Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd,David Mgwasa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu mjini Dodoma.uzinduzi huo umefanyika katika ya New Dodoma,mjini humo hivi karibuni.Katikati ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Phillipo Mulugo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mheshimiwa Phillipo Mulugo akizungumza wakati akizindua rasmi mpango huo.
Picha ya pamoja na Wanafunzi walioingia katika mpango huo.

TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) wanazindua rasmi mpango maalum wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu mjini Dodoma, ikiwa ni mpango madhubuti wa kuchangia katika maendeleo ya wakulima husika, na kutilia mkazo Elimu, ukitegemea kuwa mtoto aliyesoma atakuwa na msaada mkubwa kwa mzazi mkulima, na pamoja na nia ya kutimiza azma ya “kilimo kwanza” kwa vitendo. Mpango huu unajulikana kama ZABIBU NA SHULE KWANZA.

Uzinduzi huo ulifanywa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Phillipo Mulugo (MB) New Dodoma Hotel,mjini Dodoma.

Mpango huu unatazamiwa kusomesha watoto wasiopungua 500 katika ngazi ya elimu ya sekondari , ukitegemea kuungaana na mpango wa sasa, wa kusoma Chuo Kikuu kwa njia ya bursary kutoka serikalini. Kwa kuanzia, watoto 50 watachaguliwa katika kipindi kinachoanzia Julai 2011 na Januari 2012, watoto 10 tayari wameshachaguliwa ambao watalipiwa ada pamoja na mahitaji yote ya shule kwa kipindi cha miaka minne (4) ya elimu yao ya Sekondari kama inavyoonyesha hapo chini.

Zabibu na Shule Kwanza ni mpango utakaofanya kazi kwa karibu na vikundi mbali mbali ili kuhakikisha unafanikiwa na unaendelea kudumu kwa kipindi kirefu kama ilivyodhamiriwa. Vikundi hivi ni pamoja na:

Vyama vya wakulima wa Zabibu.
Wizara ya Elimu mkoani Dodoma.
Wizara ya Elimu Kitaifa
Wabunge wa majimbo ya mkoa wa Dodoma
Viongozi wa ngazi ya kijiji na wilaya.
Shule za sekondari na vyuo.
Wazazi na watoto husika.

Vikundi hivi vitatengeneza kamati ya uchaguzi wa wanafunzi kwenye program ya ZABIBU NA SHULE KWANZA, ambayo itasaidia kufanikisha kupatikana kwa watoto sahihi na kuhakikisha wanasoma kwa bidii zote kwa kipindi chote.

Ili kupata nafasi ya kuchaguliwa kwenye mpango huu ni lazima yafuatayo yatazingatiwa:

Mtoto ni lazima awe ameandikishwa kwenye programu.
Mtoto ni lazima awe anatoka kwenye familia ya wakulima wa zabibu.
Mtoto awe amefaulu kuendelea na masomo ya Sekondari.
Mtoto awe ameteuliwa kuendelea na sekondari ila hakuweza kupata shule.
Mtoto anaefanya vizuri zaidi kwenye Nyanja zote shuleni anaweza kuingizwa kwenye mpango wa watoto wenye vipaji maalum (kutokana na mapendekezo ya jumuia ya Elimu).
Ni lazima mtoto awe Mtanzania.
Kipaumbele kitapewa kwa watoto wanaotoka katika familia zilizo na hali duni kimaisha, mzazi mmoja, bila wazazi, Mzazi mgonjwa, mzazi mwenye ulemavu.

TDL imeweka mpango madhubuti kuhakikisha ya kwamba watakaofaidika na programu hii ni watoto halali na wanaostahili kuingia kwenye mpango huu. Mipango hiyo ni pamoja na;

Usajili wa kudumu wa watoto wote wa wakulima walio katika shule za msingi pamoja na wazazi wao.
Kamati ya program hii, itahakikisha waliosajiliwa wote ni watoto wanaotoka kwenye familia halali, kutokana na vigezo vilivyotajwa hapo juu.
Kamati itatumia majibu kutoka ofisi ya elimu mkoa, katika kutoa nafasi ya uchaguzi wa watoto kuingia kwenye program hii.

Kamati itaweka mipango na shule watakazo kwenda watoto ili kupata ripoti za maendeleo ya mwanafunzi, ili kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri kwa minajili ya kuweza kupata matokeo bora zaidi.
Kwa watakaoshindwa kumudu masomo na baada ya jitihada zote za kuwasaidia kushindikana, Kamati italazimika kuwaondoa kwenye programu na kutoa nafasi kwa mtoto mwengine mwenye bidii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...