Mjomba Ankal na Wadau,
Asalaam Aleikhum nyote!
Waama baada ya salamu mie ni mzima wa afya, hofu na mashaka ni juu yenu nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu. Msaada nnaoomba mie ni mmoja tu, nao ni kutaka kufahamishwa kinagaubaga mustakabali wa chakula ya usiku katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ambao nashukuru Mola Alhamdulillahi nimeuona na naendelea kuutukuza.
Shida ni kwamba mie ni mwanaume umri wa miaka 32, bado sijameremeta, kama unavyosemaga ankal wadau wanapofunga pingu za maisha. Ni Mwislamu swafi au tusema wa kati maana swala 5 naomba nisiongope, sipigi, ila kila Ijumaa kama ya leo hii sikosi kwenda kupiga mswala, labda niwe naumwa. Tatizo nililonalo ni kwamba nna mwenzangu ambaye panapo majaaliwa tutameremeta mambo yakija kukaa sawa. Kwa sasa siwezi kusema lini, ila twapendana vizuri tu, na ni mwaka wa tatu sasa toka niwe naye na ndugu wa pande zote wanaufahamu uhusiano wetu huu, japokuwa kila mmoja anaishi kwake.
Swala ni kuhusu chakula ya usiku wakati huu wa funga, mjomba Ankal na wadau. Je, twaweza kubwia? Unajua tena mambo yalivyo, nami naabudu sana dini na sitaki kwenda kinyume. Hivyo naomba msaada wanazuoni na wajuvi wa mambo mnielimishe. Mie na mwenzangu twaruhusiwa kula chakula ya usiku nyakati za usiku?
Mdau A.H.A
Mafia Kisiwani
Asalaam Aleikhum nyote!
Waama baada ya salamu mie ni mzima wa afya, hofu na mashaka ni juu yenu nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu. Msaada nnaoomba mie ni mmoja tu, nao ni kutaka kufahamishwa kinagaubaga mustakabali wa chakula ya usiku katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ambao nashukuru Mola Alhamdulillahi nimeuona na naendelea kuutukuza.
Shida ni kwamba mie ni mwanaume umri wa miaka 32, bado sijameremeta, kama unavyosemaga ankal wadau wanapofunga pingu za maisha. Ni Mwislamu swafi au tusema wa kati maana swala 5 naomba nisiongope, sipigi, ila kila Ijumaa kama ya leo hii sikosi kwenda kupiga mswala, labda niwe naumwa. Tatizo nililonalo ni kwamba nna mwenzangu ambaye panapo majaaliwa tutameremeta mambo yakija kukaa sawa. Kwa sasa siwezi kusema lini, ila twapendana vizuri tu, na ni mwaka wa tatu sasa toka niwe naye na ndugu wa pande zote wanaufahamu uhusiano wetu huu, japokuwa kila mmoja anaishi kwake.
Swala ni kuhusu chakula ya usiku wakati huu wa funga, mjomba Ankal na wadau. Je, twaweza kubwia? Unajua tena mambo yalivyo, nami naabudu sana dini na sitaki kwenda kinyume. Hivyo naomba msaada wanazuoni na wajuvi wa mambo mnielimishe. Mie na mwenzangu twaruhusiwa kula chakula ya usiku nyakati za usiku?
Mdau A.H.A
Mafia Kisiwani
Astakafir, astakafi, usibwie ndugu yangu ngojea umeremete kwanza. uwe ni mwezi mtukufu au kipindi chochote kile usibwie mpaka umeremete. MJOMBA.
ReplyDeleteKwa muumin wa dini ya Kiislamu au ya Kikristo, Ni dhambi kubwa kubwia chakula ya usiku kabla ya ndoa. Ni Haram usiku, mchana, Ramadahani au si Ramadahani!
ReplyDeleteKwanza unatakiwa umuombe Allah (S.W) akusameh makosa yako, pili unatakiwa usimamishe sala tano kwani hiyo ni amri ya Allah na hana funga kwa aliyekuwa haswali, na swala hukataza maovu na kuimarisha mema. Kuhusu chakula cha usiku huruhusiwi kula kama hujaowa sio tu kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan bali hata siku nyengine yeyote ile, kwani hiyo ni zinaa na zinaa ni uchafu mkubwa, na yote haya unafanya kwa sababu husimamishi swala. Kwa hiyo kuanzia leo muombe maghfira M/Mungu na tawbat nasuha. Uanze kuswali swala zote tano na suna na uache zinaa, uoe haraka sana ikwezekana hata leo na inshallah Allah atakusameh makosa yako.
ReplyDeleteMijitu mingine bwana...!
ReplyDeleteWe ushasema haujafunga ndoa, alafu unauliza "chakula cha usiku". Hivi huko kuswali kwako kila ijumaa kunakusaidia kweli?
Issue hapo sio mwezi wa Ramadhani... issue ni kuwa hata bila huo mwezi wewe (kidini) ni mzinifu tu, pumbaf yako...!
Mimi ni mkristo lakini najua Uislam unatukemea "tusi-ikurbie zina". Sijui bwana, lakini nahisi una shida na huo Uislam wako!
