Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mh Nassor Ahmed Mazrui |
NA NAFISA MADAI - MAELEZO ZANZIBAR
Wizara ya biashara viwanda na masoko imesema imeandaa mipango maalum ya kuwasilisha serikalini kwa mazingatio ya sheria za ushindani na kumlinda mtumiaji,sheria ya mizani na vipimo na sheria ya baishara pamoja na kuandaa utekelezaji wake.
Hayo yameelezwa na waziri wa biashara viwanda na masoko,Mh Nassor Ahmed Mazrui alipokuwa akisoma bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012 huko katika kikao cha baraza la uwakilishi mbweni nje kidogo wa mji wa zanzibar.
Aliseama mabali na mpango huo wizara pia imekusudia kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa utoaji leseni za biashara nchini ili kurahisisha uanzishaji na ufanyaji wa biashara pamoja na kuanzisha utekelezaji wa sheria ya viwango ya zanzibar.
Aidha alisema katika kukamilisha utafiti wa kuiwezesha serikali inafanya maamuzi makini kuhusu mkakati wake wa kuimarisha uchumi na uendelezaji viwanda vyenye lengo la kuchangamsha biashara zanzibar.
Sambamba na hayo mh. mazrui amesema wizara yake pia imepanga kuliimarisha shirika la biashara la taifa (ZSTC) kwa kulifanyia mageuzi makubwa ya kisheria na muundo ili liwese kusimamia vizuri uendelezaji wa zao la karafuu ili liweze kumudu ushindani katika soko la dunia.
Akizungumzia viwanda waziri huyo alisema wizara yake pia imeandaa mazingira mazuri ya uwekejai katika sekta ya viwanda kwa kufanya mapitio ya sera ya viwanda na kuchunguza vikwazo inavyokwamisha maendeleo ya viwanda zanzibar.
Aidha laisema wizara imeandaa mfumo mpya ya vivutio kwa ajili ya kuendeleza sekta viwanda zanzibar.
Akizungumzia shirika la biashara ya magri amesema wizara inakamilisha taratibu za kulifunga shirika hilo katika msimu unaonzia juai 2011 kwani shirika hilo limekua likikabiliwa na changamoto nyingi ikiwa na uwezo mdogo wa uzalishaji wa ndani wa bidhaa.
Akitaja changamoto nyengine ambazo zinalikumba shirika hilo ni pamoja na udaifu wa kutumia fursa za masoko ya kikanda kuongeza usafirishaji pamoja na thamani ya uzalishaji huo pamoja na ari ndogo ya wajasirialimali.
Kuhusu kushamiri kwa tatizo la magendo ya karafuu mh. mazrui amesema wizara ilifanya tafiti na kubaini kuwa nchi moja ya jirani hivi sasa imejitokeza kuwa msafirishaji mkubwa wa karafuu ingawa nchi hiyo haizalishi karafuu.
Kutoka na hali hiyo serikali imeanza kuchukua hatua za kisoko za kupunguza na hatimae kuondosha kabisa pengo la bei ya mkulima na ile ya soko la dunia ili kuondoa kishawishi cha kufanya biashara hiyo ya magendo
Aidha alisema serikali inakamilisha taratibu za kuunda mfuko wa maendeleo ya karafuu kwa madhumuni ya kusimamia vyema zao hilo.
Wiara ya biashara iwanda na masoko imelimba baraza la uwakilishi kuidhinisha matumizi ya Wizara hiyo jumla ya shilingi bilion mbili,milioni mia sita na sitini na mbili kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kati ya fedha hizo shilingi bilioni moja, milioni mia nne na sitini na mbili kwa ajili ya kazi za kawaida na shiling milioni mia tatu kwa ajili ya kazi za maendeleo.
Jana usiku baraza la uwakilioshi zanzibar lilipitisha bajeti ya wizara ya ustawi wa jamii, na maeneleo ya vijana wanawake na watoto kwa kipindi cha fedha 2011/2012, baada ya kazi kubwa iliyofanywa na mawaziri mbalimbali ya kutoa ufafanuzi juu ya suala la mkataba wa nyumba ya kulelea watoto mazizini, na suala la uzalilishaji wa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...