Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza moja wapo ya warsha za wabunge wananchama wa Jumuiya ya Madola CPA kuhusu Misingi ya Mabadiliko katika Bunge (Parliamentary Reforms: Raising the Banchmarks) katika Mkutano wa 57 wa CPA unaoendelea London Uingereza . Mhe Ndugai ni Mwakilishi wa Kanda ya Afrika katika katika CPA Dunia.
Mwakilishi wa Wabunge wanawake Afrika Mashariki katika chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) Mhe. Beatrice Shelukindo (Kulia) ambaye pia ni Mbunge katika Bunge la Tanzania akifutilia mada mbalimbali katika warsha ya wabunge wananchama wa Jumuiya ya Madola CPA kuhusu Misingi ya Mabadiliko katika Bunge (Parliamentary Reforms: Raising the Banchmarks) katika Mkutano wa 57 wa CPA unaoendelea London Uingereza. Aliyepembeni ni Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana
Naibu Spika Mhe. Jobe Ndugai (katikati) akifanya mahojiano na Mwandishi wa Ben TV Ayoub Mzee mara baada ya kumalizika kwa warsha ya wabunge wananchama wa Jumuiya ya Madola CPA kuhusu Misingi ya Mabadiliko katika Bunge (Parliamentary Reforms: Raising the Banchmarks) ambaye Mhe. Ndugai alikuwa Mwenyekiti katika Mkutano wa 57 wa CPA unaoendelea London Uingereza . Mhe Ndugai ni Mwakilishi wa Kanda ya Afrika katika katika CPA Dunia. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Kila leo viongozi mbalimbali wa nchi yetu wanatoka kwenda nje kujifunza/kushiriki jinsi wenzetu wanavyopambana na maisha katika serikali zao.
ReplyDeleteAjabu ya viongozi wetu hakuna hata mmoja ambaye kashafanya mabadiliko yoyote kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Nadhani wapo zaidi kwenye manufaa yao binafsi kuliko taifa lililowapeleka.Sioni umuhimu wa misafara ya aina hii ambayo ni upotezwaji wa fedha za walipa kodi.