Habari Ankal Michuzi,

Naomba uweke huu ujumbe kwenye Blogu ya Jamii ili wadau waweze kuupata na kuona namna hali ilivyombaya huko kwa wazungu.kiukweli ninamachungu sana na mawazo yasiyoisha kwa sasa hivi kutokana shambulio la OSLO .

Bwana Anders Behring Breivil ametoa ujumbe ambao kwa kweli unatisha kwa ndugu zetu waafrika wanaoishi Ulaya,sio tu waafrika bali pia waarabu,wahindi,waturuki,wapakistan na wageni wote wanaohamia nchi nyingine kwenda kuishi kwa ajili ya maisha bora.

Nimepitia habari moja ya bwana Anders anayomlaani mkenya aliyechaguliwa kwenye mashindano ya muziki ya ulaya akiwakilisha Norway.

TUJE KUONA UJUMBE WA ANDERS KWA WAGENI WANAOKAA ULAYA,YEYE ANAWAKILISHA.

1-Hataki watu wasio wazungu kupata vibali na kuishi Ulaya,hiyo ni sera ya kila mtu duniani kukataa wageni kuishi nchini kwake kama mfano mzuri ni Afrika kusini walipowaua waafrika wenzao.

2-Hataki watu wa dini nyingine maana ulaya ni nchi za kikristo,mifano ipo mingi kama UK wananchi walifanya maandamano ya kuzuia kujengwa msikiti jiji la Birmingham Dudley.

FUNDISHO KWA watu wote wanaoishi UGHAIBUNI ni kwamba hata kama unaishi sawa na hao jamaa na unashirikiana nao ujue kwamba sehemu isiyo ya wazazi wako yaani baba na mama kama sio wazungu au mmoja ni mzungu na wewe ni muhindi au umezaliwa ulaya na wazazi wako wote ni wageni bado utabaguliwa tu kwa hiyo huo ni ujumbe kwa kila mtu awe muhindi,mwafrika,mchina kukaa katika nchi isiyo yako ni utumwa maana unaweza ukafanyiwa kitu kibaya wakati wowote.

Mdau Mpinga Ubaguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    ni kweli mdau mpinga ubagazi ni hatari kukaa nchi iso yako kama ulivyosema lakini mbona watanzania wanafanyiwa ubaya na unyama na serikali yao wenyewe na wapo nchini mwao? yale ni mambo yametokea na mtu yule mwenye akili za kinyama ila sio kwamba wazungu wote wako hivyo. ni moja ya matukio y kishenzi duniani kama hatari kuishi ni popote pale.. serikali ya tanzania inauwa waandamanaji, inafunga watu bila ya makosa na ni nchi yao

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2011

    Ni kweli kabisaq binafsi nipo masomoni hapa Norway nimekutana na baadhi ya wa Tanzania ambao wamebahatika kupata watoto na dada zetu kutoka Tanzania kitu ambacho nimekifurahiya lakini ukiwa unaongea nao wazazi wa watoto hao unakuta wanajisifia kwa watoto wao ni Blacks Norway na sio Norway tu hata kule sweden ndio kuna baadhi ya wa Tanzania kwa bahati mabya au ukosefu wa elimu wametokea kuamoni watoto wao waliozaa nao na wanawake kutoka Tanzania au sehemu nyingine za Afrika kuwa wao ni sawa na waswidi lakini wakati utatueleza

    Mdao masomoni Norway

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2011

    Popote tu utauwawa, watu wanauwawa bongo tu kwa kijisimu cha mkononi. Haturudi ng'oooooooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2011

    ndo dunia hiyo usiogope mdau ukitaka ishi popote hamna shida , yule ana upungufu wa akili tu, huwei ua watu wako mwenyewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2011

    NAZANI AMEAMUA KUFWATA UTARATIBU AMBAO UPONCHI ZA KIARABU-MAANA HATA IRAQ NA KWINGINEKO HAWAPENDI WAGENI HASA WALE WA DINI TOFAUTI NA YAO-INAFIKIA HATUA WANACHOMA MAKANISA NA KUUA WATU

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2011

    Basi na wao wazungu waondoke Afrika kiishe. Kila mtu akae kwao. Tutashirikiana na wachina tu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2011

    Hii issue ni kubwa kuliko mnayozania. Mimi niko masomoni Netherlands, chama tawala kimekuwa kikipinga waziwazi uvamizi wa wageni nchini mwao. Na wanafikiria hata kunyang'anya uraia waliokwisha toa kwa baadhi ya watu. Kama nyie ni wafuatiliaji hii ni movement kwa ulaya nzima. France wanakataza watu kuvaa hijab maanake ki kuwa kaka wewe ni muislam kweli kweli huwezi kufikiri kuishi nchi kama hiyo.

