Ankali eee... habari yako Mkuu,
Naandika haya nikiwa sio tu na hasira bali pia kwa kukata tamaa maana hapa nilipo natumia taa ya dharura inayotumia betri (angalia picha) niliyonunua kwa Machinga pale Namanga jijini Dar juzi tu. Tena kama Mungu aliniambia nifanye hivyo maana ingekuwa soo! Maana hata mishumaa nimeuliza sehemu kibao imeisha. JAMANI!
Ni kwamba hivi tunavyoongea hapa kwangu Tabata Kimanga leo nalala giza, maana betri zikiisha na chaji kwenye hii kompyuta yangu ikikata ndio basi tena....
Pesa ninayo na leo maeneo karibu mengi ya jiji la Dar yana umeme. Lakini tatizo hakuna huduma ya LUKU!!! Nimezunguka mji wote naambulia foleni tu, nikiuliza naambiwa network ya LUKU leo imekata kutwa nzima!!! Hebu fikiria,  mwezi ungeandama na leo Jumanne ingekuwa sikukuu ya Iddi ingekuwaje???
Yaani haingii akilini kabisa kwamba network siku zoooooote isikatike ije kukatika leo. Hii kama si hujuma kwa hawa jamaa wa maudhi TANESKO ni nini? Hivi wataachwa kuendedelea kutuhujumu kila kukicha namna hii hadi lini??? TUMECHOKA NAO!!!
Rai yangu kwa wahusika ni kwamba sasa wakati umefika TANESKO wawajibishwe. Huu ni uzembe wa hali ya juu na hujuma isiyoweza kuvumiliwa katu. Hawana hata adabu wala aibu!!! Kiiiiila siku visababu tu. Ina maana hawa watu hawanaga Plan B ama C katika huduma zao??? Mara maji kwenye mabwawa hakuna, mara mitambo inafanyiwa ukarabati, haya na leo LUKU hakuna. Watatuongopea nini??? 
Serikali iache kuchekacheka nazo taasisi kama hizi. Akiwajibishwa mtu ama watu kwa kupewa adhabu kali kama wanavyofanya wenzetu wasiotaka masikhara katika utoaji wa  huduma za jamii (tena sio bure kwa kulipia) hali hii itakoma. 
Mie naomba ifikapo saa sita leo mchana tusikie mtu ama watu wamewajibishwa. Kuchekeana sasa BAAAASSSSIIII!!!!


Mdau Tabata

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mimi nafikiri sio suala la kulaumu taasisi tu bali ni kulaumu Wizara husika na Sertikali kwa ujumla kuhusiana na tatizo la Nishati ya Umeme lisilokuwa na kikomo kwa muda mrefu sasa. Kwani hainiingii akilini kuwa tatizo hili linakosa ufumbuzi kwqa takribani miaka 20 sasa. Ukizungumza ukweli unaonekana kuwa unaleta mambo ya siasa wakati suala la huduma ya nishati ya umeme ni moja kati ya mahitaji muhimu ya jamii bila kujali itikadi ya siasa.
    MIMI SIO MWANA SIASA LAKINI NASEMA SERIKALI KAMA MMESHINDWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI BORA MUACHIE WENGINE WENYE UWEZO WATEKELEZE. MAMBO YA KUBEMBELEZANA SASA TUMECHOKA JAMANIII!!!!

    Mdau MAREKANI.

    ReplyDelete
  2. pole sana kwa matatizo ndugu yetu ni imani yangu watanzania wa hali ya kati na yachini mwisho kiuchumi tumeshaa zoea sema ipo siku wanaotusababishia haya mateso yote watahukumiwa na Mungu tu na si mwingine;vile vile tuache dhana ya kuilaumu TANESCO tatizo sio Tanesco bali ni WAZEE WA SIRIKALI. Mungu ibariki TANZANIA

    ReplyDelete
  3. Mpendwa rafiki yangu, kajiunge na M-Pesa na Tigo Pesa upesi sana utaepukana na kununua umeme kwa foleni

    ReplyDelete
  4. sio siri jamani hii ni kuhujumu uchumi wa nchi. Hata mie yamenikuta ndugu yangu. Network ipo down tokea jpili usiku watu tunalala giza na hela tunayo mkononi. Ni balaa watanzania wenzangu. Mmasai wa loliondo

    ReplyDelete
  5. poleni wadanganyika, hapo hakibadiliki kitu bila ushindani wa kibiashara.Waruhusu kampuni binafsi zizalishe na kusambaza umeme fullstop.

    ReplyDelete
  6. Costantino MasingaAugust 30, 2011

    Hongera Mdau wa Tabata kwa kuibua hili, Nami nilikutana na tatizo kama hili jana, nadhani gharama nilizotumia katika kutafuta umeme, kwa maana ya mafuta ya kuendesha gari kutoka kituo kimoja cha Luku kwenda kingine si mchezo. Mimi nina wasiwasi kwamba wakati mwingine Tanesco hawaongezi bei ya umeme kwa sababu ya kuongezeka kwa gharama za uzalishaji bali kufidia uzembe kama huu. Wadau watakuwa mashahidi, ni kiasi gani jamaa hawakukusanya jana na mara zote transforma zinapoharibika na Tanesco kuchukua muda mrefu kuzirekebisha. Wadau kama mtandao umeshatengamaa Tanesco tujulishane umeme unapatikana ili tukimbilie hapo mara moja.

