Ankal Salamaleko,
Samahani naomba msaada kupitia blog yetu pendwa ya jamii. Nakupongeza sana kwa kutukabidhi chombo hichi wakati mwenyewe unabaki kumodereti tu. Yaani ghafla bin vuuup mambo ukiyaweka sawa utakuwa facebook ama twitter yetu wamatumbi. Yaani hadi raha na pia huna mfano wala mshindani. Wengine ni fotokopi tu.
Sasa bwana kuna vijimaneno vya kiingereza ambavyo vinanipaga shida sana, hivyo naomba niambiwe maana ama tafsiri zake kama ifuatavyo.
1. Nephew
2.Cousin
3. Niece
Hivi hawa ni kinanani hasa. Yaani kwa kiswahili tuwaiteje? Halafu kuna hili neno 'owe'. Yaani kama nadaiwa natamkaje na kama nadai nasemagaje. Yaani haya yananichanganya kichizi Naomba msaada tafazali.
Ni hayo tu kwa leo, na endelea na kazi nzuri
Wakatabahu
Mdau Mchopa
Samahani naomba msaada kupitia blog yetu pendwa ya jamii. Nakupongeza sana kwa kutukabidhi chombo hichi wakati mwenyewe unabaki kumodereti tu. Yaani ghafla bin vuuup mambo ukiyaweka sawa utakuwa facebook ama twitter yetu wamatumbi. Yaani hadi raha na pia huna mfano wala mshindani. Wengine ni fotokopi tu.
Sasa bwana kuna vijimaneno vya kiingereza ambavyo vinanipaga shida sana, hivyo naomba niambiwe maana ama tafsiri zake kama ifuatavyo.
1. Nephew
2.Cousin
3. Niece
Hivi hawa ni kinanani hasa. Yaani kwa kiswahili tuwaiteje? Halafu kuna hili neno 'owe'. Yaani kama nadaiwa natamkaje na kama nadai nasemagaje. Yaani haya yananichanganya kichizi Naomba msaada tafazali.
Ni hayo tu kwa leo, na endelea na kazi nzuri
Wakatabahu
Mdau Mchopa
nephew ni mtoto wa kiume wa dada au kaka,niece ni mtoto wa kike wa dada au kaka,cousin ni mtoto wa mama mdogo/mkubwa au mtoto wa baba mdogo/mkubwa.sina uhakika nafikiri mtoto wa mjomba au shangazi pia wa kike niece wa kiume nephew
ReplyDeletenephew -mpwa .mtoto wa dada yako au kaka yako wa kiume
ReplyDeleteniece-mpwa.mtoto wa dada yako au kaka yako wa kike
cousin-binamu
owe-deni
hopes thats help
Nephew = Mpwa = mtoto wa dada yako mfano mjombawako atakuita wewe mpwa uwe wa kike au wa kiume haihu
ReplyDeleteCousin = mtoto wa nduguye babako/mamako
Niece = Kitukuu =mtoto wa mjukuu wako
Kama unanidai utasema .. "I owe you"
Kama ninakudai utasema .." You owe me"
nafikiri itakusaidia kwa sasa, ila kuwa mwangalifu lugha ya kiingereza haiendi kwa kukariri na direct translation
Nephew - Mpwa i.e. mtoto wa dada yako wa kiume ambae atakuita mjomba kama wewe ni mwanaume
ReplyDeleteCousin - Binamu i.e. mtoto wa shangazi yako
Niece - Mpwa i.e. mtoto wa dada yako wa kike ambae atakuita mjomba kama wewe ni mwanaume
Pwa wenzetu wametofautisha wakati wakati sie ni neno moja awe wa kike au kiume
Mdau Igwamanoni wa Itabagumba
Nephew - mtoto wa kiume wa kaka au wa dada
ReplyDeleteNiecce- mtoto wa kike wa kaka au wa dada
cousin- mtoto wa kike au wa kiume wa mjomba au wa shangazi,
Neno owe,lisikupe taabu,kama unajua matumizi ya NINA BUDI AU SINA BUDI kwamba maneno haya yanatumika kama kinyume nyume vile,basi hata neno OWE,litumie hivyo hivyo kwenye kudai au kudaiwa.
http://www.kamusi.org/?q=en/dictionaries
ReplyDeleteAsalaam Aleykum
Miye binafsi napenda sana kusambaza lugha ya kiswahili.
