Ankal akiwa na Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile wakijipatia futari katika mkahawa unaohudumia futari ya nguvu katika mwezi huu mtukufu ya City Garden katika bustani ya Nyerere Square katikati ya mji wa Dodoma kila siku jioni.
Wadau kibau hufurika hapo City Garden kila siku jioni kwani bei ni chee na futari ni ya nguvu
Wadau wakimiminika City Gardem mjini Dodoma leo
Ankal na Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile wakijipatia futari leo jioni katika City Garden mjini Dodoma
michuzi mbona hiyo sio jioni au mzee ndio hivyo tena
ReplyDeleteKWA MTAZAMO WANGU WA PICHA ILIVYO HIO SIO FUTARI KWANI MAGHARIBI HAIJAINGIA HAPO NI KWEUPE, HAPO NI WASAFIRI WANAKULA TU ILA SIO FUTARI
ReplyDeletekaka mbona hapo mchana kweupe? halafu hilo koti dry cleaner umemlipa sh ngapi? teh teh
ReplyDeleteMichuzi mbona habari za Libya humu hamna? Kukaa kimya nako ni propaganda pia.
ReplyDeleteAnkal hiyo Futari mbana na jua kali hivyo.Duh!Hiyo sio lunch kweli??
ReplyDeleteMkulima,Kijijini Gezaulole.
we michuzi muislam jina hufungi wala huswali ...
ReplyDeleteKWeli mithupu hapo unaonekana kazee kweli kweli nimejua siri ya kale katisheti ketu kanafichaga umri aiseee!
ReplyDeleteUmejitakia mwenyewe Michuzi. Kwani siku hizi haijalishi jina kuna akina Thomas Ramadhani lakini wanafunga na sala tano haziwapiti. Akiwa (mke) nyumbani hafungi na ndie anayempikia bora ale tu au atakuwa anashinda na njaa. Unajua kuna mwanamme mmoja yuko huku marekani amezaa na kimada mkristo kwa hiyo amemhamisha nyumbani anakaa naye na yeye anafunga na sala tano hazimpiti na ijumaa kanzu nzito anavaa kwenda msikitini. HII IMEKAAJE MAUSTADH. HEBU WASOMESHENI HAWA WENZENU WANAANGAMIA NA KUUSINGIZIA UISLAMU KILA AINA YA UONGO.
ReplyDeleteUnajua Lailatu Al-qadr huwa usiku unaonekana mchana. Usijali kaka Michu, kila mtu na kaburi lake. Mwenye enzi hachakachui malipo, kila mtu atabeba msalaba wake.
ReplyDelete