Kwa uwezo wa Allah na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati yetu (watanzania wa ugiriki) tumeweza kufanikisha mchango wa kumsafirisha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE- pichani juu) ili akazikwe nyumbani. Mwili wa Marehemu utawasili Dar J'mosi13/08 saa NANE NA NUSU USIKU kwa ndege ya shirika la Uturuki.
Marehemu alikoshwa,alikafiniwa na kuswaliwa katika msikiti wa ELSALAAM uliopo Neos Kosmos Athens.Idadi kubwa ya watanzania walihudhuria msikitini.Taarifa tulizo nazo khs maziko yatafanyika J'pili 14/8 saa saba mchana Tandika Mikoroshini kwa SANDARI ila kwa maelezo kirefu fanyeni mawasiliano na FATUMA dada yake (0718567537) au (0783694736)
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
KATIBU wa JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI WADAU WAKISUBIRI NJE YA MASJID EL SALAAM JIJINI ATHENS, UGIRIKI
WADAU WAKISUBIRI NJE YA MASJID EL SALAAM- ATHENS
WADAU WAKISUBIRI NJE YA MASJID EL SALAAM- ATHENS
mimi nilishakaa hapo umangani enzi hizo tunaishi wengi magheto ya kule Piraeus pale magheto mane.Enzi zile hatukuwa kama mlivyo sasa mnashikamana sana sisi tulikuwa tunangojea meli tuzunguke. Nawaombeeni moka awazidishieni moyo wa huruma maana kwa maisha ya leo watu kuchangishana siyo rahisi na huu ni ukweli usiokatalika.
ReplyDelete