Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (suti nyekundu) akifurahia zawadi ya zulia yenye sura ya Rais jakaya Kikwete aliokabidhiwa na Meneja wa banda la Home Shopping Center Abdallah Shariff alipotembelea banda hilo na kuangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa na HSCkwenye viwanja vya saba saba kilwa road. Julai 4,2011
Mwenyekiti wa Mfuko wa fursa sawa kwa wote (EOTF) mama Anna Mkapa (kushoto) akimuonyesha Mke wa rais Mama Salma Kikwete aina ya kitambaa cha batiki wakati alipotembelea katika banda lao na kuangalia shughuli mbalimbali za wajasiriamali. (juali 4.2011)
Mwenyekiti wa Taasisis ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akiangalia kikapu wakati alipotembelea banda la EOTF katika maonyesho ya biashara (sabasaba)jini Dar es salaam Julai 4,2011. (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya Temeke Chiku Galawa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (suti nyekundu) akiangalia gari liliotengenezwa na VETA ambalo litatumia mionzi ya jua, (SOLA)alipotembelea katika maonyesho ya biashara (77- Julai 4,2011) jijini Dar es Salaam .
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Naibu Waziri wa Wanawake jinsia na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, akitoa neno katika uzinduzi wa Pedi Maalumu uliofanyika . Mh. Mwalimu alimpongeza Mkurugenzi wa kampuni ya Sinyati, ambao ndio wasambazaji wa Pedi hizo kwa jitihada kubwa ya kuwakomboa wanawake wa Tanzania kwani Pedi hizo zimethibitishwa kuwa hazina madhara yoyote kwa watumiaji.
Naibu Waziri wa Wanawake Jinsi na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu, akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usambazaji wa Pedi Maalumu kwa ajili ya wanawake wanaotoka kujifungua jana mchana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sinyati Interprises,Celina Letara, akimuonesha Naibu Waziri namna Ped hizo zinazosambazwa na kampuni ya Sinyati
Naibu Waziri wa Jinsia Wanawake na Watoto akionesha Ped hizo wakati wa uzinduzi uliofanyika jana mchana kwenye Viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara. Picha zote na Mdau Victor Makinda |
Jamani...hebu toeni maelezo ya kutosha kuhusu hiyo TEKNOMAARIFA ya gari kutumia mionzi ya jua. Hivi hamuoni twaweza wapiga bao hao wengine wanaounda magari tukiendeleza ugunduzi na ubunifu wetu?
ReplyDeletewe mwanakombo mbona umesahau dk.?
ReplyDeleteni kazi nzuri ya kujivunia Veta,Vile vile ningependekeza VETA wawe wakishirikishwa kutoa mawazo katika mambo mbalimbali ya usanifu na ujenzi,kwa mfano daraja litakalo jengwa kigamboni kuanzia Dec,pamoja na kuwa na njia tatu kila upande je watembea kwa miguu na baiskeli njia zao zikoje?au wamesaulika?
ReplyDelete