Sidhani kama Uislam unaruhusu dhambi muda wote, isipokuwa mwezi wa Ramadhani. Kama ni hivyo basi kuna shida huko uliko...! Unawatia aibu waislam wenzako.
Ikimbie zinaa mwanangu, leo na hata miezi mingine!
Huruhusiwi kubwia chakula cha usiku kama HUJAOA AU KUOLEWA kama ni muislam. Kama unataka chakula cha usiku basi haraka sana UOWE AU UOLEWE!!
ReplyDeleteTizama runinga ya chanel ten (CHAN 10)kila siku usiku saa tano hadi saa sita jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa nne hadi tano na nusu jumamosi na jumapili. Kipindi kinaitwa ARRISALLAH sheikh Idd Mohamed Idd atakujibu kama utamuuliza swali hilo. Ila kwa ufupi hutakiwi kula chakula cha usiku kwa mtu asie mke wako wakati wowote ule sio kipindi hiki cha ramadhani tu>
ReplyDeleteKaka Ankal, habari ya kazi?huyu jamaa au Mdau kama alivyosema mwenyewe hapo, labda kuna Dini nyingine zaidi ya Uislam anayo ambatana nayo au kuabudia, Chakula cha Usiku ndio nini!si useme tu wewe matendo yako sio mazuri!!!Tunavyojua sisi chakula cha usiku wakati huu wa mfungo ni Daku (kula daku),wewe kama umeweza kuwa na huyo mwenzio kwa mwaka wa 3 sasa bila kufunga ndoa ni kosa kwa DINI ZOTE,sio Uislam tu, tena ndoa kenye Uislam ndio rahisi zaidi, maana anatakiwa shekh, muolewaji, muoaji, walii wa Mwanamke,na mashahidi, ndoa inapita!!! Ila kama umezoea uzinzi ndio kasheshe, subiria mpk uwe Billionea kama sio Millionea maana siku hizi kila mtu Millionea Bongo.
ReplyDeleteKikubwa nachotaka kukwambia....wewe au nyie wote wawili wazinzi tu hamna lolotee usitake kuwatia dhambi wazazi wenu bure kwa kusema wanajua tabia yako chafu.
Ndio nyie nyie mnachezea mabint wa watu na kuwaacha!!!!!OAAAAA
NI HATARI KIJANA WA KISLAM KUULIZA KAMA ZINAA INARUHUSIWA USIKU WA RAMADHANI ILI HALI UNAJUAA TUMEAMBIWA TUSIAKARIBIE ZINAA KABISA JIEPUSHA NAYO TAFUTA MKE OWA MBONA UNA UMRIFI MKUBWA TU UNASUBIRINI NINI AU WATOTO WAKO WAKUITE BABU
ReplyDeletekwanza kabisa lengo kubwa la mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ni kujifunza au ni mafunzo ya kuepukana na aina zote za maovu. ili baada ya kuumaliza tuwe tayari shule tumeielewa na tuendelee kufanya mema katika miezi mingine hiyo ijayo. hilo ndio lengo kuu la mwezi mtukufu wa Ramadhan. pili ZINAA ni kitu ambacho Mungu amekataza kwa nguvu zote na amesema na wala usiikaribie. sasa mdau naona unataka kujihalalishia. inakubidi UOE (umeremete) then ndio utapata ruhusa ya kula hicho chakula cha usiku na tena iwe usiku. na kwa miezi mingine utakula kama utakavyopenda mwenyewe ila ni lazima awe Mke wako wa ndoa. Usiogope kuoa kijana. Oa ili upate utukufu na uepukane na dhambo za zinaa na ili upande Daraja. hope umenipata. ila kuhusu ZINAA na wala usiikaribie.
ReplyDeleteKwani bila ya mwezi huu wa toba, mnaruhusiwa?
