Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais Sheikh Sharif Ahmed wa Jamhuri ya Somalia wakipita katikati ya gwaride la mapokezi ya mgeni huyo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar leo.
Na Mwandishi Maalumu
Tanzania imetangaza leo, Jumanne, Agosti 9, 2011, kuwa itatoa msaada wa tani 300 za mahindi, ili kuwasaidia kupunguza makali ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili kiasi cha wananchi milioni 3.5 wa Jamhuri ya Somalia.Tanzania pia imeahidi kutoa misaada mingine kwa nchi hiyo kwa kadri uwezo wa nchi unavyoruhusu katika kuisaidia Somalia kukabiliana na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kuisalama ambayo yamekuwa yanaikabili nchi hiyo mfululizo katika miaka 20 iliyopita.
Mchango wa Tanzania umetangazwa wakati wa mazungumzo rasmi kati ya Serikali ya Tanzania na ile ya Jamhuri ya Somalia, na wakati wa futari ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemwandalia mgeni wake Rais wa Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed ambayo yuko katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini.
“Tunasikitika sana kuona matatizo makubwa ya ukosefu mkubwa wa chakula yanayoikabili nchi yako. Kama unavyojua Tanzania ni nchi masikini na uwezo wetu siyo mkubwa. Lakini tuna methali hapa isemayo kutoa ni moyo siyo utajiri. Kwa hiyo kwa moyo huo wa mtu masikini, tumeamua kutoa mchango wetu mdogo wa tani 300 za mahindi ambazo ni sawa na magunia 3,000 ili kusaidia ndugu zetu wa Somalia kukabiliana na hali ya njaa kubwa,” Rais Kikwete amemwambia Rais Sheikh Ahmed.
Ameongeza Rais Kikwete: “ Tunajua kuwa mahitaji yenu ni makubwa zaidi kuliko hiki kidogo tulichotoa. Lakini sasa ndiyo kwanza tumeingia katika msimu wa mavuno. Tutaangalia huko mbele kama tunaweza kuwachangia zaidi ndugu wetu wa Somalia.”
“Tunazungumza pia na marafiki zetu ili tuwashawishi kuona kama nao wanaweza kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Somalia ya kuhakikisha inapata chakula cha kutosha ili kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi.”
Wakati wa futari ambayo Rais Kikwete amemwandalia Rais huyo wa Somalia katika Mwezi Mtukufu huu wa Ramadhani, Rais Kikwete ametoa mwito kwa makampuni yanayotengeza maji nchini kusaidia kuchangia upatikana wa maji kwa wananchi hao wa Somalia. Somalia inahitaji mamilioni ya lita za maji ili kukabiliana na ukosefu mkubwa wa chakula na maji.
“Tutazungumza na makampuni yanayotengeneza maji hapa nchini kama nayo yanaweza kuchangia kupambana na janga hili kubwa linalowakabili wananchi wa Somalia,” Rais Kikwete amemwambia Rais wa Somalia katika shughuli ya futari.
Shughuli hiyo imehudhuriwa na watu wengi wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Tanzania, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi nchini, mawaziri, makatibu wakuu na maofisa waandamizi wa Serikali na mawaziri wakuu wa zamani, Mzee Salim Ahmed Salim na Mzee Joseph Warioba.
Katika mazungumzo hayo rasmi, Tanzania na Somalia, zimezungumza masuala mengi ambako nchi hizo zinaweza kushirikiana kuisaidia Somalia baada ya ujumbe wa nchi hiyo kuelezea maeneo ambako Tanzania inaweza kuisaidia Somalia kama katika mapambano ya pamoja dhidi ya ugaidi katika Bahari ya Hindi na kusaidia kufundisha wataalam wa fani mbali mbali.
Rais Kikwete pia amempongeza Rais wa Somalia na ujumbe wake wa mafanikio ya kijeshi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha El Shabaab ambacho kimefukuzwa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Mogadishu ambayo kimekuwa kunayashikilia kwa muda mrefu.