    Kwa kweli mimi nikimaliza PhD yangu siwezi ishi nchi kama hizi kwani huwezi jua ni raia wangapi wanachukia foreigners. Ukawii kupigwa kisu ukiwa matembezini. Hawa watu wanajua kuchukia aisee si kama sisi waafrika tulio na upendo.

    Jamaa wanamuita kichaa ili kuua soo. Ukweli unabaki pale pale kuna mpaka blogs za kupinga multiculturalism. Kwa hiyo alichokifanya ni kitendo ambacho kuna wengi wenye mtizamo kama wake wanakiona ni cha kishujaa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2011

    we unayesema tutashirikiana na wachina tu kwani umesikia wachina hawana ubaguzi kwa weusi?hao wabaya kama kawaida.tena waovyo kweli wakiwa kwao.ni sisi tu tunawafurahiaga wageni tukiwa kwetu ila hawa wakiwa kwetu wanajifanyaga wazuri ngoja uende huko uchina au ulaya aula.ubaguzi kila pahala ndugu yangu.maisha ni mapambano popote ulipo ni kujitahidi kuishi kwa nidhamu as much as you can.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2011

    SASA NA HUYU NI AL QAIDA? AU MTANDAO GANI JAMANI NISAIDIENI, INGEKUWA MAJINA YAALEEEEE! NA SEHEMU ZILEEEEEE SASA HIVI USA,UK WANGEKUWA WANAPASHA, KILA MTU ANA HAKI YA KUDAI HAKI YAKE HATA AITWE JINA GANI

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2011

    Ubaguzi ni hulka ya kila mtu. Mimi mwenyewe nakerwa sana na serikali yetu kugawa ardhi na uraia kwa wageni bila hata kuwashirikisha wananchi. Mfano ni juzi serikali ilipoamua kuwapa warundi wapatao 165,000 uraia bila hata kupata baraka za wananchi. Na hivi karibuni nasikia raisi amesaini mkataba wa kuwapa wanyarwanda ardhi ya Tanzania bila hata kuwashirikisha wananchi. Nafikiri haya ni maaamuzi ambayo yatakuja kujutiwa miaka mingi ijayo hasa ardhi ya tanzania itakapoisha na wazawa wakagundua kuna wageni waliochukua ardhi yao. Ni hatari!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2011

    walioanza tabia hizo ni waislamu. Kwenye nchi zao hawataki wakristo wanadiriki hata kuwaua. Angalia hata Zanzibar jinsi walivyo na ubaguzi wa dini kwa mkiristo anayetaka kuhama toka bara kwenda zanzibar. Wakati wa mwezi mtukufu wanalazimisha watu wote wafuate sheria zao hata kama sio kila mtu ni muislamu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2011

    hahahahahaaa kuna kazi humu,tutarudi maisha yatakapo kuwa sawa lakini si kwa ubaguzi,sisi wenyewe kwa wenyewe tunabaguana, wala hiyo sio sababu..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2011

    tena wachina wanaongoza kubagua watu nchini kwao, mtu mweusi wakisimamisha taksi china haisimami. sisi tunawapokea na kuwaendekeza. watu wanabaguliwa na kuteseka nchi za watu. wahindi wanachoma hadi nyumba za watu weusi huko India..ila sisi hadi uongozi tunawapa. wakati kuna baadhi ya nch mgeni haruhusiwi kufanya kazi hata ya kuokota takataka kama si raia.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2011

    Sasa dada yetu akishaolewa na mzungu watoto si moja kwa moja wanakuwa wazungu. Yaani wanachukua asili ya baba yao.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2011

