Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (kulia) akipata maelezo katika kibanda cha Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) Bungeni mjini Dodoma kuhusu mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo, ikiwa ni pamoja na mafao ya elimu ambapo mwanachama aliyechangia kwa zaidi ya miaka mitatu endapo atafariki dunia, watoto wake wanne watasomeshwa hadi kiwango cha kidato cha nne. Wabunge waliisifia sana PPF kwa kuwa na mafao hayo na kuiomba iangalie uwezekano wa kuongeza wigo wa elimu unufiashe watoto hadi kidato cha sita na hadi Chuo Kikuu. Katika banda hilo la maonesho jumla ya waheshimiwa wabunge 13 walijiunga hapo hapo, ambapo zaidi ya wageni 300 walitembelea.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. Willia Erio (suti ya kijivu) akiwa na wafanyakazi wa mfuko huo bandani hapo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio kwa kazi nzuri inayofanywa na mfuko huo
Waziri wa Nishati na Madini Mh William Ngereja akiwa na Bw William Erio
Waziri wa Ardhi na Makazi Prof Ann Tibaijuka (kati) na Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee wakimpongeza Bw. William Erio
Hongera sana PPF kwa kazi nzuri
Waziri wa Fedha na Uchumi akipena mikono na Bw William Erio
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt Mary Nagu wakimpongeza Bw William Erio
Mh Martha Mlata akimpongeza Bw. William Erio
Mmoja wa waheshimiwa akijiandikisha kujiunga na PPF Bungeni Dodoma
Nakuona mdau Justin Kassara ukiwa unamwega sera na kufanikiwa kuandikisha waheshimiwa 13 Mungu akubariki sana jitihada zako tunazitambua tokea ulipozindua mpango wa wanachama kuweza pata taarifa za michango yao online pale saba saba mpaka ilipozaliwa PPF TAARIFA ambayo ni zao la online statement,sisi wadau wa hifadhi ya jamii tunatambua hilo na daima tuko nyuma yako tukikuunga mkono. NSSF tunalitambua hilo pamoja na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii,endeleza jitihada zako wigo ni mpana na sisi tunahitaji vijana wenye damu changa wanaojituma maofisini.
ReplyDeletemimi ni mmojawapo nilowahi bahatika kufika PPF makao makuu kweli Justin Kassara ni kati ya wafanyakazi wanaojipambanua katika utendaji wake wa kazi, claim yangu ilikaa miezi mitatu ikidaiwa hakuna michango yangu ila ilo suala lilipofika kwake maramoja alilifanyia kazi na niliweza kulipwa mara moja.Hongera Mr. William Erio kuwa na vijana bora kama hawa wanoweza kufanya kazi kwa ufasaha na uadilifu mkubwa sisi wadau wa Geita mining tunakushukuru sana endeleza gurudumu...
ReplyDeletemdau apo juu umesema kweli uyu bwana Justin Kassara ni kiboko mimi nilibahatika kumuona pale kwenye maonesho ya saba saba haliweza kuupigania vizuri sana mfuko wa PPF mpaka ukashika nafasi ya pili kwa huduma bora pamoja na udhaifu mkubwa unaojionyesha kwenye huu mfuko uyu bwana aliweza jibu vizuri sana maswali tuliyomuuliza hasa hasa nini stahiki yetu kama wanachama wa PPF.
ReplyDeleteMdau Chuokikuu...
Ni kweli kabisa ata mimi nilibahatika kufanya kazi na kassara apa hazina ya kuhakiki madeni yanayopashwa lipwa apo PPF uyu kijana yuko makini sana kwani mwanzoni tulipata shida sana kwani wengi wa wafanyakazi tuliopewa tufanye nao hawakua na msaada lakini pindi uyu bwana alipokuja mambo yetu yalikwenda vizuri na zoezi likawa jepesi kwani mwanzoni kazi ilikuwa nzito ivyo tunampongeza aendeleza bidii...
ReplyDeleteMdau
Hazina!
Tunaupongeza mfuko wa PPF kwa kutuletea huduma bungeni na mimi nilibahatika kukutana na kijana kassara kweli aliweza nilidhisha na aina ya huduma zitolewazo na PPF alionekana kufahamu shughuli za mfuko wa PPF
ReplyDeleteHii ni Kutaka kujionyesha ni Mtu safi huyu Bwana Erio Ana Kashfa Kibao anataka kufanya Publicity ili aonekane ni Mtu safi na Bora!! Ila utendaji ni Kitu Muhimu katika shirika lolote na sio Ufisadi
ReplyDelete