Hello wadau ajali hii imetokea mchana wa leo saa saba na robokaribu na sealander brige magari matatu yamegongana chanzo kikiwa ni gari la wagonjwa la manispaa ya kinondoni kufunga breki ghafla likiwa kwenye mwendo wa kasi likielekea Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo kusababisha magari matatu nyuma kumgonga na yenyewe kugongana. Picha Na Mdau Paul |
Home
Unlabelled
mizinga mitatu kwa mpigo...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hapa inaonyesha haya magari yaliyogogana ni wale jamaa wanaopenda kuchukua advantage ya ambulance kukwepa foleni kujifanya nao wako kwenye msafara huo. We utawezaje kuifuata ambulace kwa kasi na kwa karibu hivyo? Hiyo ndio faida ya ujanja mwingi!
ReplyDeletePoleni kama mmetoka salama.Na hilo 'cruza' lilikuwa na mgonjwa au?Atakuwa ameshtuka sana kama alikuwemo.Pili msongamano wa magari Dar unafanya madereva wengi tunasahau umbali wa kuacha kati yako na mwenzio aliye mbele yako.Kama umbali unatosha hata mwenzako mbele akisimama ghafla unakuwa na muda/umbali wa kutosha kuweza kusimama ghafla(Ref.Defensive driving).Dar ukiacha 'Gap' kati yako na wa mbele yako mwenzio anakuja anachomeka kwenye hiyo nafasi!.Nilifanya utafiti kwenye foleni, gari zinaachana 1/2mita hadi mita 1 tu kwa kuogopa 'kuchomokewa'!Ni hatari
ReplyDeleteDavid V
Nakubaliana kabisa na MDAU WA KWANZA. Hii ni tabia ya madereva wa Dar; wanajifanya wajanja; hawajui maana ya kuheshimu magari ya dharura; na pia umuhimu wa kuacha nafasi kati ya gari na gari. Kama gari iliyo mbele yako ikiharibika na umeacha tu sentimita 30 kati yako na mtu wa mbele; na anayekufuata hivyo hivyo; si mtakesha hapo?Madereva wengine hawana ustaarabu.Ukiacha gap kidogo;unapigiwa honi; au kuchomekewa.Hata mtu akigongwa hivi; ndani ya mwezi anarudia yale yale.HATUJIFUNZI. Cha msingi hakuna aliyeumia; na Cruiser 1HZ hard top bado iko shwaaaaaaari. Mnyama huyo!
ReplyDeleteSomo kwa madereva wanaofukuzia gari za Emergency Services; Fire/Ambulance/Police, au hata magari ya kawaida. IT IS ILLEGAL!!!
Quote: TAILGATING is the practice of driving on a road too close to the vehicle in front, at a distance which does not guarantee that stopping to avoid collision is possible. Approximately one third of rear-end collisions involve TAILGATING.
In many jurisdictions this action is ILLEGAL and punishable by LAW