ReplyDeleteAlaykum msalam sk
ReplyDeleteMimi simtaalam sana ila kwa ushauri tu kwanza jitahidi sana usali sala5 kwani bila sala hio funga yako ni bure, na wewe huruhusiki sio mwezi huu tu wa ramadhani kula chakula cha usiku bali hata katika miezi ya kawaida huruhusiki......na kwa masuala yako nakushangaa kidogo kuwa kweli wewe unatoka kisiwani MAFIA na masuala uliyonayo ya KITOTO sana kwani mzaliwa au mkaazi wa mafia yeyote yule suala la dini kama ulilouliza hapa nikusema wewe hutoki mafia
zaidi mombe mungu wako akusaidie na akuongowe katika waja wenye kuishika dini kisawasawa na sio kama wewe unavyotaka kumchuzea mungu, kumbuka tu mungu hakuhitajii wewe funga yako ila wewe unamuhitajia mungu, kwani kuna mamilioni ya watu wanafunga kiilivyo hasa na mungu kukukosa wewe hapungukiwi chochote kile ni wewe ndio mwenye hasara
sasa kama uko na miaka 32 pima akili yako lipi zuri nz lipi baya, usihadaliwe na pumzi.......wako kutoka Mafia,
Huo ni uzinzi na uzinzi umekatazwa na sikatika mwezi wa Ramadhani bali siku zote za maisha yako kama hujaona. Umesema wewe ni muislam safi ulipaswa kulifahamu hili. Nakama umekuwa ukizini hata kabla ya mwezi mtukufu unapaswa kuomba TOBA kwa mola wako. Wallahu aalam
ReplyDeleteSIDHANI KAMA UNAHITAJI MSAADA ILA UNATAKA KUHARIBU SWAUM ZA WATU.TAFADHALI HEBU RUDI KWA MOLA WAKO NA VILEVILE TAFUTA MUDA WA KUPATA ELIMU YA DINI AMBAYO ITAKUSAIDIA KTK MAISHA YAKO.KUSWALI PEKE YAKE HAITOSHI ILA VITENDO PIA NI MUHIMU.UNAJUA VIZURI SANA KUWA MWEZI WA RAMADAHANI NI MWEZI MTUKUFU WA KUTUBU NA IBADA ZAIDI YA KIWANGO CHA KAWAIDA KWA MCHANA NA USIKU.HALAFU NA WEWE UNAJIITA MUISILAMU NA KUULIZA MAMBO YALIO HARAMU (UDHINIFU)KTK MWEZI WA TOBA????
ReplyDeleteTumia common sense. Kama ulikuwa unakula kinyume na taratibu halafu ukaamua kuacha kipindi cha mwezi mtukufu, wakati huohuo bado unatamani kula, haina maana kuacha. Kama umeamua kutubu kipindi hiki cha mfungo basi toba hiyo inatakiwa iendelee hadi hapo mtakapooana. Isipokuwa ndoa si lazima mfanye sherehe kubwa. Unaweza kufunga ndoa chap chap ili iwe halali kwako kutafuna mzigo.
ReplyDeleteAsalam aleykum ndugu yangu,
ReplyDeleteNashukuru kwamba unaifahamu dini ya mwenyezi mungu yaani uislam na unafunga ramadhani.
Dini hiyo pamoja na mambo mengine inakataza ZINAA kwa maana kwamba hamruhusiwi kula chakula cha usiku hadi mtakapomeremeta. Kwa kuwa umefanya mahusiano kwa miaka mitatu sasa, hiyo ni kinyume kabisa. Na kwa kuwa hujameremeta, huruhusiwi kula chakula hicho hata wakati huo wa mfungo. Unashauriwa kufanya mazoezi ili kuondoa njaa ya kula chakula; na pia harakisha kufunga ndoa na huyu umpendae kwani miaka 32 inatosha kabisa kuitwa baba.
Asante, Mfungo mwema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Yaani Braza A.H.A. hapo noma! Sijui Misingi ya Dini ya Kiislam inasemaje juu ya 'kubwia' sosi la usiku kabla ya ndoa-takatifu. Neno Takatifu hapo linamaanisha "iliyo safi, isiyo najisi" nikiwa na maana ya mkishaoana hilo suala linakuwa si najisi tena, na mnaweza kushiriki wakati wowote ili mradi mpate tu muda wa kusali pamoja. Ila ndg yangu, kabla hamjaona hili suala huwa ni "najisi" kulisalandia maana mnakuwa mnatenda "dhambi" Ndio maana kuna wakati mnaibia ibia na kujificha kwa kuwa tendo hilo lisilotakaswa ni "ovu" hata mimba ikinasa, mzee mwenyewe unaweza ukamkana mwenzio ukisema humjui na hujawahi kulala naye, ila mkiwa kwenye ndoa yaani unakuwa na amani na furaha tele na uhakika kuwa mimba ni yenu nyote wawili, kwa nini kwa sababu "alichokiunganisha Mungu ni kitakatifu, halali na ki-safi". Sasa ushauri wangu, naamini Ramadhan inamaanisha "kutembea kwenye usafi yaani utakatifu"...sidhani wala kufikiri kuwa msosi huo utafaa...ila mngekuwa mmeoana ninaamini kuna wakati maalum ungekuwa umetengwa kwa ajili ya chakula hicho. Mimi ni mkristo ila maneno yangu ya Biblia yanasema "Msinyimane, (waliooana) kwa kiingereza (Do not deprive each other except by mutual consent and for a time, so that you may devote yourselves to prayer". 1Corinthian 7:5. Yaani anamaanisha hiki chakula kisiwakoseshe kusali pale mnapokubaliana..hii ni kwa waliooana tu. Kwa wasiooana msosi wa usiku ni "DHAMBI"..Sijui Waislam upande wenu lakini.
ReplyDeleteWacha hizo wewe!
ReplyDeleteUngekuwa unaabudu sana dini ndo ungekaa na KIMADA muda wotw huo bila kufunga ndoa? Sio wakati wa Ramadhani tu bali hata baada ya Ramadhani huruhusiwi kabisa kula hicho chakula cha usiku kwa huyo demu ambae hujafunga nae ndo.
Kwa Faida yako angalia Kipaindi cha ARISALLAH pale Chanel Ten kila siku kuanzia saa 5 mpaka 6 usiku.
