Captain Abbas Mwinyi, mwanae Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akisoma hotuba kwa niaba ya baba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa Akaunti mbili zinazofuata kanuni za KIISLAMU  za CORPORATE ISLAMIC CURRENT ACCOUNT pamoja na BUSINESS ISLAMIC CURRENT ACCOUNT za Benki ya Taifa ya Biashara katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam Jumanne Agosti 9, 2011  baada ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wageni waalikwa.

 Mgeni rasmi Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua mlango kuashiria uzinduzi wa akaunti hizo
 Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru akitoa maelezo ya akaunti hizo huku mgeni rasmi Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBC Dkt.Mussa Assad  (shoto)  na Mkurugenzi Mkuu wa Islamic Banking wa benki ya NBC Bw. William Kallaghe  (kuume) wakisikiliza
 Dua baada ya uzinduzi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBC Dkt.Mussa Assad  (shoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru na Mkurugenzi Mkuu wa Islamic Banking wa benki ya NBC Bw. William Kallaghe baada ya kumuaga mgeni rasmi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. So funny! Yaani kuna hadi bank accounts za kiislamu?!!!! I was thinking kunaweza kukawa na account za "waislamu au za muislamu" lakini sio account za "kiislamu" .Kwa kweli mmeamua kujitenga na dunia kwa kila namna. Too much isolation of yourself from other people could be one of the causes of ever increasing religious conflicts in the world, something which is not good for human development. Anyway, imani ni kitu kigumu ambacho kila mtu ana namna yake ya kukitafsiri. Sorry ndug zangu waislamu kama nimewakwaza kwa kauli zangu hizi, nimejisikia tu nieleze hisia zangu.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hajui kitu kaa kimya. Waislamu wana kila kitu chao ikiwemo sheria zote za kila kitu mpaka jinsi ya kuhifadhi fedha. Ningewashauri waislamu wa Tanzania kuanzisha benki yao na kujiwekea pesa huko kuliko kunufaidha benki za Magarantia.

    ReplyDelete
  3. We anon wa Wed Aug 10, 07:25:00 AM 2011, Wacha upumbavu na chuki zako. Kanuni za benki za Kiislamu (1) zinakataza fedha zetu Waislamu zisiwekezwe kwenye (a) pombe (b) casinos na madanguro (c) biashara ya nguruwe. (2) Uislamu unakataza riba (interest/usury) lakini inakubali faida (post-tax dividends). Waislamu hatuji-isolate hata kidogo, tunafuata kanuni zetu tu. Increasing religious conflicts are caused by the imperialists' desire to totally colonize and dominate the world. We as Muslims will continue opposing that hegemonistic aspiration whether you hate us or not. (3) Islamic banking windows ziko katika benki elfu nyingi duniani, including USA, UK, France na nchi 162 nyingine kama vile zilizo "kosher banking" kwa Wayahudi ambao pia hawawekezi katika bportfolios zinazokiuka kanuni za dini ya Bani Israil (misingi ya Taurati na Talmud). Mwisho, usituite eti "ndug (sic) zangu Waislamu" kwa sababu huo ni unafiki unaotoka kwa mtu mnafiki anayetuchukia na ambaye maoni yake hayana kichwa wala miguu ila kututusi. Lakini kaa ukijua, upende usipende Wasilamu tutaendelea ku-practise dini yetu na chuki zako hazitatuzuia. Kama hufurahi kajitose baharini. Muslim banker.

    ReplyDelete
  4. Wewe mchangiaji wa 7:25:00 AM, Pilipili usiyoila inakuwashia nini? Hamna mtu atakayekulazimisha kufungua akaunti yenye kuheshimu maadili ya Kiislamu. Kwa hivyo fyata mkia wako na usituharibie saumu zetu. IloveIslam.

    ReplyDelete
  5. Ndugu zangu kama bado kuna ambao mnataka ushahidi kuwa kuna baadhi ya manasara (si wote) wanatupiga vita Waislamu na dini yetu, basi 'maoni' ya huyo 'mchangiaji' wa kwanza ni ushahidi wa kutosha. Tafadhalini zicchapisheni 'maoni' hayo na muyasambaze katika tovuti zetu ili wenzetu wote watambue harakati iliyo mbele yake. Sisi Waislamu Watanzania hatuna vita na watu wa imani nyingine lakini kuna vikundi ambavyo vimeamua kutupiga vita kwa hivyo ni wajibu wetu kupambana nao katika kila hali.

