Meneja Uhusiano kutoka Wakala wa Umeme Vijijini Bi. Jaina Msuya akimpokea Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa heshima wakati akiingia kwenye banda la Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ili kujionea shughuli zinazofanywa na wakala huo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bw. Bruno Mteta juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza kwa makini mtaalamu Bw. Godwin Msigwa kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Ensol Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA) alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Fundi Sanifu Bi Jemina Sadatale kutoka Mradi wa Umeme Jua wa KKKT Mpwapwa unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mjiolojia Mkuu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Bw. Maruvuko Msechu akimwonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda ramani ya kijiolojia mara alipotembelea banda hilo kwenye Maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata ufafanuzi juu ya shughuli zinazofanywa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kutoka kwa Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Aloyce Tesha mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkufunzi wa Chuo cha Madini Dodoma Bw. Dickson Kaijage juu ya kozi zinazotolewa na chuo hicho mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo juu ya matumizi ya gesi kwenye magari kutoka kwa mtaalamu Bw. Charles Sangweni kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) mara alipotembelea banda hilo. Anayesikiliza ni Bw. Aloyce Tesha ambaye ni msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini.Picha na Greyson Mwase.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2011

    Nimemmind kweli huyo dada anaonekana ana heshima balaa hadi anabend dah michu fanya mambo tuwasiliane.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2011

    Tunawapongeza Wizara kwa kutoa elimu kwa waheshimiwa kuhusu mambo ambayo Serikali inatekeleza. Nashauri kuwepo na elimu hata kwa njia ya TV na redio ili wananchi pia wapate fursa ya kujua kuwa Serikali inawajali na inashughulikia kero zao. Hongereni sana. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2011

    EWURA WAKO WAPI? BWANA KAGUO NA TIMU YAKO MBONA HAMUONEKANI, UMMA TUNAWAHITAJI KUFAHAMU MUSTAKABALI WA MAFUTA NA NISHATI.....!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...