Mdau wa Mafia,
ReplyDeleteWacha kutania dini za watu. Hivyo wewe kama mwislam kweli hujui kuwa zinaa ni kosa. Na sio tu mwezi wa Ramadhani hata mwezi wotewote uli katika dunia hii zinaa haikubaliki.
Nakushauri achana na mawazo ya kumeremeta kwa gharama. Hata laki moja unaweza kumeremeta na baadae utajipanga kufanya sherehe. Peleka posa kwa huyo mwenzako na wambie kwa sasa sina mahari, nahitaji ndoa na sherehe baadae. Tatizo liko wapi hapo.
Kama unataka kumeremeta kuaina basi, kubali kuwa zina haikubaliki katika imani nyingi kama sio zote kwa waislamu huruhusiwi kufanya zina hata kama itakuwa lini?
Aidha waislam huwa husali sala 5 na sio ijumaa. Wacha utani uislam hauko hivyo. Kwanini usali ijumaa tu unatania Mungu?
kama nimekupata vizuri unasema hamjaoana,ndugu yangu hairuhusiwi ila kama mmefunga ndoa ni rukhsa.Quraan surat baqra aya 187 mungu anasema:MMERUHUSIWA USIKU WA SWAUMU KUINGILIANA KIMWILI NA WAKE ZENU.WAO NI VAZI KWENU NA NYINYI NI VAZI KWAO.M/MUNGU ANAJUA YA KWAMBA MLIKUWA MKIZIKHINI NAFSI ZENU.KWAIO AMEKUKUBALIENI TOBA YENU NA AMEKUSAMEHENI.BASI SASA CHANGANIKENI NAO NA TAKENI ALIOKUANDIKIENI M/MUNGU.NA KULENI NA KUNYWENI MPAKA UBAINIKE KWENU WEUPE WA ALFAJIR KTK WEUSI WA USIKU.WALA MSICHANGANYIKE NAO,NA HALI MNAKAA ITIKAF MSIKITINI.HIYO NI MIPAKA YA M/MUNGU,BASI MSIIKARIBIE.NAMNA HIVI M/MUNGU ANABAINISHA ISHARA ZAKE KWA WATU ILI WAPATE KUMCHA...La msingi hapa funga nae ndo then chakula cha usiku utakula kwa amani bila khofu.
ReplyDeleteHuwezi kula chakula cha usiku hata siku moja mwezi mtukufu na mtu ambae hamjafunga nae ndoa, mana tangu na hapo mnadhini miaka mitatu yote hyo jiandae na la kujibu kesho kwa m'mungu, mna subiri nini kufunga ndoa ili hali hali ndoa zetu za kiislamu hazina tabu ya mkeka umemaliza km unataka masherehe ni wewe tu.
ReplyDeleteKwa ushauri zaidi angalia kipindi cha Arrisala cha Channel Ten kila siku jtatu hadi jmosi wanaanza kuanzia saa tano usiku hadi saa sita na jpili saa nne usiku hadi saa tano, kwa mwezi huu wa ramadhani baada ya ramadhani huwa kina rushwa hewani kila jpili kuanzia muda huo huo niliyokutajia hapo juu, na huwa kina kuwa live, nadhani utajifunza mengi sana.
Kwa ushauri wangu vumilieni tu mwezi mtukufu uishe kisha muendele na kudhini km kawaida.
Achana na zinaa si tu katika hiki kipindi cha mfungo wa mwezi Ramadhan bali muda wote. Kama unampenda basi fungeni ndoa na muwe mke na mme na sio kula chakula ya usiku kwa kutenda dhambi!
ReplyDeleteMdau A.H.A,
ReplyDeleteWaalaikum. Dude...you're kidding right?!. 32 years old unauliza kama kufanya zinaa, tena mwezi wa Ramadhan inafaa!!.
Kwanza umeuliza swali lako sehemu isiyofaa. Mtu yoyote anaweza kujiita muislam au shekhe na akatoa jawabu lenye kupotosha. Kwahiyo swali lako lipeleke kwa Imam aliyesomea dini msikitini.
Kaka michuzi quality ya posts zako inashuka katika alarming rate. Yaani kweli unaruhusu kitu kama hiki kuwa posted humu kweli. Mtu gani wa miaka 32 anauliza swali la namna hii. Kama nia ni ku-provoke watu bwana AHA sina la kusema. Ila si kila swali lapaswa kupostiwa huku. It shouldn't have been posted here.
Halafu mzee Michuzi hilo tangazo la Ndovu "liquid gold" kaka halifai kuwekwa na muislamu. Unabeba madhambi kebe kebe kwa kupromoti maasi ndugu yangu. Huu ni ushauri kwa upendo...liondoe tangazo hilo. Allah is watching you Muhidini Issa Michuzi.
TAFADHALI!TAFADHALI SANA USISUTHUBUTU HATA KUMKALIBIA MAANA NYIE HAPO MNAFANYA ZINAA...
ReplyDeleteAsalaam aleiykum,
ReplyDeleteMungu amekataza zinaa nadhani hilo ni jibu tosha kwako.
