Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), inapenda kuutarifu Umma juu ya Meli ya MV Serengeti kupata hitilafu ilipokuwa safarini.

Mnamo tarehe 14 Julai 2011 Meli ya abiria na mizigo MV Serengeti iliyosajiliwa Zanzibar, iliondoka katika Bandari ya Zanzibar, majira ya saa 3 usiku kuelekea Pemba ikiwa na abiria wapatao 810 pamoja na mizigo.

Moja ya injini ya Meli hii ilipata hitilafu ikiwa safarini na kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Vikosi vya ulinzi na uokoaji, viliandaliwa ili kukabiliana na dharura yoyote ambayo ingeweza kutokea kutokana na hitilafu hiyo.

 Hata hivyo kwa mwendo mdogo, Meli hiyo iliweza kuendelea na safari kwa kutumia injini moja, na kuwasili Pemba katika Bandari ya Mkoani saa 4: 35 asubuhi badala ya saa 12 asubuhi leo tarehe 15 Julai 2011 kama ingesafiri kwa mwendo wake wa kawaida, hivyo kuchelewa kwa takribani kwa saa tano hivi.

Abiria wote pamoja na mabaharia waliokuwamo chomboni walishuka salama.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu
SUMATRA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2011

    hivi kwani sumatra inapanua mbawa zake hadi zanzibar?nakumbuka ya kuwa zanzibar walilipinga sana hili na ikapelekea kutunga sheria yake iliyozaa zanzibar marinetine authority!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2011

    Kwani usafiri wa majini uko chini ya muungano?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2011

    Ankal aliyekutumia ujumbe huu, kichwa cha habari sio kiswahili sahihi, kwani kinaonyesha kutabiri kwa MV serengeti kupatwa kwa hitilafu!
    Nafikiri kiswahili sahihi ni MV SERENGETI ILIPATWA NA HITILAFU IKIWA SAFARINI. Hebu tujitahidi tusiharibu kiswahili chetu.
    Ni mimi mwalimu wa Africa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...