Swahili is my mother tongue na hata hivyo bado kila siku najifunza.
Copy and paste the above link onto your browser
Wakatabahu
Nephew ni mtoto wa kiume wa kaka yako au dada yako au mdogo wako
ReplyDeleteCousin ni binamu
Niece mtoto wa kike wa kaka yako au dada yako au mdogowako
Mdau
ReplyDeleteNephew=Mpwa(Mwanamke) Mtoto wa dada yako
Cousin=Binamu(mtoto wa mjomba au shangazi anaweza kuwa mwanaume au mwanamke)
Niece=Mpwa(Mwanaume) Mtoto wa dada yako
Niece (Mpwa)
ReplyDelete1. a daughter of a person's brother or sister.
2. a daughter of a person's spouse's brother or sister.
Nephew (Mpwa)
1. a son of one's brother or sister.
2. a son of one's spouse's brother or sister.
3. an illegitimate son of a clergyman who has vowed celibacy(used as a euphemism).
Cousin (Binamu)
1. Also called first cousin, full cousin, cousin-german. the son or daughter of an uncle or aunt.
ni hivi mzee
ReplyDeleteNephew-- ni mpwa wako wa kiume (Mtoto wa kiume wa dada/kaka yako)
Cousin---Ni Binamu wako (yaaani Mtoto wa shangazi/mjomba wako)
Niece ---ni mpwa wako wa kike (Mtoto wa kike wa dada yako/kaka yako)
owe--- ni kudai/ kudaiwa
e.g. I owe you Tsh 20 maana yake Unanidai sh 20
You owe me Tsh 20 maana yahe NINAkudai sh 20
ndivyo nijuavyo mm mzee
1. Nephew - = mpwa -mtoto wa kiume
ReplyDelete2.Niece -mpwa lakini wa kike
3. Cousin - binamu ...................upo hapo?
Neno: "owe" ni kudai au kudaiwa hasa "pesa" au kitu cha thamani, sasa jinsi linavyotumika:
Ukisema: I owe him/her - Ananidai
Ukisema: He/she owes me -ninamdai...........Upo hapo?
Neno owe unaweza kulitumia kwenye misemo mbali mbali kama ilivyo kwa kiswahili, unaposema mfano: 1."namdai salamu zangu" 2. najua unanidai sijaja kukutembelea n.k....
Haya bana...najua umepata maana ulizokuwa unazitafuta
1. Nephew = Mpwa (wa kiume)
ReplyDelete2. Niece = Mpwa (wa kike)
2. Cousin = Binamu
Nephew - Mtoto wa KIUME wa kaka au dada yako au mtu yeyote ambae anakuwa kam akaka au dada yako kwa sisi waswahili vile tuna extended (iliyoongeza family) kwa hiyo mtoto kama wa binamu yako vile ni nephew as well. (LA msingi ni nephew inatumika kwa wa kiume tuu)
ReplyDeleteNIECE -ni mtoto wa kike kwa mantiki hayo hayo hapo juu (la msingi NIECE ni wa KIKE tuu)
Cousin -hapa ni binamu yako na nikiwa na maana ya pande zote mbili so mtoto wa mjomba wako,shangazi yako, baba yako mdogo na mama yako mdogo hawa wote ni couzins wako na kama nilivyosema hapo juu kw asisi waswahii na extended family zetu basi mpaka wale jirani zako ambao umekua nao kama ndugu utawaita couzin mbele ya watu wasiowajua zaidi undani wote yote imetoka hiiiyo.