Ramadhan kareem.
yaan unathubutu kusema wewe muislm swafi?tena husirudie wewe ni chafuu!!!!!huruhusiwi hata cha mchana nini cha usiku, wewe huyo hata kumgusa hutakiwi sasa unaulizia cha usiku inamaana umeshachakachua sana then umwache,nasisitiza uruhusiwi hadi mfunge ndoa au mmeremete tu, zidi kutubu sana maana umeshachakachua bila ruksa!wewe ni bongo flaver au bongo movie?
ReplyDeleteyaan ndugu yangu hata kabla ya mwezi mtukufu wa ramadhani huruhusiwi,zinaaaaaaaaa hiyo mwanawane,fungeni ndoa hata ya mkeke basi
ReplyDeletewewe kama ni muislam safi ungelijua hili.ni haramu tena haramu si hii ramadhani hata siku za kula mchana.haaa umenishangaza sana maana waislam kuna vitu huwa hata kama hujasoma dini sana lakin lazima ufundishwe.kweli unasali sala tano kama ulivyosema??!!! ama unafurahisha baraza na kutaka kuharibu swaumu yako na za watu waliofunga kuzungumzia zinaa mchana wa mwezi huu..
ReplyDeleteIkiwa wewe una imani kweli na dini yako ya kiislamu na unampenda mwenzio basi INABIDI muoane. Mambo ya chakula cha usiku au mchana kabla ya ndoa ni HARAMU
ReplyDeleteCHAKULA RUKSA,,KAMA NI MKEO HALALI ULOPEWA NA MUNGU HAPO HAKUNA DHAMBI...WEE UNATAKA UFUNGE MPAKA NDOA JAMANI HEBU MUELIMISHENI KIJANA HAPO JUU...UKIFUNGA VYOTE WAPO WATAKAOKUSAIDIA KUFUNGUA SHAURI YAKO A.H.A...
ReplyDeleteNaamini somo limekuingia,
kula kwa nafasi...
mdau toka -ARUSHA GOLIONDOI.....JK...GLOBAL RATED
Zinaa ni kharam kwa mwislam yoyote yule. Unachofanya wewe sasa ni kuzini na mwenyezi mungu anachukia zinaa. Hutakiwi kumgusa huyo mwanamke either iwe mchana au iwe usiku mpaka umuoe.
ReplyDeleteTafadhali acha masihala na mzaa kwenye mambo ya mungu. Sura ya 2 aya ya 187 mwenyezi mungu anasema "Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha."
Mwenyezi mungu anaanza kwa kusema mmehalalishiwa usiku wa swaumu kuingilia wake zenu. Na sio VIMADA WENU, AU Mashangingi Wenu au Wakora wenu, BALI WAKE. Sasa wewe leo unakuja kuuliza kama kuzini usiku wa ramadhani ni halal?
Please stop this madness.
Mdau wa USA- Rick Perry for President.
Chakula cha usiku huruhusiwi siyo mwezi huu tu mtukufu bali siku zote mpaka hapo mtakopomeremeta.
ReplyDeleteYaani baada ya miaka mitatu ndio uulize leo na hapo hapo unasema wewe ni mtiifu wa imani, ina maana ulikuwa unafanya nini mifungo iliyopita? Pili, neno "mustakabali" linamaanisha wakati ujao (future), kwa hiyo wewe umelitumia hapa kwa maana gani? Tatu, ni vema umuulize Shekhe au imamu wako maana hilo ni suala zito na humu utaambulia kuchanganyikiwa zaidi, endapo swali lako ni la dhati.
ReplyDeletejibu ni kwamba HUWEZI kubwia hadi uwe umeremete kwanza. acha tamaa
ReplyDeletekwani hiyo miaka mitatu mliyokuwa wote ulikuwa unafanyaje? na miaka mitatu yote unam-date tu na kumpiga tarehe
Ndugu yangu mdau katika iyman ya dini ya kiislam, kwa taarifa yako ni kuwa hata hiyo miezi ya kawaida wewe na huyo mtarajiwa mwenzio hamruhusiwi hata kuonja chakula hicho hadi siku mtakayomeremeta rasmi. Adhabu yake ni kali sana siku ya hukumu ikifika.
ReplyDeleteNakushauri utenge muda angalau mfupi umuone imam au kiongozi mwengine yeyote wa dini yetu ili akufafanulie kwa undani zaidi.
Pia usisahau kuwa Mafia kwa sasa ni wilaya ya 4 ikiongoza kwa "mdudu" kitaifa hivyo kuwa makini.
Nkonongwa, safarini Koma Kisiwani.
Hebu wewe mtu 'KUA'; maana unaonyesha kwamba bado mtoto katika mambo ya Dini na Kufikia hatua ya kumeremeta.Pengine umekua KIUMRI lakini akili bado haijatanuka; kama ya mtoto wa Primary.