    Swala loote linaongelewa hapa ni ubaguzi. Tanzania kwenyewe ubaguzi kibao wenyewe kwa wenyewe hata ukienda kuomba mkopo unatokea madongo kuinama mtu atakunyanyulia pua ukitoke Masaki watakushughulikia kwa adabu. Huyu bwana ni sera yake na kundi lake. Wenzake wanakimbilia huko nje kuoa na kuolewa ambao ni wengi kuliko hao wenye matatizo ya akili. Kulitilia maanani analolisema nasi tutakuwa tumepungukiwa na akili. Tukio hili halina tofauti na huyu bwana anyeuwa wake za watu gesti sasahivi Tanzania, tofauti ni idadi tu ya mauaji. Degelavita.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2011

    hayo mambo mbona hata bongo mnayo si kila siku mnawatishia nyau magabacholi??wapi yule dada wa kihindi alieshinda miss Tz alirushiwa madongo kibao sema huko nyie ni maskini mnakosa mabomu na bunduki hata nyie siku moja mngewakimbiza wahindi.Mmemsahau Idd Amin alivyofanya???Ubaguzi uko kila sehemu kaka.tembea uone usikae hapo bongo tuu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 27, 2011

    naunga na mdau aliesema mbona tanzania unauwa watu wake naniwatanzania wenzake bora ubaguliwe nchi ambayo unajua kabisa sio nchi yako kuliko ubaguliwe ktk nchi unayojua ni yako harudi mtu hapa mimi niko marekani huu ni mwaka wa kumi pamoja na watu kusema kunaubaguzi lakini sio kiivyo sana huku kuna ubinadamu sana na haki zako zinalindwa hakuna wizi wa kijinga na hakuna ajali za kutisha za kila leo kama tz unaishi kwa uhuru na amani kila kitu unachota unakipata maisha ni popote na kifo kipo kila mahali wewe mwenyekuleta hii mada unasema sehemu isiyo wazazi wako hiyo sio tija wengi wanaishi tz nawazazi wao naniwazawa bado maisha ni magumu na kunatofauti kubwa kati ya aliyekuwa nacho na asiye kuwa nacho tz imeoza kwakila kitu siwezi hatakuelezea maana nitajaza kitabu mimi ningekuwa ninauwezo ningewaamishia ukoo wangu woote america

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 27, 2011

    nimetembelea kwa wahindi noma ila kidogo kwa wazungu ndio washenzi na waarabu sio sana ila wachina wako pooa sana

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 27, 2011

    aah wapi hiyo ni bahati mbaya tuu... haturudi ng'ooo kwenye mgao wenu wa umeme wa masaa ishirini na maji ya kubeep, hakuna cha mkataa kwao ni mtumwa bali mvumilia mateso nyumbani kwao ndio mtumwa! mbona huku majuu weusi hatukatiwi umeme na maji? wote tuna pata umeme na maji ya moto 24/7 iwe summer winter ni burdani tuu ... haturudiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 27, 2011

    mungu ni mwema acheni malumbano,tusiogope tuzidi kusali na kumwomba mungu,ila kila mtu afuate sheria ya popote alipo,wengine tunajisahau,hata kufanya kazi,tunasingizia migongo ili tule sosho,pia wanawake tupunguze kuzaa ovyo kwa kuwa watoto wanalipwa,wazawa wenyewe hawana timu ya mpira,

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 27, 2011

    mbna hata tusiende mbali tz kwenyewe tunabaguana wenyewe kwa wenyewe tena unabaguliwa kwenye nchi yako mwenyewe uliyozaliwa kisa unatokea madongo kuinama huoni inavyouma
    niafadhali niishi nje maisha bora nibaguliwe na nifanye kazi nichume mihela kuliko nibaguliwe kwenye nchi yangu mwenyewe yakuzaliwa na kuishi poor life
    kama kifo kiko kokote kinaweza kukukuta huwezi kwepa kifo
    Tanzania ni umaskinitu unatusumbua tungekua tushawalipua hawa wageni marangapi tunawawasema wahindi na wakenya na wageni wengine wanaoishi hapo unadhani wao wanafurahia au unadhani huo sio ubaguz?
    be realistic bwana acheni kuchukulia mambo juujuu
    Uarabuni wenyewe wanabagua Wakristo nakuchoma makanisa
    so hii isue nikubwa iacheni jinsi ilivyo.
    but for me nikipata chance yakuishi nje nitakimbia kama risasi nakuhamishia familia yangu yote huko maisha kkote bwana

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 27, 2011

    popote ni ubaguzi mtupuuuuuuuuuuuuuuuu.Hata kwenye familia kama kuna waliofanikiwa basi wasiofanikiwa katika maisha hubaguliwa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 27, 2011

