
Baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta ya petroli na dizeli wameendelea na mchezo mchafu, wenye lengo la kuhujumu uchumi wa taifa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la UHURU umebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kuamua kukaidi kwa makusudi kukaidi amri ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nishati, William Ngeleja Bungeni juzi akiwaagiza wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta, kufungua vituo na kuuza mafuta hayo. Badala yake, baadhi yao wameyaficha na wengine wakipeleka shehena ya nishati hiyo kwenye migodi ya madini.
Makampuni ya BP, Engen, Oil Com na Camel Oil, yalitakiwa kujieleza kwa nini yasiadhibiwe kutokana na kutajwa kuwa chanzo cha mgomo. Hatimaye, Kampuni za Engen, Oil Com na Camel Oil, zilitekeleza agizo hilo kwa kuuza mafuta kwenye vituo vyake, licha ya baadhi kutotoa huduma, huku BP ikiwa haijatekeleza amri hiyo hadi siku inapoisha ya Alhamisi, Agosti 12, 2011. BP inadaiwa kuchukua mafuta kwenye maghala yake kwa ajili ya kusambaza vituoni lakini yamepelekwa kusikojulikana.
Katika maeneo mbalimbali nchini vituo vya BP havitoi huduma tangu Agosti 3, mwaka huu, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), kutangaza bei mpya. Hata hivyo, imebainika shehena kubwa ya mafuta iliyobebwa kwenye maghala ya BP, ikidaiwa inasambazwa vituoni imepekekwa kwenye migodi ya madini. Kutokana na hilo, EWURA imetangaza kuanza kuchunguza mwenendo wa BP.
Wananchi wengi wameshangazwa na hatua ya kujifanya 'kichwa ngumu' ya BP Tanzania, ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki hisa asilimia 50, na wameitaka serikali kuwawajibisha viongozi wote wa kampuni hiyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe somo kwa wajeuri wengine kama wao.
"Hii kiburi ya BP sio bure kuna jambo.." wamesikika wadau wa mafuta wakisema. "Hawa aidha kuna mtu ama watu wanaowapa jeuri kwa kuwalinda ama basi tu ni kutaka kuhujumu uchumi wa Taifa.
"We uliona wapi kampuni ama taasisi inayomilikiwa nusu na serikali ikawa na maluweluwe hivyo? Pengine hizo hisa 50 ni za mtu binafsi na sio kweli za serikali..."
"We uliona wapi kampuni ama taasisi inayomilikiwa nusu na serikali ikawa na maluweluwe hivyo? Pengine hizo hisa 50 ni za mtu binafsi na sio kweli za serikali..."
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha EWURA, Titus Kaguo, alikiri BP ilipakia shehena ya lita 400,000 kutoka kwenye maghala yake kwa lengo la kusambaza katika vituo vya Dar es Salaam na Pwani.
Hata hivyo, uchunguzi umebaini mpaka sasa vituo vya BP vimeshindwa kuuza mafuta na wateja wamekuwa wakijibiwa hayapo. Kaguo alisema Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA itakutana kupitia taarifa na kujadili hatua zilizofikiwa katika kutatua kero ya mafuta nchini. Pia itajadili na kutoa uamuzi dhidi ya BP iwapo itaendelea kukaidi amri halali ya Serikali.
source: http://www.wavuti.com/
Nadhani viongozi wetu wanaliangalia hili suala kwa upeo mdogo. Athari za nchi kuwa katika hali kama hii zinaweza kuwa long-term ukiachia mbali short-term effects kama hatari za moto kwa watu kubeba mafuta kwa vigudulia vingine vimetengenezwa kwa plastic ambazo ni very thin na havikusudiwa kwa kazi hiyo. Haya hilo tuliache. Kuna athari za "image"...sasa hebu niambie kazi zote wanazofanya viongozi za kuvutia wawekezaji, watalii na kujenga image ya nchi ni ya bure? Kwa hiyo ninyi viongozi hamuoni kuwa mnalichafulia sana jina taifa? Kwani mnashindwa nini kuwapiga teke hao BP mkawanyang'anya vituo vya mafuta na kuwapa wanaotaka kufanya biashara hiyo kwavile huu ni uhujumu wa uchumi na makampuni kama haya hatuyahitaji Tanzania. Hao BP walimwaga mafuta two years ago huko kwenye coast ya kusini mwa USA na usually hawako responsible....wana kiburi sana ilibidi watu walalamike sana kwa wao ku-increase speed ya kusafisha uchafu wao. Hebu angalieni hili swala kwa upana wakati tunaingia miaka 50 ya uhuru, mmeturudisha nyuma kabla ya uhuru..kubeba mafuta na vigudulia. Halafu nasikia ati kuna sherehe kubwa za uhuru sijui Washington DC...tuende tukafuate nini?? aibu tupu na nasika ati na Kikwete anakwenda huko...watu wamekosa cha kufanya?
ReplyDeleteBP wanachosha sana na tabia zao za kuharibu mazingira. Kuna LUKOIL warusi naona afadhali kufanya biashara nao. Kampuni za mafuta nyingi tu, lazima BP watakuwa wanakula na mafisadi...
ReplyDelete