ReplyDeleteNasema 'hujakua' maana sidhani kama hilo ni swala la kuleta kwenye blog. Kama unatambua maana ya dini; pia utajua maana ya Kiasi; na pia utatambua maana ya kuwa katika ndoa.Kwa mtu anayetambua hayo;wala hawezi kuuliza maswali kama hayo kwenye umati;kwani wanategemea mtu akisema .Naamini dini, na nafuata dini' basi majibu yanakuwa 'obvious'.
Tunaomba Michuzi uwe unaweka mada zinazoeleweka hapa; topic kama hizi ni kujaza tu nafasi kwenye blog ya jamii
Mdau
Walek salaam kaka swali zuri sana na litaelimisha wengi pia ambao wako na situation kama yako kaka bora tu usubiri mpaka mwezi huu mtukufu upite, kama ingekuwa mmeshaafunga ndoa hii ni ruksa kabisa tena hata ukihitaji pale muazini akiazini tu mkeo ana haki kabisa ya kukupa, kwa hiyo si ruksa mpaka mfunge ndoa ndio imehalalishwa kwa dini yetu ya kiislam inavyotuambia na utaharibu mfungo wako pia vumilia tu kaka mwezi mmoja si mrefu na hata romance pia hurusiwi kwa kuwa utakuwa unaikaribia zinaa pole sana na kuwa na subra ili uchume thawabu zako. Mdau mkubwa wa glob hii wa Oslo Norway.
ReplyDeletenimefurahishwa na hofu yajo juu ya ALLAH kwa kujizuia kufanya maaswi lkn kaa ukijua ZINAA ni haram muda wote iwe ramadhan au la.unachotakiwa ni kufunga ndoa ambayo ktk UISLAM ni rahisi sana anahitajika muoaji,muolewaji,walii(mtoaidhini)na mashahidi 2 waadilifu kuhusu mahari mtapanga wenyewe na sherehe sio lazima inategemea uwezo wako.jitahidi kufanya ibada kikamilifu kwani kuswali ijumaa pekee si mafunzo ya mtume wetu
ReplyDeleteNdugu yangu, wa alaykum salaam!
ReplyDeleteKuhusu ulivyooomba maelekezo yako , jawabu ni kuwa Uislamu hauruhusu kwa namna yoyote ile kufanya tendo la ndoa pasipo na ndoa, Iwe ni mwezi wa ramadhani au mwezi wowote ule.Allah anatuambia kuwa tusikurubie zinaa, hakika zinaa ni uchafu. Kukurubia zinaa ni kuikaribia zinaa kwa namna yoyote ile yaani kufanya matendo ambayo yatakupelekea kutenda zinaa. Sasa kuna waislamu walio wengi wananadhani wanatakiwa kujiepeusha na mwezi huu wa ramadhani tu na hivyo baadhi yao utakuta wanatengana na vimada wao muda huu wa ramadhani na kurejea kuushi pamoja baada ya mfungo kuisha. Jambo hili si sahihi hata kidogo. Mungu unayemwogopa wakati wa ramadhani ni yule yule anayepatikana katika miezi mingine. Ukiwa unafanya hivi basi utakuwa unaabudu mwezi badala ya Allah. Na hiyo ni shirki kubwa kabisa. Ni ALlah peke yake ndiye anapaswa kuabudiwa kwa haki wakati wowote ule. Allah anatufahamisha ya kuwa lengo la ramadhani ni kumfanya mja awe mchamungu kwa maana ya kuwa matendo unayojifunza ukiwa ndani ya ramadhani unatakiwa uyatekeleze pia ndani ya miezi na hapo ndipo lengo la swaumu litakuwa limetimia na kinyume chake ni kutwanga maji kwenye kinu yaani unaoga kwa maji safi kisha unakwenda kujigalagaza kwenye matope!
Kwa kifupi unachotakiwa kufanya ni kuoana na huyo bibiye na kisha kuishi pamoja, hapo ndipo utakuwa unapata radhi za ALLAH.
Na Jambo lingine ninakuhusia ndugu yangu katika kumcha ALlah kwa kusimamisha nguzo zake. Kwani Swala ni nguzo katika uislamu, na mwenye kuacha swala hakika amekufuru!
Tumuombe ALLAH atujaalie kuwa waja wake wema na atufanye tuwe miongoni wa wanaomwabudu yeye tu na siye mwezi wa ramadhani. Amiin
Wabillah Tawfiq.
Mudy.
chakula ya usiku ni halali kwa wenye ndoa tu.iwe mwezi mtukufu au la! vinginevyo unachuma dhambi kwa kwenda mbele..
ReplyDeleteWE JAMAA NIAJE UMESHAAMBIWA MWEZI MTUKUFU NA UNASEMA UNAENDA KUSALI KILA IJUMAA INAMAANA HUJUI KAMA KUFANYA HIVYO UNAENDA KINYUME NA MWEZI MTUKUFU??? KWANI UKIVUMILIA MWEZI UKAISHA INAKUAJE ACHA SNEMA BANA...
ReplyDeleteMiaka mitatu katika uhusiano? Unangoja nini? Huoni kama unamchelewesha tu mtoto wa watu?Unakula vyote halafu hutaki kufunga ndoa unasubili nini? au ndo unataka kumsusa baadaye?Kwanza unaiba tu hicho chakula cha usiku, halafu unataka kukufuru mfungo kwa mtu asiye mke wako.