    Nakuunga mkono mdau hapo juu uliyesema mbona Watz wenyewe wako katika nchi yao na masikini wanabaguliwa,ni kweli bora ukabaguliwe na kunyanyaswa katika nchi ya watu kuliko nchini kwenu yaani inauma sn saaaana mnno!!!! mpaka mtu unakosa kwa kwenda!Kidogo hapa UK nimeishi nimeona kweli kwa mtu ambae ni raiya anafanyiwa Uttu kuanzia makazi,matibabu,usalama na mambo mengi anayohitaji mwanadamu,,ni kweli kodi ni nyingi sana lakini unaona kweli hizo kodi zinafanya nini!sio watu mnatoa kodi au kupewa misaada hujui zinakoishia watu ni kujinufaisha wenyewe,,magari ya kifahari majumba na kuuziana wenyewe kwa wenyewe na hizo tu nyumba za NHC wanainchi wamekaa miaka na miaka masikini mpaka zinawabomokea wanalipa kodo tu ,,,kuuziwa uongozi umegoma!!!1Sisi Watz tutakaa masikini na kushuhudia viongozi wanafaidi Dunia mpaka mwisho wao tutalalamiaka lakini hatutafanya lolote,kwa kuwa sisi WaTZ si asili yetu kuvamia viongozi au kuamsha vita!!!lakini nahisi iko siku ya siku litakuwa jambo!maana ukiona kobe kaina ujuwe anatunga sheria!!!na umuogope mtu unaempiga kofi la kulia akakugeuzia na la kushoto,,,baadae ukiona kakugeukia na kustare at you oohhh kimbia haraka anakumaliza,,,thats what I can say!!Naliona hilo mbeleni,kwani hata Misri hakuna mtu ambae alitegemea wataamka kivita!maana ni nchi ilokuwa na Amani kama TZ,,,,akiamka mmoja wa kulalamika ujue waliodhurumiwa ni wengi na wanaofaidi ni wachache kwa hiyo huyo mmoja ataungwa mkona na karibia T-A-N-Z-A-N-I-A,,,,NZIIIMA maana wenye njaa tuko wengi sana na hata mtuletee majeshi ya US hatutasurrender,,hata kama wachovu wameezeeka auwamekufa basi vijukuu vyao vitasimliwa manyanyaso ya wazee wao,,hivi Tanzania haijengi ila inabomoa!Kumbukeni mla ndizi huwa anasahau ilamtupa maganda hasahau hata sehemu alipoyatupa!!!!Kweli kuishi nchi za watu ni kazi ila kama kwenu ni kama TZ unajiuliza mara mia mia kurudi!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 27, 2011

    Ubaguzi upo kila mahali ila bongo cases ni chache sana mfano yule mzungu wa Bongo Star Search(BSS) sio kama nchi zingine kama ulaya,India hata kwa watani zetu wa jadi(KENYA)wao ndo usiombe. Tena Wakenya ndo hovyo kabisa wakija hapa wanaonekana wakarimu kumbe hamana ki2.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 27, 2011

    Ubaguzi kila mahali opo kama uko uswazi ndo duh, kama mdau mmoja apo juu, mashindano ya umiss alishinda ndugu yetu hadi nakulia wengine walilia eti ohhh si mtanzania....aibu tupu. Uku maisha ni matamu hakuna kupigana mizinga ya buku kama uswazzy. Ubaguzi upo kila mahali...ni afadhali kuishi Ulaya au popote ubaguliwe kuliko kuishi Tz. Tz matatizo mengi magonjwa maisha mabovu yaani kila kitu taabu.Toka nihamie Ulaya sijawahi ona maji yamekatika au umeme umekatika. au ata kuona gari mtaani limepata pancha, au jamaa kafungua boneti, au gari watu wanasukuma limekataa kuwaka. Sijawahi ata kuumwa kichwa.

