfananisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2011

    yuko wapi ahmed kampira,samli ayoub

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...