Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue akimpongeza afisa wake Dkt. Justin Seruhere kwa kupata Shahada ya Uzamivu kutoka Commonwealth Open University, United Kingdom ( UK) katika pongezi zake zake akimnukuu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuhusu kauli Mbiu yake " Elimu Haina Mwisho",Balozi amewaasa wafanyakazi na kila mtu kuwa na kiu ya kujiendeleza bila ya kuchoka na kwamba Dkt. Seruhere ameonyesha njia.
Wanadiplomasia kibao walijitokeza kumpongeza Dkt Justin Seruhere, pichani ni Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa, Mhe.Elmi Duale akimpongeza.
Na jirani zetu pia walijumuika nasi, pichani ni Naibu Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Mhe. Josephine Odhiambo, naye akifurahia mafanikio ya Dkt. Jastin Seruhere.
Dkt. Justin Seruhere,Afisa Ubalozi Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, akielezea kwa wageni waalikwa hawapo pichani, alivyoianza safari yake ya kuitafuta Shada ya Uzamivu ( PHD) pembeni yake ni Mai Waifu wake Bibi Leonila Seruhere.
Baadhi ya wageni waaalikwa waliofika kumpongeza Dkt. Seruhele.
Hivi vyuo si ndiyo vipo discredited na research ya Msemakweli Kainarugaba
ReplyDeletePhD haina tatizo maana ni mawazo ya mtu binafsi ambapo wengine hawajaweza kuwaza na ufanye machapisho alau matano ambayo yachapishwe. Ndio maana TZ hatuvumbui kitu chenye kuzalishwa kwenye viwanda maana PhD zetu ni mawazo yasiozalishika zaidi ya kuchapishwa tu kwenye majarida ya wanavyuo.
ReplyDeleteElimu haina mwisho siyo kauli mbiu ya nyerere. Msitake kumpa sifa asiyostahili.
ReplyDeleteKauli mbiu ya nyerere ni "ubepari ni unyama". tehetehehehe.....