owe -mie mwenyewe bado inanipa utata utumiaji wake na ndio ninaishi huku ughaibuni kulikoanzia hiyo lugha soo hapa siwezi kukusaidia samahani sana......
mdau
Nijuavyo mie niece ni binti wa kaka au dada yako yeye atakuita shangazi , mjomba, baba mdogo au mkubwa, mama mdogo au mkubwa.(Mpwa wa kike)
ReplyDeleteCousin ni binamu kwa maana ya mtoto wa mjomba au shangazi aijalishi jinsi( me or ke)
na Nephew ni mtoto wa kiume wa kaka au dada yako atakuita mjomba au shangazi,baba mdogo au mkubwa, mama mdogo au mkubwa (mpwa wa kiume)
Tafuta kwenye dictionary kwenye mtanda ya English to Swahili utapata majibu yako hapo
ReplyDeletei owe you - unanidai
ReplyDeleteyou owe me - nakudai
NIMEPENDA WACHANGIAJI WOTE KATIKA MADA HII,WATU WAMEONYESHA UELEWA NA UKOMAVU,KILA MAWAZO YA MTU YAMEHESHIMIWA ,HAKUNA LUGHA YA MATUSI HATA KIDOGO,TUENDELEE HIVI HIVI HII NI BLOG YA JAMII ,ASANTENI SANA.
ReplyDeletekazi kweli kweli, job true true.
ReplyDelete= = =
Buffalo,
New York
NIECE - (Mpwa) Mtoto wa Kike wa Kaka au Dada yako..
ReplyDeleteNEPHEW - (Mpwa) Mtoto wa Kiume wa Kaka au Dada yako..
COUSIN - (Binamu)Ni mtoto wa Kike au Kiume wa ndugu wa Baba au Mama
yako...
OWE - Kama unadaiwa inakuwa I Owe You..
Kama unadai inakuwa You Owe Me..
Huo ni mtazamo wangu kwa maelewo yangu lakini mimi siyo mtaalamu wa Lugha
Kaka supu,huyu braza kweli ameishiwa!! na mnaomfahamu msaidieni,atakuwa maralia imemkwea kichwani.Sasa la kujiuliza ni kwamba,umri wote huo haya ni mambo ya kuuliza watu mtandaoni?hapo jirani hakuna shule ya kata? hakuna walimu wa kata?Jamani jamani!!tusiwe washamba kupita kiasi.
ReplyDeleteWswahili bwana!!! Jamaa anataka kujua WANAITWAJE KWA KISWAHILI we unamuambia "mtoto wa kiume wa dada", mtot wa kike wa kaka"!!! Hayo yote ya nini sasa. Badala ya kutafsiri(translate),mnafasiri(Define). Mnachotakiwa mtoe DEFINITION, sio TRANSLATION. Jamaa anajua kabisa kuwa ni mtoto wa mjomba wa kaka au wa dada, sasa kwa kiswahili wanaitwaje?
ReplyDeleteLabda mi nimsaidie kwenye swali analouliza juu ya neno la Kiingereza OWE.
Nalifafanua neno hili kwa kulitungia sentensi:
I owe you ten thousand shillings - Unanidai shilingi elfu kumi.
You owe me ten thousand shillings - Ninakudai shilingi elfu kumi.
Neno hili huwachanganya watu wengi kwa kutaka kufanya tafsiri ya moja.
Nimejaribu kupitia majibu yaliyotolewa kuhusu;
ReplyDeleteNICE, NEPHEW, COUSIN, na OWE ni kagundua kuwa wachangiaji wengi wameeleza vizuri maana ya "Owe" kuliko nahau nyingine.Tatizo limejitokeza baada ya tofauti zinazotokana na tamaduni fulani kujitokeza katika tafsiri. Kwa mfano,wakurya humuita mtoto wa mama mdogo 'Binamu'. Wengine humuita kaka au dada kulingana na jinsia. Tofauti hizo zimeathiri tafsiri zinazotafutwa na kumfanya muuliza swali aanze kuwa makini na baadhi ya majibu. Ili kuondokana na ugumu huo, napendekeza kwamba tafsiri itolewe bila maelezo; mfano Binamu- Cousin, Nephew (Mpwa-Kiume), Niece (Mpwa-kike), bila kutoa ufafanuzi ambao ki-msingi unatokana na mila flani au kabila.
