 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiongea na wafanyakazi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) leo alipotembelea ofisi hizo kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa mfuko huo kuhamasisha jamii kufanya kazi kwa bidii na kuibua masuala mbalimbali na fursa zilizopo nchini kwa maendeleo taifa. |
 |
Mpiga picha na mwalimu wa fani hiyo kutoka Flame Tree Media Trust Bw. Mwanzo Millinga akimwonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi baadhi ya picha za matukio mbalimbali alizopiga katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa habari kwa umma kutokana na ufadhili wa Mfuko wa vyombo vya Habari (TMF) leo jijini Dar es salaam. |
 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi( wa kwanza kulia) akiwa na Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura(kushoto) pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo na waandishi wa habari wakiangalia moja ya kipindi cha Nchi Yetu kilichoandaliwa kwa ufadhili wa TMF kumulika Haki za Binadamu na masuala mbalimbali ya kijamii. |
 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya picha zilizopigwa mkoani Lindi leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania. |
 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiongea na wafanyakazi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) leo alipotembelea ofisi hizo kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine kazi mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa mfuko huo kuhamasisha jamii kufanya kazi kwa bidii na kuibua masuala mbalimbali na fursa zilizopo nchini kwa maendeleo taifa. |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Ruzuku kwa vyombo vya habari nchini (TMF), Saeed Kubenea, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanahalisi, wakati waziri huyo alipofanya ziara kwenye ofisi hizo Dar es Salaam leo kujionea shughuli mbalimbali zinaofanywa na mfuko huo. Wa pili kushoto ni Meneja Mipango wa mfuko huo, Bw. Ernest Sungura na nyuma yake ni Mwandishi mwandfamizi wa wa gazeti la Serikali la Daily News, Bw. Deogratias Mushi (kushoto)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...