Rais pia amempongeza Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed kwa mafanikio yake mengine ya kuleta utulivu zaidi ndani ya Serikali yake na kuongeza muda wa utumishi wa Serikali na Bunge kama moja ya njia ya kuleta maelewano ndani ya Serikali, na kati ya Serikali na Bunge la nchi hiyo.
Rais Ahmed ambayo amewasili nchini leo asubuhi, ataondoka nchini kesho baada ya kuwa amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kilimanjanro Hyatt Regency mjini Dard Es Salaam ambako amefikia.
Je, kuna chakula cha kutosha watanzania?
ReplyDeleteWewe mchoyo hapo juu unayeuliza tuna chakula cha kutosha acha roho mbaya na choyo, kwani hayo magunia 3000 ndio yatawafanya Watz wafe njaa? Wewe utakuwa mgala tu!
ReplyDeleteUnauliza chakula cha kutosha kwa watanzania hivi upo duniani kweli wewe au hauna hata TV yakuangalia habari za duniani na matokeo.Hivi unaijua hali iliyokuwepo huko Somalia?unajua watoto wangapi wanakufa kilasiku kwa kukosa chakula na maji safi ya kunywa?Wacha utani wewe usijifanye kipofu.Hiyo ni roho ya uchoyo.Tunatakiwa tuwachangie hawa binaadamu hawana kosa jamani wanatia imani sana.
ReplyDeleteanony wa kwanza kusaidia watu wanaokufa kwa njaa sio lazima TZ tuwe na chakula cha kutupa jalalani. Swali lako linaonyesha kuwa hukusoma habari yote hapo juu, au umesoma lakini sio kwa makini. Soma tena. Mh. rais ametamka wazi kuwa hata TZ ni nchi maskini.
ReplyDeleteKumbuka urithi wetu: BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRICA NI MOJA. Tuliposaidia nchi za kusini kupata uhuru hatukuwa na chakula pia. Unakumbuka?
Swala ni kwamba hapa penyewe watu wanakufa kwa njaa, nyie mko tanzania ipi?
ReplyDeleteTukianza kutoa msaada ..Tunaweza kutokomeza umaskini..
ReplyDeleteSaidia ili ujisaidie..
Inamaana tukilima vizuri,tukiwa na viwanda vizuri vya kuhifazi matunda ,tunaweza kuwekeza chakula chetu nje ya nchi kwa kutumia Watanzania waliopo huko tukawa na maduka ya kitanzania.
Kwa kufanya hivyo basi Taifa litakuwa na kipato kizuri tu.
Huwa nawashangaa sana baadhi ya watanzania yani sisi watanzania tukitoa hayo magunia 3000 tutapungukiwa na nini jamani?kumsaidia mtu ni jambo la hiyari na ni jema kwa wanaadamu na wewe wa kwanza kabisa lazima utakuwa mbeba mabox ulaya au muosha vyombo maana ndo kazi zenu huko njoo nyumbani uone mlo mara tatu kama kawaida.....ipende nchi yako wacha kuwa mtumwa wa wazungu.....
ReplyDeleteUNA MAANA UKO TAYARI KUWATOSA WATANZANIA WAFE KWA NJAA KWA AJILI YA KUWASAIDIA NDUGU ZETU WA SOMALIA? USIZUNGUKE SANA JIBU SWALI.
ReplyDeletehivi hawa waliotoa ujumbe wa ku-support hii idea ya kugawa chakula Somalia ni raia wa nchi hii hii (ambao hawakutapika upupu huu wakati wale wananchi wa Arusha walipotimuliwa na ardhi kupewa mgeni na wao kubaki na njaa!) au ni raia wa kigeni?
ReplyDeletemaana wanachoongea kinaweza kuwa na mashiko kama ni wageni (mf. al-shaabab militia) ila kama ni raia wa nchi yangu, ama kwa hakika matatizo yanayoikumba nchi kwa sasa yanatustahili (watanzania wengi ni mahayawani!)
naahidi kutomlalamikia tena rais
kumbe tatizo ni sisi wala si yeye wala baraza la mawaziri.