MAENDELEO YA MSIBA,DC.
Macrina Samaka enzi ya uhai wake
Watanzania wenzangu,DMV,leo ni wiki na siku 3 tangu marehemu alipoaga Dunia Jumamosi July 30,2011
Pesa zilizopatikana kwenye Harambee na michango ni $3,500/= tunaomba Watanzania wote tusaidiane kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu Tanzania.
Gharama zilizobakia sasa ni $ 5,500/= bado tunaomba msaada wako,muonee huruma Macrina,anahitaji msaada wako ili akapumzike kwenye nyumba yake ya milele,najua tunaweza kama Watanzania wenye upendo na Mtanzania mwenzetu,mshikamano na moyo wa huruma,chohote ulichokua nacho kitasaidia.
Kumbuka kifo hakina mmoja leo Macrina,kesho ni mimi na wewe.
Kitabu cha michango kipo wazi muda wote,au kama ratiba yako hairuhusu unaweza kupita Wachovia Bank au kumpigia mtu yeyote kati ya hao hapo chini nasi hatutasita kufuata mchango wako tunatanguliza shukrani zetu kwa wale wote waliosaidia na wanaondelea kusaidia lengo nikujaribu kusaidia kupeleka mwili wa marehemu Tanzania
Address ya msiba ni
4303 FRANKFORT DR,
ROCKVILLE,MD,20853
TUNAOMBA WENYEVITI WA JUMUIA ZA WATANZANIA ZILIOPO NJE YA DMV,WASAIDIE KUTOA TAARIFA HII KWA WANAJUMUIA KWENYE STATE ZAO,MICHANGO INAWEZA KUPITIA Routing #055003201-A/C #1010323780193-WACHOVIA BANK-Arthur Gao/Memorial Funds a/c for Macrina Samaka.
kwa mawasiliano na maelekezo
Afisa Ubalozi,Abass Misana-202 378 8066
Rasheed Mkakile-240 938 3177
Arthur Gao-240 408 1422
Magrette Wahida-301 915 5821
Dj Luke Joe-301 661 6696
Malecela(New York)-914 473 1033
Boston(MA)
Juliana-413 330 3891
Abela- 781 913 2107
Suzie-617 306 1645
Houston,TX
Georges Assenga-713 894 9403
Wichita,KS
Erick Tagalile
316 993 0843
Bruce Bond-301 254 2806
MWENYEZI MUNGU AMETOA,MWENYEZI MUNGU AMETWA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE,
AMIN
sitaki kupinga juhudi lakini tungeweza kumhifadhi hapahapa. Watanazania wengine tumeshaona kwenye blogu wanazikwa ughaibuni kama UK, Greece, na majimbo kadhaa hapa.
ReplyDeleterecession hii jamani, tunatakiwa tupunguze matumizi ya fedha kwa kufuata njia mbadala zilizopo kwenye jamii.
Michuzi hii sio ile tuliyokutumia,hii ni ile ya 02 August na leo ni 09 August,wanajumuiya watatukaba tukiwaambia bado hela ni ile ile $3500, watu siku hizi hawana imani, hawakawii kukuletea polisi na kudai hela walizochanga.
ReplyDeleteAnyway,message muhimu ni kuwa pesa bado zina upungufu,tunaomba tushirikiane tuzimalizie,ni kiasi gani kimebaki,tafadhali wasiliana na hao wahusika waliotajwa.
Kiongozi underground
Poleni sana wafiwa,lakini kuna nini hapo DC na MD,mbona ni kawaida yetu kusaidiana ktk misiba lakini sasa hatuelewi wapi kuna tatizo mbona kule Texas na hata Ugiriki hii michango inachukua siku moja tu,kuna mtoa maoni alipendekeza kama marehemu ana life insurance mchukue mkopo halafu mrudishe ili marehemu asafirishwe haraka,mji mkubwa huo na wote ni watoto wa mjini fanyeni $30 kila mmoja DC yote na Maryland watu zaidi ya 300 mnalimaliza hili,labda pia mmeweka contact namba nyingi- watu wanaogopa, wekeni watu watatu tu na akaunti vitatosha.
ReplyDeleteMnatutisha jamani,mungu atusaidie tupendane ,tuwe na moyo wa kutoa ili tufanikiwe.
Ni mawazo tu, samahani kama itawagusa.
poleni sana, mdau wa tatu amesema kweli. dc in watu wengi sana, lakini kutwa kumuaibisha huyu marehemu kwenye blog na vikao vya kila siku. pia dada mtu hiyo nauli ya kutoka tz hadi huko ingepunguza kiasi kikubwa, haya jamani jitoeni kwa bidii nyinyi watu wa dc.
ReplyDeletepoleni sana wafiwa. ila mimi pia naona kama uwezo haupo wa kuusafilisha mwili wa marehemu kwanini asizikwe hukohuko tu jamani + - mdogo wake kaja huko anatosha kuiwakilisha family jamani maisha yanaenda yakibadilika. unafanya unachoweza usichoweza sio zambi wala kosa.
ReplyDeletejamani huyu dada mnamtesa bure, kama uwezo ni mdogo msilazimishe, azikwe tu huku huku DC. hata huko nyumbani hawawezi kutulaumu. atakaye laumu angetuma peas za kusafirisha. mnaufanya msiba unakuwa mrefu mno, hata huko bongo nadhani wameshachoka kusubiri. tuzikeni tu DC, naye safari yake ndo imeishia hapo, hatuwezi tukubali yaishe.
ReplyDeleteKwa sisi tuliopo Tanzania msiba uko wapi huku? Tunaweza kuchangia kivipi kwa urahisi zaidi?
ReplyDeleteNadhani overtime watu wataanza ku-reevaluate mambo ya misiba na kuona kuwa in the future wengi tutazikiwa ughaibuni. Sasa karibia kila mwezi kuna msiba mahali ughaibuni. Hivi kweli tutaweza kufanyia kazi misiba na hali ilivyo mbaya? Mimi nadhani ni cheaper hata kuwatumia wawakilishi wawili watatu nauli toka bongo waje kwenye msiba kuliko kusafirisha mwili wa marehemu. Inabidi tuanze kufikiria haya masuala upya maana kama watu wanaoishi West Coast (California), ni dola at least 12,000 kusafirisha mwili kwenda bongo. Sasa tutayaweza kweli? Nadhani tutumie hekima kidogo na watu huko bongo wanaotegemea mwili wabadili mitazamo kwani haina tofauti yoyote mtu anapozikiwa. Ukifa umekufa tu....!!
ReplyDeletePOLENI NDUGU JAMAAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU HAPA NCHINI NA HUKO NYUMBANITZ .Ndugu yangu wa tue Aug 09. 06:58:00 PM 2011 ,kuzikia America inagharimu $6000 na zaidi ,umeshauri kuwaalika ndugu wawili watatu wahudhurie mazishi tiketi ya haraka haraka ni ghali pia ,yaweza kuwa $1500 . Ninawaasa wote mliochangia tujaribu kuwa na simile tumuogope Mungu kabla hatujaandika chochote.Kitu kimoja cha KUSAIDIA HAPO SIKU ZA USONI NI KUHUDHURIA AU KUWASILIANA NA DACOTA KWENYE KILELE CHA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU,YAPOMASHIRIKA KADHAA YANAYOTOA HUDUMA YA AFYA YA MAISHA KUTOKA NYUMBANI KWA GHARAMA NAFUU,TAFADHALI TUFUATILIE HILO.
ReplyDelete