    Bongo harudi mtu,

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 27, 2011

    popote tu unaweza fanyiwa baya kwanza hiyo hali imepungua sana kuliko zamani, huko nyie mafisadi wanawatafuna watu wanakua maskini wanashindwa kulipia hata matibabu wanakufa kwa umasikini ni mamilioni, watu wanakufaa mamiliioni kwasababu ya kuwa mafisadi, halafu mnabaki kusingizia ukame,si afadhali mtu alopiga risasi na kuua watu 76 norway, angalia somalia, watu akili hakuna ni kutafunanana wenyewe kwa wenyewe njaa sasa hivi mamilioni wanakufa, tanzania tunauana kwa style ingine, bora hata uonewe sehemu sio kwenu kuna logic kuliko kuonnewa na kukosa usalama kwenu.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 27, 2011

    UBAGUZI TANZANIA NAKO JE?

    Tanzania watu wanaua maalbino na kuwakatakata viungo vyao na kuviuza...huo ni unyama uliokithiri. Ni ubaguzi...unambagua mtu kwa kisa ngozi yake.

    Tanzania kuna ubaguzi wa dini. Leo hii familia moja ya kikristu kwelikweli mtoto wao aseme anaoa mtoto wa kiislamu, let's say mtoto wa Shehe, hapo familia inaweza kumtenga mtoto wao. Huo ni ubaguzi wa kidini.

    Tanzania tuna ubaguzi wa kikabila. Kupata kazi lazima utoke kabila fulani...ukitaka kuoa lazima uangalie kabila kwanza nk. Hilo ni sawa na kwa wazungu nao, wazungu ni kama kabila fulani, nalo linataka mtu wa kabila la wazungu aoe mzungu mwenzao.

    Mfano dhahiri wa ubaguzi Tanzania: Miss Tanzania Richa Adhia, aliposhinda kuwa Miss, watu walilia mfano Hapiness Magese kuwa wamechagua Muhindi...vyombo vyote vya habari vikasema Mhindi ashinda kuwa Miss Tanzania. Wanahabari wakazidi kusema kuwa India inawakilishwa na mamis wawili, mmoja ni yule kutoka India, na mwingine ni Richa Adhia. Huo ulikua ubaguzi mkubwa sana...ila watu tunaona poa tu.

    Tanzania kuna ubaguzi wa aliyenacho na asiyenacho. Masikini anabaguliwa na kunyanyaswa na mfumo wa kitajiri wa watu wachahe nk.

    Popote pale kuna ubaguzi ndugu

    Mdau

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 28, 2011

    Haya mambo yameanza kule Norway lakini katika mtazao wangu hapa sweden kuna warabu wengi sana kuliko sisi wafrika naweza kusema wanachukuwa nafasi ya pili baada ya waswidis nahofia ipo siku waswedi wenye siasa kali watatikisa nchi hii

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 28, 2011

    SERIKALI YETU YENYEWE NI WAUAJI WACHILIANA VICHAA AU MTU MMOJA MMOJA, MWAKA 2001 WATANZAIA ZAIDI YA 2000 WALIKIMBILIA NCHI JIRANI NA IDADI KUBWA KUUWAWA KULE ZANZIBAR, MWEMBECHAI NA JUZI KULE ARUSHA, TUACHE MATOKEO MADOGO MADOGO AMBAYO NDIO MENGI, WATANZANIA NINI WAMEKIFANYA WAMEUWA WATANZANIA WENZAO WAFANYA BIASHARA YA MADINI, MIMI NIPO USA NIKO MORE CONFORTABLE KULIKO NILIPOKUWA HUKO KUNAKOITWA KWETU TANZANIA, AJIRA TUNAANGALIA KWA MAKABILA, HAPA USA STATE YOYOTE ILE NAWEZA KUISHI NA KUFANYA KAZI, ILI MRADI NIPO KISHERIA, NYUMBANI SIHITAJI KIBALI CHA KAZI, LAKINI KAZI MPAKA NIHONGE AU KABILA FULA LINALOFANANA NA MWAJIRI.
    BADO NITAENDELEA KUWEPO UGENINI, MANUFAA NILIYO YAPATA HAPA YAMEWASAIDIA WENGI NYUMBANI TZ, UKIFIKA WAKATI TUTARUDI.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 28, 2011

    Ubaguzi wa Mtanzania ni umaskini. Ukipata basi hubaguliwi tena. dawa watu kusoma na kupata elimu ya kutosha. Kiwango cha lazima cha elimu kiongezwe kutoka msingi kwenda sekondari

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 28, 2011

    Ni bora nibaguliwe na kuuwawa kwa shaba norway kuliko kubaguliwa na kuuwawa na dnugu zangu bongo kwa njaa.

    kifo chaja hata ukikwepa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...