Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe ( watano waliokaa kulia) akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chai Tanzania, Mh. Anne Makinda ( wanne kulia waliokaa) ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wadau wengine wa zao hilo, ( wapili kushoto waliokaa ) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Mh. Issa Machibya, sambamba na Wakurugenzi wa Bodi, Wakuu wa Wilaya na Wenyeviti wa Vyama vya wakulima pamoja na Wenye viwanda vya zao la chai nchini,
Mmoja wa viongozi wa wakulima wa dogo wa zao la chai nchini , Rehema Malekela ( aliyesimama) akichangia hoja kuhusu hatua za mikakati ya kuboresha zao hilo ili wakulima waweze kupata bei nzuri kwenye masoko ya ndani na nje
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akionesha hisia ya kushangazwa kuwepo kwa mogogoro kati ya wakulima wadogo wa chai dhidi ya wakulima wakubwa na wenye viwanda ambayo haileti tija ya kuongeza uzalishaji wa chai nchini , wakati alipofungua mkutano wa wadau wa zao hilo mwaka 2011, uliofanyika Julai 8, mwaka huu mjini hapa.
Baadhi ya wadau wa chai wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe ( hayupo pichani) alipo soma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano kwa wadau wa zao hilo mwaka huu mjini hapa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chai Tanzania, Anne Makinda, ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,akifafanua jambo katika hotuba yake ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe ( hayupo pichani) kufungua mkutano wa wadau wa chai mwaka 2011.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...