Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea tuzo ya ushiriki katika uandishi wa kitabu kiitwacho “The Evolution of Commonwealth Parliamentary Democracy: The CPA at 100” kutoka kwa Mwenyekiti wa CPA Dunia Mhe Mohamed Shafie Apdal, (Mb) Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya madola CPA na waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Malaysia katika Mkutano Mkuu wa 57 wa chama hicho uliofanyika London Uingereza. Mhe. Makinda amenadika mada iitwayo “ The transition from One party to Multiparty Democracy in Africa” ambapo jumla ya mada 31 zimeandikwa katika kitabu hicho na wabunge na maspika Mbalimbali Dunian. Kutoka Tanzania Mhe. John Momose Cheyo naye ameandika Makala katika kitabu hicho iitwayo “Parliamentary Finacila Scrunity”.
Mhe. Mussa Azan Zungu akipokea kwa akipokea tuzo ya ushiriki katika uandishi wa kitabu kiitwacho The Evolution of Commonwealth Parliamentary Democracy: The CPA at 100” kwa niaba ya Mhe. John Cheyo aliyeandika makala iitwayo “Parliamentary Finacila Scrunity” kutoka kwa Mwenyekiti wa CPA Dunia Mhe Mohamed Shafie Apdal, (Mb) Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya madola CPA na waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Malaysia katika Mkutano Mkuu wa 57 wa chama hicho uliofanyika London Uingereza. Jumla ya mada 31 zimeandikwa katika kitabu hicho na wabunge na Maspika Mbalimbali Duniani.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa mwaka wa 57 wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya madola (CPA) wakijadili jambo mara baada ya kumalizika hotuba ya katibu Mkuu wa Chama hicho DKt William Shija (hayupo Pichani) wakati wa mkutano Mkuu wa chama hicho Jijini London jana. Ujumbe huo umeongozwa na Mhe. Anne Makinda, Spika wa Bunge, na wabunge ambao ni Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Beatrice Shelukindo, Mhe. Zungu na katibu wa Msafara Said yakubu.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na Spika wa Bunge la India (Lok sabha) Mhe. Meira Kumar wakipongezana mara baada ya kutunukiwa tuzo za uandishi wa kitabu kiitwacho “The Evolution of Commonwealth Parliamentary Democracy: The CPA at 100” katika Mkutano wa mwaka wa 57 Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya madola (CPA) ambapo Mhe. Makinda amenadika mada iitwayo “ The transition from One party to Multiparty Democracy in Africa” na Meira Kumar ameadika mada iitwayo “ India Democracy ”. Picha na owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    Mkono wa kulia wa Zitto unafanyajee tena hapo?(Utani)

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2011

    acha wapate fursa ya kujinafasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...