ReplyDeleteUshauri, tafadhali usimcheleweshee maisha binti wa watu amua haraka kufunga ndoa, la sivyo kama humpendi au hujaridhika naye mwachie aendelee na maisha kuliko kuendelea kuendekeza ngono pasipo halali halafu unathubutu hata kuja kutafuta ushauri humu jamani.Miaka mitatu ni mingi sana,hata kama ni kujiandaa bado huo muda ni mrefu mno.mambo mengine mtayamaliza mkiwa pamoja.Usithubutu kula hicho chakula kuanzia sasa hata baada ya mfungo kuisha.
Ndugu yangu uliejiita muislam wa kati kwanza napenda kukupongeza kwa kuuliza,maana aulizae ataka kujua,nami kwa elimu yangu ndogo ya dini ya kiislamu naomba nikupe darasa kidogo. kwanza kwa kujiita muislamu ulitakiwa utambue kuwa uislam ni mfumo wa maisha ambao mwanadamu anatakiwa aishi akiwa dunia na kesho akhera atalipwa kwa mujibu wa amali zake alizochuma akiwa katika kituo hiki cha duniani(vituo vingine ni tumboni mwa mama na kwaburini ila vyenyewe havina amali za kuchuma! kwa kuwa ni mfumo wa maisha Allah swt alituleta waislamu muongozo wa namna ya kuishi na kupata hizo amali njema pamoja na kuepukana na mambo mabaya,muongozo huo ni kitabu kitakatifu cha Quran,na kama ilivyo kwa vitabu vingine vyooote huwezi jua kilichomo ndani ya kitabu pasi na kukisoma(ima kusoma mwenyewe ama kusimuliwa). kwa kutambua hilo Allah kupitia kwa mtume wake Mohammad(SAW)aliutaka umma wake wote wasome(waitafute elimu kwanza),kwa maana nyingine huwezi kuwa muislam bila elimu,na uislamu hauji kwa kuzaliwa na wazazi waislamu,uislamu husimama kwa kusoma ili uelewe uislam ni nini unakubali nini na kukataza nini! kukusaidia uislamu una nguzo kuu tano(kutoa shahada ya kuwa hakuna mola wingine wa kuabudiwa isipokuwa yeye Allah SWT na Mohammed ni mtume wake,2:kusimamisha swala 5, 3:kutoa dhaka, 4:Swaum ya Ramadhan 5:Hija) hizi nguzo tano ni faradhi(lazima kwa kila aliye muislam na usipafanya hayo unapata madhambi na unakuwa umetoka katika uislam) na si sunna. Nadhani mpaka hapo nitakuwa nimekujibu kiasi,kwa kutokuswali kwako swala 5 ww haomo katika uislam na utakuwa na la kujibu mbele ya Allah SWT siku ya kiama,lakini kwa kuwa Allah SWT ni mwenye kusamehe bado unanafasi ya kusamehewa kwa kutenda yaliyo sahihi na ndio maana Allah akaleta funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuufanya umma wake umrejee kufata aliyoelekeza na kukatazika na aliyoyakataza,ndio maana unaona mwezi huu dada zetu wanajihifadhi kwa kuvaa vizuri,walevi hawanywi pombe,wazinifu kama ww mnataka kujua zaidi na wengi wao hawazini so sio kwamba hawajui kuwa waliyokuwa wanatenda ni katika yaliyokatazwa la hasha,Ila ni kwa kupitiwa na shetani ama kibur,sasa mwezi huu ni wa kuwarudisha darasani. Na ili uone dalili ya funga yako kupokelewa uantakiwa Ramadhani ikiisha uendelee kama ulivyokuwa ndani ya mwezi mtukufu yani kutenda mema na kukatazika na mabaya la ukiona baada ya Ramadhani unarudi kumuasi Allah basi ni utakuwa ni kati ya wenye kushinda njaa tu na Allah hatakuwa na haja ya funga yako. Kumalizia ningependa kukwambia hicho unachoita chakula cha usiku kina sharti zake kuliwa na kubwa lazima kuwe na ndoa, na laiti ungekuwa na Ndoa nadhani hata hili swali lako usingelileta hapa kwa namna Allah alivyotufanyia wepesi kwenye mambo ya kheri. Ndugu yangu acha zinaa na tangaza ndoa,bado unaweza kuoa ndani ya mwezi wa Ramadhan na kutubia kwa Allah akusamehe madhambi yako yaliyopita huku ukijutia na kuadhimia kutorudia tena. Wabillah Tawfiq Wasallamu Aleyka W'Wabaraakat
