NA NAFISA MADAI - MAELEZO,ZANZIBAR.

Katika kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana,serikali ya mapinduzi ya zanizbar imeandaa mpango mathubuti wa kutatua tatizo la ajira kwa vijana wa unguja na pemba ili waweze kujikimu kimaisha katika shughuli zao za kila siku.

kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa wizara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana wanawake na watoto fatma gharib bilal katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana dunia ambapo zanzibar kitaifa yalifanyika katika ukumbi wa salama hall bwawani.

amesema mpango wa huo wa serikali itakua ni chachu ya maisha kwa vijana hao kwani imekusudia kuandaa sera ya mafunzo kazi, vituo vya ujasirialimali kwa Unguja na Pemba pamoja na mifuko ya vijana kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa vijana.

aidha alisema serikali kwa kuona umuhimu wa vijana kwa makusudi imeunda wizara ya uwezeshaji ili iweze kubuni mbinu za kuwakwamua vijana kiuchumi na kuweka kituo maalum cha kuapata habari za ajira na masoko kwa biashara zitakazozalishwa na wajasirialimali.

katibu huyo alieleza kuwa vijana ndio rasilimali kuu ya kuleta maendeleo kwa taifa ndio maana serikali ikaamua kumshirikisha kijana kikamilifu katikakuleta maendeleo yake na ya nchi kwa ujumla.

aidha alisema mbali na jitihada zinazofanywa na serikali bali kuna mashirika mbalimabali ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali yanafanya juhudi kubwa za kuwakwamua na kuleta maendeleo kwa vijana yakiwemo, ILO,ubalozi wa Norway,UNFPA, UNICEF, UN HABITAT na mengine ambayo yana lengo kama hilo.

akitaja twakimu ya vijana kwa upande wa zanzibar katibu huyo amesema zanzibar ina asilimia kubwa ya vijana wapatao 449,586 sawa na asilimia 34.2 amabapo 219,331 ni wanaume na 230,255 ni wananwake ambapo alisema kundi hili la vijana linakabiliwa na changamoto mbali mbali.

akitaja changamoto hizo katibu alisema ukosefu wa ajira, afya ya uzazi, ukimwi na madawa ya kulevya ambapo alisema imesemekana kwamba tatizo la ukosefu wa ajira kwa zanzibar ni asilimia saba.

akizungumzia janga la ukimwi amesema ukimwi umeathiri sana rika ya vijana na twakimu zinaonesha kuwa asilimia 10.1 ya vijana waojiuza miili yao, asilimia 12.3 ya vijana wanaofanya ngono kinyume na maumbile na asilimia 1.1 ya vijana wanaojidunga sindano wameathirika na virusi vya ukimwi.

mapema akisoma hotuba katika maadhimisho hayo mwakilishi kutoka UN HABITAT tanzania bwana Philomon Mutashubirwa kwa niaba ya katibu mkuu mwandamizi wa umoja wa mataifa dk Joan Clos amesema athari za mtikisiko wa uchumi bado ni nzito kwa mamilioni ya watu wanaoishi katika umaskini uliojikita katika makazi duni ndani ya vitongoji vya mji duniani kote.

amesema kuwa kutokana na hali hiyo ina maana kwamba miji yote inapashwa kuwa ni maeneo yenye fursa kwa vijana ili yawasaidie kujikwamua katika janga la umaskini na waweze kujikwamua kimaisha.

aidha alisema katika dunia ambapo zaidi ya nusu ya wakazi wotewanaishi mijini, na wengi ni vijana wanahitaji kuhakikisha kuwa miji ni salama, imetokana na umaskini ni endelevu na pia ilipangwa kwa ajili ya wote.

hata hivyo amesema UN HABITAT inatambua umuhimu wa kukuza uwezeshaji na ushirika wa vijana katika juhudi za kubadilisha mazingira ya mji kwa njia ya mafunzo ya ujasirialimali, mafunzo ya uongozi bora, maafa na usimamizi wa majanga na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na utoaji wa mikopo ya fedha kwa vikundi sita vya vijana ambao waliomba mikopo kwa ajili ya kuzifanyia miradi mabalimbali ambayo itaweza kuwakwamua kimaisha kwa masharti maalumu.

chimbuko la siku hii limetokana na waheshimiwa mawaziri wanaoshughulikia maendeleo ya vijana katika mkutano uliofanyika Lisbon nchini Ureno mwaka 1998 kwamba kila ifikapo 12 agosti iwe ni siku ya kimataifa ya vijana na mwaka 1999 umoja wa mataifa ulipitisha rasmi azimio hilo na bara la afrrika lilianza rasmi kuadhimisha siku hii kuanzia mwaka 2000, na kauli mbiu ya mwaka huu '' VIJANA LAZIMA WAPEWE FURSA ILI WAWEZE KUHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UTOAJI WA MAAMUZI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA, TAIFA NA KIMATAIFA.''

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...