    ReplyDelete
  6. Safi sana. Mimi nina account NBC lakini siku zote nilikuwa nakwazwa na ukweli kuwa huenda pesa zangu zikawa zinategewa uchumi katika viwanda vya pombe. Asante NBC kwa kwenda na wakati ijapokuwa benki za wenzetu wa Kenya zimetupita kwa miaka 20 katika issue hii.

    ReplyDelete
  7. Ankal, mimi nimeishi USA kwa miaka mingi sana. Kuna Wakristo wa madhehebu ya Quaker ambao hawatumii huduma za benki yoyote yenye kuinvest katika viwanda vya silaha kama vile Wabuddhist na Wahindu hawawekezi katika benki yoyote yenye kuinvest katika biashara ya nyama. Sasa nashangaa kuna huyo mwenzetu hapo juu amecharuka na kuanza kutushambulia Waislamu. Wanaotaka kuvaa hijabu wazivae wanaotaka kuvaa misalaba pia wazivae na sioni tatizo kwa hayo. Live and let live.

    ReplyDelete
  8. Wala hujamkwaza mtu, maana hujui usemalo.

    ReplyDelete
  9. Salaam.Mtoa mada wa kwanza huko peke yako katika kuushangaa mtindo wa maisha yetu waislamu. We are indeed so funny and so isolated. Na kama unavyodhani,yawezekana sana kuwa religious conflict nyingi zinasababishwa na ukweli kuwa tuko so isolated. Wewe,kama wengi tu hamjatuelewa. Hamjaelewa tunaamini katika nini. Na labda kwa sababu hiyo, baadhi ya watu wanaprefer kututenga na kutuignore badala ya kutusikiliza ili watuelewe.
    Mimi kwa miaka 12 sasa naishi hapa ukerewe. Hapa kwa mujibu wa takwimu, idadi yetu ni ndogo sana kulinganisha na population ya nchi,tuko milioni 2 tu. Lakini pamoja na uchache wetu,hapa kuna mabenki yenye akaunti za kiislamu, kuna shule zetu, mabucha yetu, university zetu, wasichana na dada zetu wana uhuru wa kuvaa vazi la kiislamu madarasani na makazini, tuna channels zetu za TV, tuna wabunge wetu na hata tunayo mahakama inayofuata sharia law. Jumuia nyingi tu za kiislamu hapa ukerewe zinapata ruzuku kutoka serikalini. Kwa maana gani nasema yote hayo? Maana yangu ni kwanza kumwonesha mtoa maoni wa kwanza kuwa kama yeye hatuelewi,hilo ni tatizo lake na la wenzake binafsi. Tunaeleweka na kukubalika, and we are not isolated. Pili ni kumfahamisha yeye na wenye fikra potofu na finyu kama zake kuwa ni mara chache mno kusikia kuna religious conflicts hapa ukerewe kwa sababu waislamu tumeeleweka na kukubalika. We are not ignorant, we are genuine. We never compromise our faith.
    NAMWALIKA MTOA MADA AUSOME ILI AUELEWE UISLAMU, HUENDA AKATUFAHAMU VYEMA. AKIPENDA, ANITUMIE E MAIL ILI TUMTUMIE VITABU BURE, ATUSOME,ATUELEWE NA KUELIMIKA. lessauk@lycos.com
    Mimi ni mndengereko, nilipokwenda Moshi na kuoa mchaga, mambo mengi nilikuta yametofautiana na mazoea na mila za pwani, badala ya kuconflict, nikaamua kuzisoma!!!!!
    Mndengereko,Ukerewe.

    ReplyDelete
  10. Ndugu yangu Mndengereko. Tatizo la huyo mtu unayemwalika ajifunze ni kuwa mimi nahisi kuwa yeye ni mmoja wa watu ambao wamekuzwa kutuchukia sisi Waislamu na dini yetu, kwa hivyo yeye ni katika wale watu waliozama katika chuki inayowafanya wasione ukweli, wasisikie ukweli na, mbaya zaidi, wasitafute ukweli. Nyoyo na roho zao za chuki zimesababisha bongo zao zitandwe na ukungu wa giza ambao hauwezi kuondoka mpaka watakapoamua kutumia akili zao badala ya jazba zao zilizopanda farasi wa chuki ambaye mwisho wa siku watawabwaga katika miiba na matapishi ya huzuni. Nawatakia Ramadhani ya utulivu wa moyo na uongofu.