ReplyDeleteNDUGU YANGU KWANZA MUISLAM AMEKATAZWA USIKARIBIE ZINAA SASA WW UNAFANYA ZINAA NDUGU YANGU MUOGOPE M,MUNGU HUU MWENZI WA RAMADHANI NI MZURI KWETU KUTUBU MAKOSA YETU KUMBUKA MAUTI YANAWEZA KUKUTA WAKATI WOWOTE ISHI KISLAMU FUATA MAAMRISHO YA QURAN,IOGOPE SIKU YA KIYAMA HALITAKUFAA JAMBO LOLOTE ZAIDI YA MATENDE MEMA NA KAMA UMEACHA MABAYA ZINAA ULEVI KAMARI NA MENGINEYO,
ReplyDeleteCHANGANUA AU JIBU MWENYEWE KWA KUTUMIA AKILI. HALAFU USIJIPAKAZIE KTK UISLAM, WEWE BADO SANA KUWA MWISLAM MAANA KAMA UNGEKUWA MWISLAM ILE KUSWALI IJUMAA MPAKA IJUMAA UNAVYOFANYA JAPO HAIKUBALIKI TAYARI UNGEKUWA UMESHAPATA JIBU SIKU NYINGI SANA. INAVYOONEKANA HATA HIYO IJUMAA HUENDI NDIO MAANA UNAULIZA MASWALI YASIYOHITAJI KUFIKIRIA ILI KULIJIBU...PIMA SWALI LAKO NA MAJIBU YALIYOTOKA NDO UTAJIJUA UKO UPANDE GANI KAT YA WENGI....TUBIA SWALI, FUATA SHERIA ZA MUNGU BADO UNAYO NAFASI...OMBA DUA SIKU ZOTE UFE HALIYAKUWA NI MUISLAM MUUMIN KWA FAIDA YAKO HUKO UENDAKO/TUENDAKO
ReplyDeletenenda alhidaaya.com ukaulize huko
ReplyDeletemdau wacha kumchezea mungu achana na mambo ya mikasi fanya umeremete kwanza alafu ndio uzame huko chumvini
ReplyDeletemambo ya ngono yamekatazwa swahiba khaaaa!!!
Shame shame on U kama wazazi wote wanajuwa kwa nini msifunge ndoa!Ee wewe unajiita mwislam kweli hujui kama zinaa ni haramu kwa Dini zote mbili,,lakini nina wasiwasi maelezo yako I dont think U r a Muslim,,unataka tu uwachemshe Waislam!Pengine huenda huyo kimada wako ndo Muislam unamuulizia tu sheria!Anyway hata kama ni Kristian,,,,Kuzini wewe ni Kuni ya Jahhanam,,,na wengine wote wanaozini Achani kuziiiini Ni Haramu jamani,,,Ukizini unakuwa umeivua Imani yako je ukitoka hapo Mwenyezi Mungu akakutoa Roho Je Utafanya nini?Maana siku ya kufa wote hatujui,,ni Haramu iwe Ramadhan au sio Ramadhan,,,Na mtu kuoa Dini Nyingine pia ni kama mnazini ttuuuu
ReplyDeleteAhlam UK
kuuliza si ujinga na weye wataka kujua ila cha umuhumu hapo ni kungojea mana uislamu hamfanyi mtu kuikaribia zinaa hata siku moja na si ramadhani tuu hata iyo miezi mengine hauruhusu na weye ivo kujita muisalam u safi maana yake nini? wakaana mwanamke miaka mi3 hujamnusuru tu wangoja nini hapo kumnusuru namanisha kumuoa jamani nieleweke vizuri,
ReplyDeletefabya umnusuru ishatodha icho kipindi muitacho uchumba
wa
wallaahu aalam
naitwa taalib ahmed wa wete pemba
Jibu ni hapana huruhusiwi, chakula cha usiku kama ulivyoita mwenyewe, kwasabu bado hujameremeta, siyo tu wakati huu wa ramadhani bali pia wakati usio wa ramadhani mpaka mmeremete. Ok.
ReplyDeleteYAANI WATZ MNASIKITISHA KAULIZA SWALI
ReplyDeleteNIMESOMA SOMA KWAKUDOKOA ILA SIJASOMA MTU ALIYEANZA KWA POINT NZURI NA KUSEMA KAMA
NI HIVI WAKATI WA RAMADHANI UKIWA MUME AU SIO
NI HIVI WAKATI HATUKO KWENYE RAMADHANI UKIWA MUME AU SIO - KUMUELIMISHA ZAIDI.
FULL STOP
MMEONGEA NYIE MAJIBU MIA MBILI KWANI KAWAOMBA USHAURI WA KUMSOMEA DINI NI NINI? AMESHASEMA ANAJIJUA MAKOSA YAKE NA JINSI ANAVYOFATILIA DINI SASA NYIE NINI KUDAKUA HUMU KAMA VILE KASEMA ANATAKA USHAURI WA MAPENZI
NA UTAZANI NYIE WOTE HAMJALA CHAKULA CHA USIKU KABLA YA NDOA. ACHENI DHAMBI KUJIFANYA WATAKATIFU
MDAU XTIAN
Ankal Umebania maoni yangu maana nilikua nimempania sana huyu Mjinga analeta utani kwenye safu kama hiii. akatafute blog za- mtaani maana kwa ukweli hana nidhamu na naweza kusema amewadhalilisha sana waislam.
ReplyDeleteSiku njema