Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh Steven Wassira akipongezwa baada ya kuwezesha bajeti ya Wizara ya Maji kupita mchana huu. Mh Wassira alisoma hotuba na kuitetea kwa niaba ya Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya ambaye yuko India kwa matibabu na habari za uhakika zinasema anaendelea vyema
Baadhi ya waheshimiwa wakitoka bungeni kwa mapumziko ya mchana
Mbunge wa Mbeya Mh Joseph Mbilinyi (CHADEMA) akiwa na Mbunge wa Mtera Mh Livingsgtone Job Lusinde (CCM) wakihudhuria kwa pamoja semina ya Majukumu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Women katika ukumbi wa Pius Msekwa leo
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mh Jenista Muhagama (shoto) akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakisimiamia semina hiyo ya UN-Women leo
Waweweshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Women wakijiandaa kuendesha semina hiyo
Baadhi ya waheshimiwa katika semina hiyo
Ankal katika semina hiyo
Mama Anna Collins Falk, Country Programme Manager wa UN-Women akiwa tayari kutoa mada leo
Ankal naona umejipiga picha, kwa nini usitumie automatic function ili upozi vizuri?? Hapo unaonekana kama una mawazo ile mbaya, tena kuhusiana na madeni.
ReplyDelete