    ReplyDelete
  7. Ni vichekesho suala la luku kulahumu wizara kwanini usilahumu TANESCO watu wake wa IT wameshindwa kufanya kazi vizuri. Hili ndilo tatizo la technology walipaswa IT wa TANESCO walifanyie kazi mapema. Kuhusu M-Pesa au Tigo-pesa kuna bahadhi ya mita hazitambui. Poleni kwa matatizo lakini Rashidi alisema 'Yana mwisho' KULI

    ReplyDelete
  8. Acheni kelele wenzenu wa vijijini mbona hawalalamiki kwa kukosa umeme. Serikali imeshindwa kupata umeme nafuu ndio maana hili tatizo haliondoki. Wewe fikiria wangapi wana uwezo wa kutumia generator kila siku? Ili umudu umeme wa genereta inabidi uwe na magenereta mawili na kila siku mafuta ya 50,000/=. Wangapi wenu wataweza hizo gharama. Network ya luku kuwa hapatikani hilo ndio unaweza lalamika maana Tanesco walitakiwa wawe na network mbadala inapotokea tatizo, kwa hiyo hilo ni tatizo la uongozi wa Tanesco ambao hawakuweza kuweka mikakati mbadala. Hiyo Tanesco ilikuwa ikiongozwa na wazungu sasa sijui walikuwa wanafanya nini muda wote. Hivi sasa ndani ya taasisi nyingi za serikali kuna watu ambao ni wafanyakazi wa hizo taasisi wanaharibu kwa makusudi vifaa vya kazi kwa manufaa yao. Kwa utafiti niliofanya sehemu yangu ya kazi kuna ufisadi wa makusudi unaofanya na wafanyakazi tena hawa wafanyakazi wana umoja halafu mbio wanasingizia serikali. Gamba sio kuvua kwa wanasiasa bali hata wasiokuwa wanasiasa ambao wanaendesha taasisi za umma wanatakiwa wajivue au kuvuliwa. Ndio hii nchi itakwenda.

    ReplyDelete
  9. pole hii ndio Tz

    ReplyDelete
  10. Chezea Tanesco weye?? hilo ni litwiga likubwa lisilo na ufikiri! Una pesa, uko tayari kulipia gharama za umeme zote yet unakaa giza mwaka mzima?? chezea ooh. sio mbaya kujaza nafasi za kazi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo nishati. yana mwisho, yameshakinaika tayari bado kutapika. pole mdau,mengi tuu, hela unazo na ATM zote Mujini hazifanyi kazi lol............

    ReplyDelete
  11. hehehe next tym uwe unanunua umeme mwingi usisubiri karibia na sikukuu ndo utujazie blog yetu,

    ReplyDelete
  12. kaka, Mpesa,Tigopesa, NMB bank na Nbc Bank ndio suluhu, hizi option zote zimewekwa kumrahisihia mteja kupata huduma bila kuhangaika, sehemu za mauzo ya Luku pia ni nyingi sana, haya yote kukurahisishia wewe kaka. Kwa hili tusiwalaumu TANESCO kwani breakdown ya siku moja ni kwawaida, ingawa pia yaweza kutokana na wewe mwenyewe kutokuwa na mpangilio mzuri wa shughuli zako(kusubiri mpaka unit ya mwisho kabisa ndipo kushtuka kuwa umeme haupo sasa nikimbilie kununua umeme. Wazo la jumla: kuna mambo mengine serlikali ibebe mzigo na lawama lakini kwa mambo mengine si ya serikali. jamani watanzania mmojammoja kama 90% kila anapoulizwa shida zake atasema ooh serikali haituoni( tunalaumu sana serikali hata kwa mambo binafsi. MKOMBOZI WA MAISHA YETU NI SISI WENYEWE selikali ina chango wake wandugu , ila si kila kitu(kama hili). tutalemaa. kaka weka mpango mkakati wa kupata solar ndogo kwa matumizi nyeti usipate breakdown na kukasirika sana. ukisubisri serlikali yako, utakosa maendeleo sijui utawaambia wanao kuwa selikali hii jamani ndio maana hatuna maendeleo, selikali hii jamani ndio maana mnakosa hili na lile. kwa kifupi tujue namna ya kujua wajibu wetu na wa selikali pia.Asanteee

    ReplyDelete
  13. na hicho kijikitabu unachosoma cha muungano wa tanzania unakisomea gizani ? ndo ujue hamna faida ya muungano

    ReplyDelete
  14. nyie woote mnayemwambia anunue kwa mpesa ,tigo pesa au nmb kwani hamuoni kama yeye anatumia luku ya kizamani ya kuingiza kadi , yeye lazima akapange foleni huyo kazi anayo kweli kweli , nenda tanesco wakubadilishie hiyo luku

    ReplyDelete
  15. Mnasema Mpesa, tigopesa hakuna chochote mimi nimununua kwa MPesa tangu saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa hizi saa kumi na nusu hakuna majibu.
    Nimekwenda kuunga foleni ndio kwanza napata umeme sasa hivi. poleni wadau, hii ndio nchi yetu na tunaamani tele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...