Brother Michuzi salama?
Waanbie wadau wote ukiwemo na wewe kwamba leo Manchester United ilikuwa ikitoa zawadi ya Eid fitr kwa wapenzi wake palee Old Trafford kwa Kuichabanga timu ya Washika Magobole (Arsenal) bao 8-2.

Nani kama Man Yuuuuuu..........??haha ahha ahha

Maganga One.

Matokeo Mengine ya leo.

Man Utd 8-2 Arsenal
Newcastle 2-1 Fulham
Tottenham 1-5 Man City
West Brom 0-1 Stoke

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu kweli hii ni noma, hakuna daku leo.Hata mechi za mchangani hawafungani hivi. Ila kwa upande mwingine ni safi Wenger may be atasikiliza kilio cha wengi kusajili wazoefu na sio watoto.

    ReplyDelete
  2. tatizo ni wenger na si Arsenal.
    hapa lazima ataaamka na kujifunza.
    natamani afukuzwe akalime kwao Ufaransa.

    ReplyDelete
  3. Hii kitu inaitwa UMITASHUMTA

    ReplyDelete
  4. sina la kusema man uu daima, ila jamani kama tatizo ni huyo mawenge sijui wenger aangalie timu kiupya raha ya mpira kutoana jasho. asernal ni timu kubwa sana huyo wenger wenu vipi jamani?
    ankal makoye man uu tuko pamoja, mshua wangu dunia nzima usijali.

    ReplyDelete
  5. Uwe wa kwanza pia kutuwekea matokeo ya Ligi Yetu ya Nyumbani, tujifunze kupenda vya kwetu asiopenda vya kwake ni mtumwa. Utumwa sio lazima ufungwe minyororo unaweza ukawa mtumwa wa mawazo na kifikra ambao ni mbaya zaidi kuliko hata kufungwa Minyororo !!

    ReplyDelete
  6. WEWE HAPO JUU KWANI TATIZO NINI???MICHEZO NI SEHEMU YA MAISHA MWENZIO YUPO UGHAIBUNI MATOKEO RAHISI KUYAPATA NI YA EPL HAYO YA TUKUYU STARS ATAYAPATA WAPI?MATOKEO YA NYUMBANI AKITUJULISHA MICHUZI INATOSHA.HII NI KAWAIDA KWA WANAOPENDA MPILA KUKEBEIANA IWE NJE AU NDANI/SIMBA AU YANGA.MIMI SISHABIKII MAN U ILA HUYO MDAU HAJAKOSEA HATA KIDOGO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...