    ReplyDelete
  11. Waislamu wenzangu, huyo jamaa aliyeamua kututukana ni wakala wa iblis/lucifer/shetani. shetani aliyelaaniwa anajua kuwa katika mwezi huu tumeamrishwa kutotii matamanio yetu. Pia tueamriwa kufanya ibada zaidi, kuwasamehe maadui zetu, kuzidisha kuwasaidia wanyonge, kutosema uongo, kuacha kusengenya na kuacha hasira kiasi cha kwamba Mtume wetu (SAW) alituusia kuwa hata mtu akikutukana na akitaka kupigana na wewe mwambie "Nimefunga sitaki ugomvi", ijapokuwa ukishambuliwa una haki kabisa kujihami kikamilifu by any means necessary. Sasa shetani anawatuma mawakala wake kama huyo mtoa maoni wa kwanza atukasirishe ili tupunguze fadhila za saumu zetu. Ninachoshauri ni kuwa tumwombe Allah amvue chuki zake na ampe mapenzi na uvumilivu; lakini kama shetani amemwingia kabisa rohoni mwake basi tumwombe Muumba wetu (Subhana Wataala) awaangamize yeye na huyo shetani wake. Amin.

    ReplyDelete
  12. We anon wa )7:25:00 AM, There is nothing funny. We Muslims have our own principles regarding investments, borrowing and lending. We are not allowed to impose extortionist interests on loans. For example, if you are banking with an Islamic bank in the UK and you take a 150,000 pound mortgage loan you will end up paying 200,000 pounds(regardless of repayment period), the extra 50,000 quids being contribution to the bank's operating costs and taxes as well as the builder's profit. On the other hand, if you take out a 150,000 pounds loan from a non-Islamic bank, you will end up paying a whooping 600,000 pounds. Now that's usury. Even the Bible forbids usury, kwani hiyo ndiyo silaha kubwa ya matajiri kuwakandamiza wanyonge. Hali kadhalika, kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa juu, Islamic banks haziwekezi katika biashara ya pombe na majumba ya kamari (casinos). Sasa wewe kabla ya kujitia kutuita kwa kejeli eti "ndugu zangu Waislamu" ungelitakiwa uombe kuelimishwa. Kuuliza si ujinga. Lakini chuki ndiye mama wa vita zote. Oh by the way, kabla sijamaliza: What is funny (and sad at the same time)ni yale makanisa ya Ulaya na USA yanayofungisha ndoa za wasenge na wasagaji wakati wakijua kuwa matendo ya Sodom na Gomorah ni haramu katika Uislamu, Ukristo, Uyahudi, dini za jadi na hata katika Ubaniani/Uhindu. Mdau wa sekta ya benki.

    ReplyDelete
  13. Ama kweli anayetaka kukutukana hachagui matusi. Hilo jinga la kwanza katika kutoa comments ameanika chupi yake yenye m*** hadharani kwa kutoa hoja za uongo zisizokuwa na mantiki kwa kuwa anatuchukia tu. Hao ndio watu au makundi ya kuyajua na kupambana nao katika ngazi zote watakazoturushia mashambulizi. Waislamu tuwe macho. Kuna watu wanatamani tusingelikuweko hapa TZ, lakini kwa uwezo wa Muumba wetu tutaendelea kuwepo na hawatuzuia kufuata dini yetu. Venceremos!!!!

    ReplyDelete
  14. Wewe anon wa 7.25 a.m. Let me tell you what is the root cause of religious conflicts: Basically it is haters like you!!! As soon as you saw the word "Islamic" you had a massive adrenaline rush which put you in a cantakerous and fight-or-flight state. If you learn how to be more tolerant of other faiths then there will be no religious conflicts, and that applies to people of all faiths. Muslim by Nature. DSM and New York.

    ReplyDelete
  15. Nawashukuruni woote mliochangia maoni niliyotoa. Na nilimalizia kwa kuomba radhi kama nitawakwaza ila nashangaa jazba tayari zimeshaanza. Sikuwa na nia ya kuwadhihaki na wala siwaonei wivu hata kidogo kwa kuwa na banking system yenu ila ni katika harakati za kuelimishana. Nimetoa maoni yangu mimi binafsi na si kwa niaba ya wasio waislamu na hata siku moja uislamu sijauchukia kwani katika imani yangu nilifundishwa kwamba sote tu viumbe wa Mungu mmoja na hivyo siwezi kumchukia muislamu wakati sijakuumba mimi. Nina mengi sana yanayohitaji majibu ili niilewe dini yenu vizuri lakini kutokana na response naona sinsiendlee kutafuta ukweli. Ila contradictions bado zipo, kwa mfano watoa maoni wamesema kuwa na Islamic bank ni kuepuka kuchanganya pesa na za pombe lakini mwingine anasema UK wanawapa ruzuku waislamu. Hii ruzuku hujui kama imetokana na kodi nyingi zikiwemo zile zinazotoka kwenye pombe na kwenye brothels. Ninavyofanhamu mimi mwanadamu ni yule yule ndio maana hata waliotuletea hizo dini wenyewe wanashindwa kutekeleza jinsi zinavyotaka. Naomba nirudie tena kuwaomba radhi saba mara sabini.

