Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya Ikulu mjini Zanzibar jana,na kujadili namna ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha mmoja ujao,hasa kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi.
 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya hiyo kuhusu azma ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake,kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,  kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya hiyo kuhusu azma ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake,kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,  kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012 (10/08/2011).
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya hiyo kuhusu azma ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake,kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,  kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012, Picha na Ramadhan Othman Ikulu.


Na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, ameanza kukutana na Uongozi wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuangalia Mipango ya utekelezajai wa Malengo Makuu ya Wizara na Uhusiano wake na Dira 2020 na Mpango wa kukuza na kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA).

Dk Shein alianza kuzungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya mapema leo ambapo Wizara hiyo ilielezea Mipango yake na Mikakati iliojiwekea katika Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2011/2012.

Katika kikao hicho , ambapo pia Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alihudhuria, Wizara ya Afya ilielezea mipango yake ya kuimarisha sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na kueleza ufumbuzi wa Chumba Cha Wagonjwa Mahtuti katika hospitali ya Mnazi Mmoja ambacho kimekuwa hakifanyi kazi kwa muda hivi sasa.

Wizara hiyo ilieleza pamoja na mambo mengine inakusudia kuendelea kuwaleta Madaktari Bingwa kutoka Uturuki kwa ajili ya kutoa huduma za Maradhi ya Moyo,Mkojo, Saratani, Figo na Watoto.

Wizara hiyo ya Afya ilielezea mafanikio makubwa ya ziara ya Dk Shein alioifanya huko Uturuki,ambapo tayari Madaktari kutoka nchini humo wamekuja Zanzibar na wataendelea kuja kwa awamu kwa ajili ya kutoa huduma za Afya sambamba na kutoa nafasi za Masomo nchini Uturuki na kuwapeleka Wagonjwa wa Zanzibar kwenda kutibiwa nchini humo.

Katika kikao hicho Wizara ya Afya pia ina mipango wa kuweka Mtambo wa Oxygen kwenye Chumba cha Upasuaji, Chumba cha Wagonjwa Mahtuti,Chumba cha Wazazi na sehemu nyengine.

Kwa upande wa huduma za Madawa Wizara ya Afya ilimuelezea Dk Shein mikakati yake ya kuendelea kuhakikisha Wananchi wanapata huduma za Dawa katika vituo vyote vya Afya Unguja na Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...