Mzee wa Bondeni kwa Madiba (anayetumia kiswahili ughaibuni).
Wewe uliyedai kuwa muulizaji ameishiwa, mbona unachafua hali ya hewa? Mbona wenzako wamechangia bila ya kumkejeli wala kumtukana muulizaji? Kuuliza siyo ujinga na elimu siyo lazima uipatie tu shuleni. Mimi nimefurahishwa na alivyouliza na namna alivyojibiwa na wadau kwani majibu hayo yatawasaidia hata na watu wengine waliyokuwa hawajui. NA HAYO NI MOJA YA MATUMIZI MAZURI YA MTANDAO.
ReplyDeletehuyu mchangiaji wa jul06;07;47;oo pm anatakakuharibu hali ya hewa woote wachangiaje wamemjibu muuliza swali kistaarabu lakini yeye akataka kuleta zake iliaonekane yeye ni mjuaji zaidi si ungekaa kimya kwani lazima uchangie wote hapo juu wamemjibu vizuri wewe mara maleria mara umri wote huu yote ya nini usiukae kimya kwani lazima uchangie umeniudhi sana watu wengine kwakuvunja wenzie moyo hamjambo
ReplyDeleteAnon wa Jul 07,01:01:00 AM Wakurya hawajakosea kabisa kumuita mtoto wa Mama mdogo BINAMU kwa ufupi ni sisi waswahili ndiyo tunakosea tunapowaita ndugu za wazazi wetu Mama mdogo au Baba mdogo tulitakiwa tuwaite MJOMBA ndugu zote wa kiume waliozaliwa pamoja na wazazi wetu na Kuwaita SHANGAZI wale wote wa Ndugu wa Kike waliozaliwa pamoja na wazazi.. Kwa ufupi ni matumizi mabaya ya lugha au ufahamu ndiyo maana tunawaita Mama Mdogo au Mama Mkubwa, Baba Mdogo au Baba Mkubwa..
ReplyDeletekwa kukurahisishia nianze na neno "owe",tumia njia rahisi tu kulikumbuka jinsi ya kulitumia,PALE KIDOLE CHAKO KINAPOELEKEZEA MARA YA MWISHO,huyo ndiye mdai, mfano kama kidole chako kitakuelekea wewe ukisema 1. you owe "ME" inamaana wewe ndiye mdai, na kama ni 2. i owe "YOU" Yeye ndiye mdai,3.he owe "HIM","HER" "US" "THEM" n.k zingatia tu kidole chako kinaelekea wapi kwa mara ya mwisho.
ReplyDeletekuhusu nephew-hutumika kwa mtoto wa kiume wa ndugu zako wawe wa kiume ama wa kike.
niece-hutumika kwa mtoto wa kike wa ndugu zako wa karibu wakike ama wa kiume9kaka zako,dada zako,kaka au dada wa mkeo/mmeo)
cousine-huyu ni mtoto wa kike ama wa kiume wa ndugu za baba yako au mama yako,hawa ndugu kwa kimombo wale wote wa jinsia ya kiume huitwa uncle,na wa jinsia ya kike huitwa auntie, sio kama sisi waswahili tutavyo baba mdogo/mkubwa,mama mdogo/mkubwa, then ndo shangazi na mjomba la hasha!kimombo ni mjomba/shangazi full stop. ndiyo maana kwa kimombo huwezi kumuita kijana wa kaka wa baba yako BROTHER au SISTER, hawa ni cousine tu.na huyo mzee ni uncle tu kama kawaida.
nadhani imekuwa clear.
hivo vyo basi;
nephew-mpwa wa kiume,
niece-mpwa wa kike.
cousine-binamu wakike au wa kiume.
Dr.phillip