    ReplyDelete
  16. Jamani watanzania, haya mambo ya dini yatatuletea al shabab hapa hapa bongo halafu tutamtafuta mchawi. Huyu jamaa kakosea nu kweli ila hizo hasira zinazidi mipaka na sio maadili hasa katika mwezi huu. Tusiwe na jazba tunapodili na mambo kama haya ya kiimani. Si tunafundishwa kusamehe na na kuwaombea dua watu kama hawa? Kwa nini tusifanye hivyo badala ya kukoleza mkaa halafu tuanze kuuana kama somalia na pakistan. Tusiache mtu mmoja aharibu mfungo na kutufanya tukose amani. Kila mtu ana wajibu wa kukemea uchochezi wa aina hii lakini si lazima presha ipande wakati una fanya hivyo.

    ReplyDelete
  17. Mnajidai na hiyo dini yenu kama vile kuwa muislam ni kuiona pepo. ati mnachukiwa, hivi kwa nini mtu akitoa maoni hata kama anataka kuhoji kitu nyie tayari mnadai mnachukiwa na dini yenu? kwani ina lipi la ajabu?

    ReplyDelete
  18. Kwa sheria ya Kiislamu, mtu anayeomba msamaha anasamehewa. Kwa hivyo pamoja na kukasirika mimi nimemsamehe huyo ndugu yetu. Uislamu unasema "Ukimsamehe mwenzako basi na wewe Mwenyezi Mungu atakusamehe". Kwa hivyo mimi nimemsamehe kwa roho ya ukunjufu huyo ndugu yetu aliyeeleza kuwa nia yake haikuwa mbaya.

