Asalam Aleykum,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE Bw. Mohammed Sharrif anawataarifu kuwa mazishi ya Marehemu Bw. ISIHAKA KIBENE yatakuwa mchana huu.
Marehemu atazikwa huko kwao Masaki, Kisarawe, Pwani. Msafara wa kuelekea Masaki Kisarawe utaondoka nyumbani kwa Marehemu Kinondoni baada ya Swalat Adhuhuri swalat Janaiz itakapokwisha.
Jumuiya ya Watanzania UAE inazidi kumuombea maghfira marehem na Allah amjaalie makazi mema peponi na inatoa pole na kuungana na ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu katika msiba huu.
Jumuiya ya Watanzania UAE inawaarifu Wanajumuiya, Watanzania wote na Marafiki wa Marehemu kutoka mataifa mbalimbali kuwa kutakuwa na HITMA ya Marehemu siku ya Alhamisi tarehe 14 Julai baada ya Swalat Maghribi (siyo I'sha kama ilivyoelezwa awali) kwenye Msikiti wa Zanzibar Rashidiya.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE.
Issa Majid Maggidi
Naibu Katibu Jumuiya ya Watanzania UAE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...