Bunge limepitisha hoja ya kuundwa Kamati Teule ya kuchunguza swala la Bw. David Jairo, ikiwa ni pamoja na mchakato wa pesa alizodaiwa kuchangisha ili bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ipite, mantiki ya Katibu Mkuu Kiongozi kulitolea maamuzi swala lililotoka Bungeni.
Kamati hiyo itaundwa keshokutwa Ijumaa ambapo wajumbe wake na mwenyekiti watatajwa, na inatarajiwa kutoa ripoti yake kwenye kikao kijacho cha Bunge mwezi Novemba.
Hii imekuja baada ya Mbunge wa Simanjiro (CCM) Mh. Christopher ole Sendeka kutoa hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza swala hilo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh Kabwe Zitto, kutoa hoja ya kutaka swala hilo la Katibu Mkuu Kiongozi Mh Philemon Luhanjo kutoa maamuzi ya kumrudisha kazini Bw. Jairo baada ya ripoti ya awali ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubainisha kwamba uchunguzi wake haujabaini kuwa ana hatia.
WABUNGE MNAFANYA UCHUNGUZI GANI TENA? SI MAAMUZI YAMESHATOLEWA NA LUHANJO? KWANI NINYI WABUNGE HAMJACHANGISHA FEDHA KUPITISHA BAJETI ZENU?
ReplyDeleteNINYI NDIO MLIOTUNGA SHERIA ZILIZOMUWEZESHA JAIRO KUCHANGISHA FEDHA. NCHI HII NZURI SANA. HAKUNA KUMUONEA KIONGOZI.
Wabunge wanaopewa hayo mabahasha ya Jairo si mnao huko Mjengoni? Mpelekeeni basi ushahidi Utouh, Luhanjo au Hosea ili waweze kumfungulia mashtaka! Kazi ni kuunda vi-kamati tu vya kutafuna miposho wakati watu wanahangaika!
ReplyDeleteSame bloody old politics! Another waste of Taxpayers money! What is so seriously wrong with you people? So Luhanjo's and the rest have formed a committee and concluded Jiro has done nothing wrong whatsoever and he was re-instated. What was Hosea's department doing about this because I believe his dept. has the funds and means of dealing with the issue, but instead, we hear from Luhanjo (whether Hosea's dept was involved I do not know). Now, another committee would be formed to investigate the same, which is ok because people have more faith in the opposition now. But why wasn't the joint commettee formed in the first place to save money and time(i.e which would have involved the oppostion).
ReplyDelete