    ReplyDelete
  19. We anonymous wa 03:22:00 PM. Wewe ni moja ya mnaotuchukia. Tazama tu "tone" ya barua yako. Lakini nakuhakishia hamtuwezi ng'ooo!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. Mdau umeomba samahani!Kwa niaba ya Waislam wenzangu na mimi mwenyewe Tumekusamehe!Ila hapo chini umesea 'Waliotuletea Dini walishindwa kutekeleza jinsi zinavyotaka'!Ee umenistua kwani wewe ni Dini gani kama ni mkristo unayeamia kuwa Nabii Issah(A.S)Mtu wa Mwenyezi Mungu,kwa sisi Waislam tunavyoamini na nyie Wakristo ndio Yesu Kristo,kwani matendo yake hakuyatekeleza?Au husomagi Bible?Sisi Tunaamini kuwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W)Ambaye Matendo yake yote ndio mifano yetu sisi Waislam kufuata na Qur'an Maneno ya Mwenyezi Mungu ndo Mwongozo wetu!Sasa nani tena aliyeleta dini hakutekeleza?????
    Kuhusu mdau 10.03 unasema Waislam tunajidai eti tunachukiwa eti Dini yetu ina lipi la Ajabu!Ee kama hulioni la Ajabu wewe jiulishe,,,kwa nini America,Ulaya Israel,,wote kutwa ni kuusema Uislam mara ooh materrorist,mara ooh kuban Hijab kwani kuna watu wangapi wanalipuana wenyewe kwa wenyewe na sio Waislam na mavazi mangapi hata kutembea uchi katika nchi nyingi huku Ulaya wanaruhusu kwani Hijab inawadhuru nini,,,Kwa faida yako ngoja nikwambie hakuna atakae Ingia Pepo ya Mwenyezi Mungu kirahisi hivi hivi bila kupata misukosuko ya Duniani,Hata Mwenyezi Mungu ametwambia katika Qur'an kuwa atakae mcha yeye kikweli kweli mitihani itamuandama,na sio kila unae msikia kwa jina la kiislama ni mcha Mungu No No No Uislam ni Matendo Mema na Kusimamisha Swala!Wengine wanamajina ya Kiislaam lakini hawafuati maadiili yake,na hao wadau wote hapo Juu inaonyesha kweli Ma'ansha'Allah ni wacha Mungu wanaipenda Dini yao na wanajaribu kuitetea kwa Maandishi kwani Mtume wetu katufundisha hivi ukiona kuna pahala mtu yeyote anafanya uonevu au ukatili au kama hizo chuki za dhahiri basi kama kuna aina ya kupigana tia mkono wako,kama huwezi basi tumia mdomo wako na kama huwezi basi sikitika tu rohoni!!!Hao Waislam wameisha umwa na nyoka sasa wakiona michusi wanastuka!
    Kuhusu Bank A/C za Kiislam Tanzania ndo ilikuwa bado imebakia nyuma Nchi zingine ni kitambo kwa mfano hapa Uk Bank Lloyds TSB miaka mingi ina a/c ya Kiislam mimi nilivyofika hapa nilishangaa maana huko kwetu sikuviacha ila najuwa Kenya Bank ya hapo Bongo ni ya Kiislam!Nimefungua hiyo A/C ya Kiislam na najuwa sili riba Alhamdulillahi!kuhusu hiyo uliyosema Waislam wanapata Ruzuku hicho ni kitu cha kuumpa masikini mwenye shida hakuna jinsi,ni kama mtu anakuja kukulilia ana njaa na wewe unampa pesa kwa kutaka ale na familia yake kisha yeye anaenda kulewea pombe,,,tofauti na pesa yako wewe uipeleke kuekeza katika pombe kamali au biashara nyingie haramu au mikopo ya riba!Mwislam ukiwa na shida unaweza kujikopesha bila riba!,,,Hiyo Bank ya hapa hata Wakristo wengi wanafungua A/C ya kiislaam kwa kukwepa mambo mengi!Ni kweli Mwenyezi Mungu akisema kitu ni haramu ni haramu huwa kina madhara yake,,,na Mkubwa mmoja wa kanisa hapa UK alisema watu tufuate Sheria za kiislam naona yeye alisoma kweli akajuwa Sheria za kiislam ni MadhubutiiUtake Usitake kama mtu Uislam unauchukia hata ukapewa Ushahidi wa Namna gani hutakubali!Mwenyezi Mungu anasema hivi!WATAKUWA NA MACHO YA KUONA USHAHIDI NA MASIKIO YA KUSIKIA USHAHIDI LAKINI HAWATAKUBALI!Insha'Allah Mwenyezi Mungu atuongoze sisi Waislam tusiteteleke na Dini yetu!Na Tufuate Sheria zake kama alivyotufundisha Mtume wetu kwa Mwongozo wa Qur'an na Hadithi!
    Wabillahi Tawfiq!
    Ramadhan Maqbour!!!!
    Muislam Ahlam UK!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Mtoa maoni wa kwanza ione siku yako ya leo ni siku ya kuzaliwa upya, sababu maoni yako yamekuwa sababu ya kukuelimisha. Lakini pia yametoa mwanya kukuonesha waislamu ni watu wa aina gani. Yalipotokea matukio ya milipuko ya 9/11 uvumi ukaenezwa kuwa uislamu ni ugaidi. Waislamu wengi tukaingia matatani, tukapatwa na misukosuko mingi sana. Lakini kwa kuwa mara nyingi shari huzaa heri, takwimu za sasa zinathibitisha kwamba uislamu ndio mfumo unaoingiza wafuasi wengi zaidi kuliko mfumo (dini) nyingine yoyote,huku USA ikiingiza wafuasi wengi zaidi katika uislamu kuliko popote pale hapa ulaya na kule america. Ukija hapa ukerewe hushangai tena kukutana na wazungu wengi tu waislamu. Hivo ndivo uislamu ulivo; the more u attack it, the more it proves to u.
    Hivo nawe naamini utajifunza mengi kuhusu uislamu kuanzia leo.
    Lakini pia utaelewa kuwa wafuasi wa mfumo huu ni shupavu sana, hawapendi kukebehiwa. Hata unapotaka kudadisi jambo linalowahusu inabidi upange vizuri sana maneno ya kutumia,na zaidi ni kwa sababu wengi tu wameshajaribu kutubeza nakutudhihaki hata kututukana na kututukania Mungu na Mtume wetu. Enough is enough!!!
    Ndio maana sasa tunadefend kwa kushambulia,kabla amani haijachafuliwa. Mara ingine mtoa maoni wa kwanza sidhani kama utatumia same approach kujadili issue zetu.
    Hakuna controversy yoyote kuhusu waislamu ukerewe kupokea ruzuku za serikali ambayo kwa maneno yako pato lake linatokana na ulevi. Vyanzo vya ruzuku viko anuai. Serikali hapa ina mwongozo kamili wa aina zipi za ruzuku zinakubalika na vyama vya kiislamu. I wish mtoa mada wa kwanza ungenitumia e mail nikakupa somo kamili ili uondokane na misunderstanding ulizonazo.
    Mndengereko,Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...